Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?

Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?

Katika sheria ambazo ni ngumu kueleweka hata kwa wanasheria wengi ni PUBLIC INTERNATIONAL LAW. Ubaya zaidi linapokuja suala zima la mikataba ya kimataifa ndiyo mambo yanazidi kuwa makubwa kwasababu kipengele ambacho kinahusika ni THE LAW OF TREATIES, kama umesoma sheria utafahamu kwamba hii ni mada ngumu na ndefu mno kama ilivyo THE LAW OF THE SEA.

Linapokuja suala zima la uwekezaji ndiyo mambo yanazidi kuwa magumu zaidi kwasababu mada ambazo zinahusika sana ni THE LAW OF TREATIES, INVESTMENT LAW, DISPUTE RESOLUTION. Unaweza kukuta mtu kasoma PhD ya sheria lakini hizi mada bado haziwezi. Ndiyo maana hata ukija hapa Tanzania wanasheria wanaofanya INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION ni wachache mno.

Kuweza kuelewa vizuri ule mkataba inahitaji uwe zaidi ya mwanasheria. Inahitaji kwanza kabisa uifahamu vizuri PUBLIC INTERNATIONAL LAW, bila hivyo utaingia chaka. Tafasiri za vifungu vya sheria za kimataifa hasahasa mikataba (Treaties), ni tofauti kabisa na tafasiri ya kwenye mikataba ya kawaida (Contracts). Kuna mambo kadhaa wa kadhaa ambayo kifalsafa mwanasheria anahitaji kuyafahamu kabla ya kuanza kutafasiri vifungu vya mkataba kama ule wa DP World.

Sasa ndugu zetu wametafasiri wenyewe, sijui tafasiri zao wamezitoa wapi. Leo hii mambo yamelipuka vibaya mno. TLS wamekuja na tafasiri yao, AG yuko na tafasiri yake, SPEAKER yuko na tafasiri yake, BUSH-LAWYER MBARAWA naye yuko na tafasiri zake. Kiufupi ni vurugu mechi tupu. Nchi za wenzetu suala kama hili lingekuwa limefanyiwa mjadala mpana, huenda hata kupelekwa kwenye mahakama ya katiba uli kupatiwa ushauri. Huku wanazima mjadala kwa nguvu.

Binafsi waache wanasheria wajadili hoja ili tufahamu nani ameliingiza taifa chaka....
Kwa uelewa wako wa Law of Treaties agreemet kati ya nchi na DP world ( kampuni) inahitaji ratification?
 
Hili wasingelikubali kwasababu wangetakiwa kwanza kupewa kitu kiitwacho A CERTIFICATE OF COMPLIANCE na kusajiliwa kama kampuni la Tanzania kule BRELA. Kule Uingereza DP World wamesajiliwa kama DP World London Gateway, hivyo wanakuwa chini ya msajili wa makampuni ya Uingereza. Sisi huku kwetu hawajafanya hivyo kwasababu wanafahamu fika, wakifanya hivyo itakula kwao. Unakumbuka yale ya bwana Aliko Dangote na Mzee Chuma ???

Tanzania na Nigeria hatukuwa na BIT wala IGA, ila mzee wa watu akaja akawekeza hivyo-hivyo kwa kupewa ahadi kibao na Mzee Jakaya. Kampuni lake likapewa A CERTIFICATE OF COMPLIANCE, sasa alipokuja kukosea na kuonekana baadhi ya mambo hayakufuatwa alipigwa rungu zito mno na hakuweza kufanya lolote kwasababu hakukuwa na mkataba mama BIT/IGA ya kumlinda. Au kama unakumbuka vizuri moja ya sababu ambazo Tanzania ilitumia kule London dhidi ya Acacia ni kwamba walifanya biashara bila A CERTIFICATE OF COMPLIANCE baada ya BARRICK kuondoka.

DP World na makuwadi wao wanayafahamu haya fika ndiyo maana wamefanya walichofanya....
Inasikitisha wakati tuna nguri wa Sheria za Kimataifa wanaandaa IGA katika hali hiyo ya utata na Bunge lenye wasomi, uelewa na uzoefu linaridhia.

Hoja zako za awali zimenisukuma kutafiti na kupata moja ya BIT kati ya Oman na Tanzania (ambatanisho), ambao kama mkataba wa IGA kati ya JMT na Falme ya Dubai ungeandaliwa hivyo, kusingetokea sinyofahamu kubwa kama ilivyo sasaView attachment The Sultanate of Oman - Republic of Tanzania BIT.pdf
 
Bwana mwengeso swala la mwisho kabisa ambalo sikutaka kulisema, lakini naomba nilisema ili nitoe dukuduku langu la moyoni. ...
NB: DP World wasipopowa certificate of Compliance kule BRELA watafanya kazi kama mawakala wa serikali ya Dubai, hivyo yakitokea ya kutokea hatutaweza kuwafanya lolote lile kwasababu wanachukuliwa kama "State Agents". Njia ambayo tutatumia ni kuishitaki Dubai na siyo DP World. It's a tregady my friend...

Kwa huo mkataba wa IGA, ulivyotayarishwa, hakuna shaka ya kutokea yatatokea. Sasa najua nyuma ya sakata hili la mkataba wa hovyo kuna rushwa kubwa ya kimaifa iliyofubaza akili na kufunga midomo ya wenye maamuzi kwa niaba ya WaTz.

Kwa msingi wa hoja yako hiyo, kuna ukweli usio na shaka, kuwa nchi inawekwa kwenye utawala wa Falme ya Dubai kupitia DPW inayopewa hadhi ya kinchi kwa mkataba wa IGA.
 
Yaani Bunge limeridhia mkataba kati JWT na kampuni badala ya Dubai kama nchi? Duh makubwa.

Kwa taafsiri (isiyo rasmi) “DPW” au “DP World” (kwenye huo mkataba batili) inamaanisha DP World MEA Ports FZE, kampuni inayomilikiwa na serikali ambayo inamilikiwa kikamilifu na PCFC inayomilikiwa kikamilifu na Emirate ya Dubai (100%) ambayo kwa mkataba huo (IGA) inapewa mamlaka na madaraka ya kuanzisha Kampuni moja au zaidi za Miradi nchini Tanzania kwa madhumuni ya kutekeleza Shughuli za Mradi (kuendeleza na/au kuboresha uendeshaji na usimamizi wa miundombinu ya kimkakati ya Bandari za Bahari na Maziwa Tanzania, kanda maalum za kiuchumi, hifadhi za usafirishaji na ukanda wa kibiashara wa Serikali ya Tanzania; na kuboresha bandari).

NB: Katika mkataba huo IGA eneo inamaanisha eneo la nchi kavu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikijumuisha eneo lake la bahari, anga, na maeneo ya baharini ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatekeleza mamlaka
yake na haki zake za kujitawala kwa mujibu wa Sheria ya Kimataifa ya Umma. Hivyo basi, eneo lililo kwenye mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pia linahusika. Alooo!!!

YAJAYO YANAFURAHISHA kama si KUHUDHUNISHA
 
Wala usichanganyikiwe ndugu yangu, hili ni jambo rahisi kabisa kuelewa!

Iko hivi, kikawaida ni kwamba mikataba yote ya uwekezaji kuanzia miaka ya 1970's imeanza kufanywa kupitia kitu kiitwacho BIT (Bilateral Investment Treaty). Ambapo huu huwa ni mkataba baina ya mataifa mawili (Two Sovereigns/Nation-States) yanayokubaliana kuruhusu uwekezaji baina ya nchi zao mbili.

Sasa, mkataba huwa unasainiwa na mataifa lakini ili kuruhusu uwekezaji ambao utafanywa na watu, mashirika na makampuni kutoka nchi hizo mbili. Mfano, wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini kwetu Tanzania na kusaini mikataba ya hovyo mara nyingi hufanya hivyo kwasababu nchi zao zilishasaini mikataba ya uwekezaji na Tanzania huko miaka ya nyuma. Mpaka sasa Tanzania ina BIT zisizopungua ishirini na moja (21). Ukienda kwenye mtandao wa UNCTAD utazikuta ziko wazi kabisa.

Hapa ntazungumzia kitaalamu kidogo. Nchi yetu inafuata mfumo wa sheria wa Uingereza (The Common Law System), unaitaka kila sheria ya kimataifa kabla ya kupitishwa ni lazima ipelekwe kubengeni kurasimishwa (Ratification Process) ili uwe sehemu ya sheria za nchi yetu. Hili limefanyika hata kwenye hati za muungano (Articles of the Union) zilizounda Tanzania. Hivyo basi, mashirika ya nchi ambazo zina BIT na Tanzania yanaruhusiwa kuja kuwekeza nchini kwetu na kusaini mikataba chini ya mwamvuli wa kitu kiitwacho BIT (Bilateral Investment Treaty).

Ulinzi ambao unatolewa na BITs hutoa kanuni zifuatazo ambazo huwa tunaziita "Minimum Standards":
1. Rule against discrimination.
2. Rule against expropriation
3. The Most Favoured Nation & The National Treatment
4. The Rule on Admission and Establishment of Investment

Mfano hai kabisa ni yale mazengwe ya Acacia & Barrick ambao nchi yaliyokotoka yana BIT na Tanzania. Sasa Mzee wetu alipoanza kufanya yake tu wenyewe, wakaenda kufungua kesi kule LCIA (London Centre of International Arbitration) wakitumia kanuni ya "Rule Against Expropriation" iliyowekwa ndani ya BIT. Au kama unakumbuka zengwe jingine la Sun-Lodges (Mikindani Estates) ambapo muwekezaji wa kiitaliano alinunua maelfu ya hekali za ardhi kwa ajili ya uwekezaji lakini hakuendeleza sehemu, Mzee wetu CHUMA alipotaka kunyang'anya ardhi awape wananchi jamaa akaenda kufungua kesi nje ya Tanzania kuzuia hilo lisifanyike.

Nadhani hapa sasa utakuwa umepata picha kidogo, hivyo twende kwenye IGA na DP World:

IGA ni INTERGOVERNMENTAL AGREEMENT ambayo husainiwa na serikali za nchi mbili. Tanzania na United Arabs Emirates (UAE) hatuna BIT, hivyo ili kuruhusu uwekezaji nchini kwetu basi tukaamua kutengeneza mkataba wa uwekezaji baina ya Tanzania na Dubai. Hivyo IGA ni baina ya Tanzania na Dubai, na taratibu za mikataba ya kimataifa kwenye nchi ambazo zinafuata mfumo wa Uingereza ni kwamba mkataba wowote wa kimataifa ukitiwa siani haitoshi ni lazima upitishwe na bunge. Ndiyo ukaona walivyofanya wakina Dada Tulia ndani ya siku moja tu, kitu ambacho kinatia sana ukakasi.

Kwanini sasa tunaukataa huu mkataba: Mambo ni mengi mno ambayo siwezi kuyasema yote hapa, ila nijaribu kukuelezea kwa kifupi tu. Naamini utaelewa, utafanya utafiti wako na wedau wengine wataongezea mambo mawili matatu:

Mosi, hii IGA ni mkataba wa kimataifa kama mingine lakini umekaa vibaya sana tofauti kabisa na BIT nyingine. Huu mkataba unampa kibali Dubai peke yake kuja kuwekeza Tanzania ilhali Tanzania hairuhusiwi kuwekeza nchini Dubai. Hili limekaa vibaya mno.

Pili, hii IGA imeingiwa kwa dhumuni la kuwekeza kwenye bandari kupitia DP World peke yake. Tofauti na BIT nyingine ambazo huwa zinasema kwamba watakuja wawekezaji kedekede kuwekeza baada ya kufuata sheria na utaratibu wa nchi. Mkataba unasema wazi kabisa mwanzoni kwamba mfalme wa Dubai (The Emir of Dubai) atawakilishwa na baadhi ya shirika fulani ambalo litaratibu ujio wa DP World.

Tatu, hii IGA imeshasema kabisa kwaba Tanzania na Dubai wanafanya makubaliano kuruhusu DP World kutekeleza miradi kupitia mikataba midogo, HGA (Commitment to enter into HGA). Ambapo hapa tunakuja kwenye kanuni ya muhimu kabisa niliyoisema hapo juu iitwayo "Rule on Admission and Establishment of Investment". Sisi tumeshasema kabisa mwanzoni kwamba baada ya kusaini huu mkataba DP World akitaka kuwekeza ataruhusiwa moja kwa moja bila kizuizi cha serikali ya Tanzania.

Binafsi naona huu ni ukichaa, kwasababu BIT nyingine duniani zimeweka utaratibu tofauti kwenye "Admission and Establishment of Investment". Kwamba kusaini BIT siyo tiketi ya moja kwa moja kuruhusu wawekezaji wa nchi fulani kuingia nchini kiholelea. Bara za Ulaya linafuata huu utaratibu kwenye BITs zake, kwamba hata kama mabunge yamepitisha mkataba (BIT), hicho siyo kigezo cha kusema mwekezaji aje tu. Kitaalamu UNCTAD wanaiita hii mbinu "Selective Liberalisation" ambapo hata kama tumepitisha mkataba tunaweza kuamua kukatalia baadhi ya wawekezaji wako kupitia sheria za nchi yetu.

Mfano wa sheria kama hii kule Ulaya ni ule uitwao The Energy Charter Treaty (ECT) ambapo Ibara ya 10 (1)-(4) zinasema kwamba kusaini makubaliano hakuwapi wawekezaji "An Automatic Right to come and Invest". Sasa hebu tujiulize swali rahisi kabisa, hivi kwenye huu mkataba wetu, pala wanaposema DP World atakuja kuwekeza kupitia HGA (Host Government Agreement), na hatutakiwi kabisa kumpa vizuizi unadhani ni akili kweli ??? Labda mimi niwe nakosea tafasiri, ila hata kule Uingereza na Marekani, DP World aliwekewa masharti katika kuanzisha shughuli za uwekezaji.

Kule Uchina BITs zao ambazo wameingia na mataifa makubwa zinatoa kitu kinachoitwa "Performance Requirements". Kampuni linapoenda kuwekeza Uchina halifanyi moja kwa moja, ni lazima lifuate vigezo. Sasa vigezo hivyo vinaweza kuwa kama "Export Requirements", "Forming Joint-Venture Agreements with Local Companies", "Transfer of Technology Requirements" n.k Hizi mbinu, ndizo zimeifanya Uchina kuwa na teknolojia ya kisasa hadi Marekani analalamika wanaibiwa haki miliki zao "Intellectual Property".

Sasa sisi tumekubali kuwaruhusu bila kuwapa masharti yoyote yale. Huu kama siyo uhaini ni nini mkuu ??? Kama TICTS hawana uwezo wa kuendesha bandari kwa ufasaha, kwanini basi msiwajengee uwezo kwa kulazimisha DP World wayape tenda mashirika ya Tanzania ili yajengewe huo uwezo ??? Kuna mambo yanasikitisha sana kukuta yanafanywa na watawala. Yaani unaona waarabu ni wazuri kuliko wamatumbi wenzako.

Nne, hii IGA imempa DP World kitu kiitwacho haki ya upekee wa kutumia na kuendesha bandari zote (Exclusive Rights and Monopoly Over Our Natural Resources) za Tanzania, kuanzia baharini na ziwani, na maeneo yote ya kibiashara (Special Economic Zones). Mkataba umeweka bayana kabisa, kwamba kukiwa na fursa za uwekezaji kwenye bandari basi ni lazima serikali iwape DP World kabla ya kufikiria hatua yoyote ile. Huku kama siyo kuuza uhuru wetu (National Sovereignty) ni nini ??? Kiufupi, huu mkataba ni LOCK-OUT AGREEMENT kwamba hatuwezi kuruhusu muwekezaji mwingine kuja kuwekeza Tanzania kwenye bandari, awe wa ndani au nje.

Nasema haya kwasababu nimefuatilia kesi ya DP World dhidi ya Djibouti, ambapo aliwadai dola za Kimarekani milioni 200 kwa uvunjifu wa mkataba mkuu wa uwekezaji. DP World alizembea kuwekeza kwenye eneo la Doraleh tofauti na alivyoahidi hapo mwanzo. DP World wakaamua kumpa Uchina kupitia kampuni la CHINA MERCHANTS wajenge bandari. Waarabu wakapeleka kesi moja Hong-Kong na nyingine London na wakashinda kwasababu walisema Uchina ametumia rushwa kupata tenda, pili Djibouti is in material breach of their exclusive rights to utilize the ports. Hivi unadhani siku yakitokea ya kutokea watanganyika tutapona kweli ???

Mpaka sasa, ule mradi wa Bandari ya Bagamoyo ambapo ulitakiwa kujenga bandari kubwa barani Afrika kuweza kushindana na zile za Rotterdam ndiyo umeshakufa kibudu. Kama unakumbuka CHINA MERCHANTS ndiyo kampuni lililotaka kujenga bandari ya Bagamoyo. Marekani katumia DP World kuhujumu maendeleo ya Tanganyika. Kama siyo uhaini, hiki tuitaje ???

Tano, hii IGA inasema hata lilitokea tatizo lolote kidiplomasia au kwenye hali ya kimataifa, hatuwezi kabisa kuvunja mkataba na Dubai, au kuzuia utekelezwaji wa HGA za DP World. Wakaenda mbali na kusema kwamba, hata nchi ikifa na kuzaliwa nyingine, huu mkataba utabaki tu. (The IGA/HGA will subsist even in case of state succession). Wakimaanisha kwamba hata leo hii Tanzania ivunjike na Tanganyika na Zanzibar waachane basi mkataba utaendelea kuwa sehemu ya Tanganyika, tupende tusipende.

Huu ni uhaini kwasababu, hili liliwekwa wazi mwaka 1962 na Mzee Nyerere kupitia kitu tulichokiita Nyerere's Doctrine of State Succession. Kwamba mikataba ya hovyo tuliyorithi kutoka kwa mkoloni hatuwezi kuendelea nayo hata iwe ya namna gani, bila makubaliano na hayo mataifa. Hebu nikupashe siri ambayo wanasheria wengi wamepitwa. Hii siyo mara ya kwanza bandari ya Dar Es Salaam inauzwa kiholela kwa mataifa ya nje. Wakati Tanganyika inapata uhuru kulikuwa na mkataba wa Belbase (The Treaty of Belbase) ambao uliingiwa baina ya Tanganyika, Congo, Rwanda na Burundi kutumia bandari yetu milele (Infinitely) huku wakilipa paundi mbili (2) kwa mwaka. Mkataba ulisainiwa na serikali ya Uingereza na Ubelgiji.

Mzee Job Lusinde aliandika barua kusema kwamba mkataba wa namna hii hawawezi kuukubali hasa kwenye sehemu nyeti kama bandari. Ukavunjwa kibabe ili kulinda nchi. Sasa wanaposema kwamba hata mahusiano ya kidiplomasia yakivunjika au litokee jambo lolote basi hauvunjwi, huu ni ukichaa. Nyerere's Doctrine of State Succession ndiyo mbinu ambayo inakubalika na wasomi wote wa Tanganyika kufuatwa katika haya mambo ya mikataba.

Lakini kubwa, huko duniani siku hizi kuna kitu kinaitwa "The Principle of Necessity" kinawekwa kwenye BITs nyingi. Kanuni hii inasema kwamba mkataba hauizuii nchi kulinda usalama wake au maslahi yake makubwa endapo italazimika ifanye hivyo. Hivi fikiria leo, inatokea vita hapa Tanzania halafu tunataka kutumia bandari kuratibu mipango au kuzifunga bandari, hawa DP World tutawatoa kirahisi kweli ???

Au unatokea mdororo mkubwa wa kiuchumi ambao utahitaji serikali itumie rasilimali zake kubwa kama bandari kujinasua hapa tutafanyaje ndugu zangu. Mnamo mwaka 1912 asilimia 95 ya mali zote za Uingereza hasa mashirika makubwa yalikuwa mikononi mwa watu binafsi, ila baada ya vita na mdororo wa uchumi Uingereza wakayataifisha ili kuendesha serikali kwa ufasaha.

Hebu fikiria sisi hata tukutwe na lolote hatutaruhusiwa kufanya lolote, maana mkataba unasema hatuwezi kuwatoa kwa namna yoyote ile. Kama huu siyo uhaini ni nini ???

NB 1: Mwisho kabisa IGA ni baba wa HGA. Hakuna IGA hakuna HGA. Kitaalamu, HGA ndiyo mkataba mdogo unaoingiwa katika utekelezaji wa hii miradi yote ya bandari. Hivyo IGA ni mkataba baina ya nchi na nchi (State vs State), huku HGA ni mkatababaina ya nchi na mwekezaji (State vs Investor). Duniani kote huwa inakuwa hivi. Sasa kila mradi utakaofanywa ndani ya hii IGA utatekelezwa kupita HGAs/Project Agreements ambazo zitakuwa nyingi kutegemea miradi itakayokuwepo.

Kuna kitu kinaitwa "UMBRELLA CLAUSES" ambapo zipo ndani ya IGA na zitafanya kazi pia ndani ya HGA kwasababu mpaka sasa huu mkataba ni sehemu ya sheria za nchi ya Tanzania kwasababu umeshapitishwa na bunge. Mfano vile vifungu vinavyosema DP World ndiyo atakuwa mwekezaji pekee, kwamba DP World atapewa kila ruhusa bila kuzuiwa, n.k Kutudanganya kwamba HGAs/Project Agreements zitakuwa ni tofauti na IGA ni kutufanya watanzania mabazazi. Hili halikubaliki kabisa.

NB 2: Jambo muhimu jingine, ni kwamba DP World ni kampuni la Dubai lakini linauza hisa zake kwenye masoko makubwa kama kule London (Listed within London Stock Exchange). Hivi leo likaamua kuuzwa na nchi ambayo ni adui wa Tanganyika au nchi yenye milengo ya kifashisti au likanunuliwa na magaidi au likanunuliwa ili kutakatisha fedha na kutenda uhalifu, mtasemaje ??? Sasa hapa ndipo "Principle of Necessity" inabidi ifanye kazi.

Sisi haya hatujayazingatia kabisa, tunachotaka ni mapesa ya waarabu ili tupate cha kusema kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.

Mengi yapo ya kiutalaamu, ila hapa nimejaribu kuzungumza kwa lugha rahisi kabisa....
👏👏👏
 
Wakati Tanganyika inapata uhuru kulikuwa na mkataba wa Belbase (The Treaty of Belbase) ambao uliingiwa baina ya Tanganyika, Congo, Rwanda na Burundi kutumia bandari yetu milele (Infinitely) huku wakilipa paundi mbili (2) kwa mwaka

Naongezea kuweka historia isiyofahamika sana wala kuandikwa katika lugha ya kiswahili lakini imeandikwa sana katika lugha zingine kubwa za kimataifa

22. Exchange of notes accepting the protocol signed at Kigoma, on 5 august 1924, relative to the Tanganyika-Ruanda-Urundi frontier. Brussels, 17 May 1926 46,47

(46League of Nations, Treaty Series, vol. 54, p. 239.)

(47See also the Agreement between the United Kingdom and Belgiun regarding Water Rights on the Boundary between Tanganyika and Ruanda-Urundi, London, 22 November 1934, in Legislative Texts and Treaty Provisions concerning the Utilization of International Rivers for Other Purposes than Navigation (United Nations publication, Sales No. 63.V.4), p. 97.)

No. 1 - The British Ambassador at Brussels to the Belgian Minister for Foreign Affairs

Brussels, 17 May 1926

Monsieur le Ministre,

I have the honour, under instructions from His Majesty's Principal Secretary of State for Foreign Affairs, to convey to Your Excellency by the present note the formal acceptance by His Majesty's Government of the Protocol signed at Kigoma on 5 August 1924, with its accompanying maps, as defining the boundary between Tanganyika territory and the Belgian mandated territory of Ruanda-Urundi.

I am at the same time instructed to draw the attention of the Belgian Government to paragraph 51 of the Protocol in question and to invite them to agree that, notwithstanding the new boundary in Lake Tanganyika which is defined by the said paragraph, all customary rights of fishing and passage exercised by natives living on either side of it should be preserved, but that, at the same time, even with regard to the rights of fishing and passage, the respective Governments should preserve their common law rights and should not, for instance, be debarred from levying a fishing tax on all persons alike who use their territorial waters.

I should be grateful if Your Excellency would be good enough to confirm to me that the Belgian Government is in agreement with His Majesty's Government with regard to the arrangements indicated in the preceding paragraph.

I avail myself of this opportunity, etc.

No. 2 - The Belgian Minister for Foreign Affairs to the British Ambassador at Brussels

Brussels, 17 May 1926

Your Excellency,

I have the honour to acknowledge receipt of your letter of today's date, in which you are good enough to inform the Royal Government that His Britannic Majesty's Government accepts the Protocol signed at Kigoma on August 5, 1924, with its accompanying maps, as defining the boundary between Tanganyika Territory and the Belgian mandated territory of Ruanda-Urundi.

The Belgian Government also approves these documents.

At the same time you draw the attention of the Belgian Government to paragraph 51 of the Protocol in question and invite them to agree that, notwithstanding the new boundary in Lake Tanganyika which is defined by the said paragraph, all customary rights of fishing and passage exercised by natives living on either side of it should be preserved, but that at the same time, even with regard to the rights of fishing and passage, the respective Governments should preserve their common law rights and should not, for instance, be debarred from levying a fishing tax on all persons alike who use their territorial waters.

The Belgian Government has the honour to confirm to Your Excellency that they are in agreement with His Britannic Majesty's Government with regard to these arrangements.

................................................................

100 YEARS BELBASES

A FORGOTTEN PAGE OF BELGIAN COLONIALISM IN AFRICA

Belgian bases in East Africa

The Belgian colonial period ended with the independence of Burundi and Rwanda on July 1, 1962, but there is still a vestige of our colonial past: the Belbases in Tanzania.

In 1919, during the negotiation of the Treaty of Versailles, Great Britain was able to seize almost all the German colonies in East Africa. Rwanda and Burundi became Belgian mandate areas.

But Belgium, which had also participated in the war effort in East Africa, was not satisfied, protesting strongly. She received in 1921 from the British a commercial gesture as a consolation, the so-called Belbases (from "Belgian Bases"), sites in two ports of Tanganyika: Kigoma on Lake Tanganyika, and Dar es Salaam on the Indian Ocean , with free transit on the railway between these two ports.

This agreement was signed 100 years ago, on March 15, 1921.

Belgium leased the concession for a symbolic franc per year, where it could build docks and warehouses, initially in perpetuity, from 1956. for 99 years.

Goods to and from the Belgian colonies in Central Africa could pass tax-free via the railway. The Belgian government entrusted the operation to a private company, the Belgian East African Agency, which later became the International Maritime Agency (AMI).
In 1956, the Belbases were transferred to the colonial government, which now funded the infrastructure. After the independence of Congo, Burundi and Rwanda, the Belbases became the joint property of the former colonies.

The transit zone gradually lost its economic importance and, certainly after the riots of 1991 (Congo) and 1994 (Rwanda), traffic from Central Africa stopped. Between 1994 and 1995 the AMI began discussions on an "honorable end" to the management agreement, in 1996 Tanzania took over the sites.

Even if they have not been used for 25 years, in theory these Belbases still exist, because the four countries (Tanzania, Burundi, Congo and Rwanda) have not yet been able to agree on compensation for the takeover of the installations.

March 15, 1921​

On March 15, 1921, the Belgian and British governments signed a convention concerning " the free passage of persons, mail, goods, ships, vehicles and wagons from or to the Belgian Congo ", including the protectorate of the Rwanda - Urundi.

The last Belgian manager​

From January 1992 to December 1995, Guido Fallentheyn was the last Belgian manager of the Belbases in East Africa.

Source : Belbases - Une page oubliée du colonialisme Belge en Afrique
 
Inakuwaje Bunge tukufu chini ya mwalimu wa sheria linatunga sheria batili??
Bunge lililopitisha madudu haya sio hili Bunge la Dr. Tulia, ni mabunge ya nyuma!
Tatizo la bunge letu ni la kimfumo, tofauti na mabunge ya nchi kama Uingereza au Marekani ambayo yanafanya kazi ya 'kutunga' sheria, bunge letu 'linapitisha' sheria.
Ni kweli, Bunge letu ni Rubber Stamp tuu linapitisha madudu yote ya serikali!. Ukiondoa Bunge la Mzee wa Speed and Standards, sikumbuki Bunge lingine lolote kugomea hoja za serikali!. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
Kila kitu kinafanywa na serikali, sheria zote zinaandikwa na serikali na kupelekwa bungeni 'kupitishwa'.
Ni kweli, huu ni udhaifu mkubwa!.
Hata wakijaa ma profesa watupu, as long as mwenyekiti wa CCM anatarajia bunge 'lipitishe' sheria na maazimio ya kuisifu serikali kwa maslahi ya chama chao, basi madudu haya hayawezi kuisha.
Naunga mkono hoja, na niliwahi kushauri Je, Bunge letu linaendeshwa kikada? Ili tuwe na Bunge la haki, lenye uwezo wa kuisimamia Serikali Kikamilifu, kuna haja Spika asitokane na vyama?
P
 
Bunge lililopitisha madudu haya sio hili Bunge la Dr. Tulia, ni mabunge ya nyuma!

Ni kweli, Bunge letu ni Rubber Stamp tuu linapitisha madudu yote ya serikali!. Ukiondoa Bunge la Mzee wa Speed and Standards, sikumbuki Bunge lingine lolote kugomea hoja za serikali!. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?

Ni kweli, huu ni udhaifu mkubwa!.

Naunga mkono hoja, na niliwahi kushauri Je, Bunge letu linaendeshwa kikada? Ili tuwe na Bunge la haki, lenye uwezo wa kuisimamia Serikali Kikamilifu, kuna haja Spika asitokane na vyama?
P
Tatizo la msingi katika mbunge ni nini?
1) Mfumo wake wa kujadili na kufikia maamuzi?
2) Uongozi wa Bunge, kwa maana Spika na timu yake?
3) Wabunge kwa maana:
• wanavyopatikana?
• elimu, uwezo, uzoefu, ufahamu?
• uaminifu kwa chama?
4) Utashi wa kisiasa wa viongozi wa Serikali kwa maana ya Rais na wateule wake?
 
Wanabodi,

Nikiwa ni mwanachama wa TLS, nimeisoma taarifa ya TLS kuhusu issue ya Bandari na DPW, kiukweli kabisa TLS inastahili pongezi za dhati!, imefunga huu mjadala, ingekuwa mimi ni Mnyamwezi, Kinyamwezi hii inaitwa "funga kalomo", yaani funga mdomo!. Taarifa hii ya TLS ni funga kazi, na huu ndio uzalendo!, hongera sana TLS kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Kama mwanachama mwaminifu wa TLS, kwa heshima ya chama changu cha wanasheria wa Tanganyika, naomba nisikosoe jambo lolote kwenye taarifa ya TLS, ila sio vibaya kuzungumzia baadhi ya hoja ambazo TLS haikuzigusia kabisa!.

Ni baada ya kuisoma taarifa ya TLS, ndipo nikagindua mtu mwandishi wa habari kwanza, halafu ukaingia kwenye sheria, unakuwa na jicho kali zaidi kuliko jicho la mwanasheria mwanasheria tuu ambaye sio mwanahabari!.

Jicho la Mwanasheria linaangazia vifungu vya katiba, sheria, taratibu na kanuni, jicho la mwanahabari linaangalia mtazamo wa jamii, Mwananchi wa kawaida, anaona nini, anataka nini, hivyo jicho la mwanahabari linaona kuliko jicho la mwanasheria.

Baada ya Bunge letu kuridhia, niliandika makala hii, Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! humo niliainisha mapungufu ya IGA hiyo kisheria kwa jicho la kiuanahabari.

TLS katika taarifa yao, kuna maeneo mengi wamepita mule mule nilimopita mimi, ila lile kubwa kuliko, "The Capacity" to contract, TLS wamelikwepa na kuliweka kiporo kusubiria wawasiliane na Dubai.

TLS hawakuyaona yale niliyo yaona mimi!. Tanzania ni nchi, inakwenda kuingia mkataba wa kimataifa wa nchi na nchi, yaani Tanzania na UAE, lakini signatories wa Tanzania ni nchi, halali signatories wa UAE ni kampuni ya DPW!, tena imesaini bila POA yoyote toka UAE!.

Kwa maneno mengine ni kampuni ya DPW imejigeuza ni nchi ya Dubai wakati ni kampuni binafsi!, sio nchi, Dubai sio nchi, nchi ni UAE!, nchi yetu haiwezi kuingia mkataba wa kimataifa wa kuwa ratified na Bunge letu kama an international Treaty wakati signatories ni kampuni na sio nchi na hakuna POA yoyote ya UAE kuruihusu DPW to transact an international Treaty on behalf of UAE!.

Nimeipongeza TLS kwa uzalendo kwenye hili, ila nikiri kuwa nimeshangazwa na umakini huu wa TLS katika hili la Bandari.

Sheria Kuu kuliko zote nchini kwetu ni katiba, katiba ndio sheria Mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni sheria batili!. Kinachoibatilisha hiyo sheria yoyote kinyume cha katiba, ni katiba yenyewe!.

  1. Serikali yetu ime draft sheria batili, inayokwenda kinyume cha katiba, ikaipeleka Bungeni kutungwa kuwa sheria!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
  2. Bunge letu likaitunga hiyo sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, kwanini TLS walikaa kimya?.
  3. Rais wa JMT akaisaini hiyo sheria batili kuwa ni sheria!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
  4. Mahakama Kuu kupitia kesi ya Mtikila, ikatamka sheria hiyo ni batili na kuitaka serikali iifute. Kwanini TLS walikaa kimya?!.
  5. Ubatili wa sheria batili yoyote unabatilishwa na katiba, Mahakama Kuu ikiisha tamka sheria fulani ni batili kwa kwenda kinyume cha katiba, automatically sheria batili hiyo inakuwa imebatilika from there and then. Kazi ya serikali ni procedures tuu za kuifuta!. Kwanini TLS walikaa kimya na sheria batili hiyo mpaka sasa bado iko kwenye sheria zetu licha ya Mahakama Kuu kutangaza ni batili?.
  6. Serikali yetu ikakata rufaa kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, ikashidwa!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
  7. Serikali yetu baada ya kubwebwa, ikafanya kubwa kuliko, ikapeleka Bungeni mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, batili ile ikachomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!. Kwanini TLS walikaa kimya?!.
  8. Bunge letu likafanya mabadiliko ya katiba na kuichomeka hiyo batili ndani ya katiba yetu!. Hivyo katiba yetu imenajisiwa kwa kuchomekewa ubatili!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
  9. Mchungaji Mtikila hakukubali katiba yetu inajisiwe, akafungua shauri kupinga mabadiliko hayo ya katiba, Mahakama Kuu ikampa ushindi na kutangaza mabadiliko hayo ni batili!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
  10. Serikali yetu ikakata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, serikali ikashinda, kwanini TLS walikaa kimya?!.
Mpaka leo ninapoandika hapa, Katiba yetu bado inacho kifungu batili hicho!, sheria zetu bado zina ubatili huo na TLS wako kimya!.

Nimalizie kwa pongezi tena, TLS kwa hili la Bandari, ila kuna makubwa kuliko hili la Bandari, TLS bado hamjachelewa!.

Mungu ibariki TLS
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Rejea
1. Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
2. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
3. Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu?

Hivi wewe ni Mwanachama wa TLS? Kweli vigezo vya uanasheria viangaliwa upya
 
Sawa Mkuu, ahsante sana kwa muda wako na ufafanuzi murua ulioutoa.
Kumbe huwa huishii tu kuandika hapa jamvini badala yake huwa unawatumia nakala kabisa!
Hapana, mimi nina safu zangu weekly kwenye baadhi ya magazeti, hivyo wanasoma wenyewe au kupitia wasaidizi wao, mimi na monitor tuu matokeo.
Maana najua wana majukumu mengi sana.
Hivyo kupata muda wa kusoma makala zako (ambazo mara nyingi huwa ndefu sana) ni nadra sana.
It's true nyingi ya makala zangu ni ndefu ila huwa naweka short version kwenye Twitter hivyo ujumbe unawafikia.
Lakini kama huwa wanapata watu wa kuwafikishia basi ni jambo jema sana.
Yes kuna watu wanawafikishia, na nyingine wanasoma wenyewe in person Thinking Aloud: Hongera JF kulisaidia Taifa, "Atakuwa anaingia JF in person na kutusoma!". 2021 let's be more responsible, more strategic

"Serikali yetu ime draft sheria batili, inayokwenda kinyume cha katiba, ikaipeleka Bungeni kutungwa kuwa sheria!, kwanini TLS walikaa kimya?"

Wewe si TLS? Nikisemaga wewe ni mtu wa hovyo nashambuliwa, wewe kama mwanachama hai, tujibu hili swali faranga wewe.
 
Yes mimi ni TLS, ila mwanachama yoyote wa TLS yuko huru kufanya lolote as an individual lakini TLS ni taasisi, maamuzi ya TLS ni maamuzi ya ki taasisi.

Mimi as individual member wa TLS sijafanya lolote, ila hata kuhimiza tuu kama hapa Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu? it is something.
P
 
Wanabodi,

Nikiwa ni mwanachama wa TLS, nimeisoma taarifa ya TLS kuhusu issue ya Bandari na DPW, kiukweli kabisa TLS inastahili pongezi za dhati!, imefunga huu mjadala, ingekuwa mimi ni Mnyamwezi, Kinyamwezi hii inaitwa "funga kalomo", yaani funga mdomo!. Taarifa hii ya TLS ni funga kazi, na huu ndio uzalendo!, hongera sana TLS kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Kama mwanachama mwaminifu wa TLS, kwa heshima ya chama changu cha wanasheria wa Tanganyika, naomba nisikosoe jambo lolote kwenye taarifa ya TLS, ila sio vibaya kuzungumzia baadhi ya hoja ambazo TLS haikuzigusia kabisa!.

Ni baada ya kuisoma taarifa ya TLS, ndipo nikagindua mtu mwandishi wa habari kwanza, halafu ukaingia kwenye sheria, unakuwa na jicho kali zaidi kuliko jicho la mwanasheria mwanasheria tuu ambaye sio mwanahabari!.

Jicho la Mwanasheria linaangazia vifungu vya katiba, sheria, taratibu na kanuni, jicho la mwanahabari linaangalia mtazamo wa jamii, Mwananchi wa kawaida, anaona nini, anataka nini, hivyo jicho la mwanahabari linaona kuliko jicho la mwanasheria.

Baada ya Bunge letu kuridhia, niliandika makala hii, Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! humo niliainisha mapungufu ya IGA hiyo kisheria kwa jicho la kiuanahabari.

TLS katika taarifa yao, kuna maeneo mengi wamepita mule mule nilimopita mimi, ila lile kubwa kuliko, "The Capacity" to contract, TLS wamelikwepa na kuliweka kiporo kusubiria wawasiliane na Dubai.

TLS hawakuyaona yale niliyo yaona mimi!. Tanzania ni nchi, inakwenda kuingia mkataba wa kimataifa wa nchi na nchi, yaani Tanzania na UAE, lakini signatories wa Tanzania ni nchi, halali signatories wa UAE ni kampuni ya DPW!, tena imesaini bila POA yoyote toka UAE!.

Kwa maneno mengine ni kampuni ya DPW imejigeuza ni nchi ya Dubai wakati ni kampuni binafsi!, sio nchi, Dubai sio nchi, nchi ni UAE!, nchi yetu haiwezi kuingia mkataba wa kimataifa wa kuwa ratified na Bunge letu kama an international Treaty wakati signatories ni kampuni na sio nchi na hakuna POA yoyote ya UAE kuruihusu DPW to transact an international Treaty on behalf of UAE!.

Nimeipongeza TLS kwa uzalendo kwenye hili, ila nikiri kuwa nimeshangazwa na umakini huu wa TLS katika hili la Bandari.

Sheria Kuu kuliko zote nchini kwetu ni katiba, katiba ndio sheria Mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni sheria batili!. Kinachoibatilisha hiyo sheria yoyote kinyume cha katiba, ni katiba yenyewe!.

  1. Serikali yetu ime draft sheria batili, inayokwenda kinyume cha katiba, ikaipeleka Bungeni kutungwa kuwa sheria!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
  2. Bunge letu likaitunga hiyo sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, kwanini TLS walikaa kimya?.
  3. Rais wa JMT akaisaini hiyo sheria batili kuwa ni sheria!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
  4. Mahakama Kuu kupitia kesi ya Mtikila, ikatamka sheria hiyo ni batili na kuitaka serikali iifute. Kwanini TLS walikaa kimya?!.
  5. Ubatili wa sheria batili yoyote unabatilishwa na katiba, Mahakama Kuu ikiisha tamka sheria fulani ni batili kwa kwenda kinyume cha katiba, automatically sheria batili hiyo inakuwa imebatilika from there and then. Kazi ya serikali ni procedures tuu za kuifuta!. Kwanini TLS walikaa kimya na sheria batili hiyo mpaka sasa bado iko kwenye sheria zetu licha ya Mahakama Kuu kutangaza ni batili?.
  6. Serikali yetu ikakata rufaa kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, ikashidwa!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
  7. Serikali yetu baada ya kubwebwa, ikafanya kubwa kuliko, ikapeleka Bungeni mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, batili ile ikachomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!. Kwanini TLS walikaa kimya?!.
  8. Bunge letu likafanya mabadiliko ya katiba na kuichomeka hiyo batili ndani ya katiba yetu!. Hivyo katiba yetu imenajisiwa kwa kuchomekewa ubatili!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
  9. Mchungaji Mtikila hakukubali katiba yetu inajisiwe, akafungua shauri kupinga mabadiliko hayo ya katiba, Mahakama Kuu ikampa ushindi na kutangaza mabadiliko hayo ni batili!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
  10. Serikali yetu ikakata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, serikali ikashinda, kwanini TLS walikaa kimya?!.
Mpaka leo ninapoandika hapa, Katiba yetu bado inacho kifungu batili hicho!, sheria zetu bado zina ubatili huo na TLS wako kimya!.

Nimalizie kwa pongezi tena, TLS kwa hili la Bandari, ila kuna makubwa kuliko hili la Bandari, TLS bado hamjachelewa!.

Mungu ibariki TLS
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Rejea
1. Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
2. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
3. Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu?
Kaka Paskali,
Nimeshangazwa na baadhi ya mitazamo yako kwenye hili andiko lako. Nina maswali haya ambayo naomba unipe majibu au ufanunuzi wake;

1. TLS ni nani? Rais wa TLS, wanachama wa TLS, au wote rais na mwanachama ndiyo TLS? Kama jibu TLS ni rais wa TLS, kwanini kwenye kujadili lolote lazima aite wanachama? Kama jibu ni Rais na wanachama, kwani hukuyasema hayo yaliyokaliwa kimya wakati wa mkutano?

2. Unasema wewe ni mwanachama wa TLS kwa vile ni mwanasheria, HAYA UNAYOSEMA TLS IMEKAA/ILIKAA KIMYA WAKATI YANATOKEA, HUONI KUWA UNAJISEMA MWENYE KWAMBA ULIKAA KIMYA?

3. Kama TLS wana uwezo wa kukosoa kama ilivyofanya kwenye hili la bandari, kwanini mngoje hadi wakosee ndo muamke kusema makosa? Kwani msiwe sehemu ya kinachokwenda kutokea?
 
Tatizo la msingi katika Bunge ni nini?
Tanzania tuna matatizo makubwa katika mifumo, systems, serikali ina matatizo, Bunge lina matatizo, Mahakama ina matatizo!.
1) Mfumo wake wa kujadili na kufikia maamuzi?
Bunge lilipaswa kuwa linatunga sheria, Mahakama inatafsiri sheria na serikali inatekeleza sheria, lakini Bunge letu halitungi sheria, serikali ndio inatunga sheria, Bunge linaipitisha kwa rubber stamp.
P
 
Tanzania tuna matatizo makubwa katika mifumo, systems, serikali ina matatizo, Bunge lina matatizo, Mahakama ina matatizo!.

Bunge lilipaswa kuwa linatunga sheria, Mahakama inatafsiri sheria na serikali inatekeleza sheria, lakini Bunge letu halitungi sheria, serikali ndio inatunga sheria, Bunge linaipitisha kwa rubber stamp.
P
Kwenye hili hata sisi wananchi tuna matatizo kaka Paskali. Mfano mdogo, tu, ULIYOAMBIWA WAKATI UMEITWA BUNGENI HUJAWAHI KUYASEMA..!! Why?
 
Hapana, mimi nina safu zangu weekly kwenye baadhi ya magazeti, hivyo wanasoma wenyewe au kupitia wasaidizi wao, mimi na monitor tuu matokeo.

It's true nyingi ya makala zangu ni ndefu ila huwa naweka short version kwenye Twitter hivyo ujumbe unawafikia.

Yes kuna watu wanawafikishia, na nyingine wanasoma wenyewe in person Thinking Aloud: Hongera JF kulisaidia Taifa, "Atakuwa anaingia JF in person na kutusoma!". 2021 let's be more responsible, more strategic
P
Mr. Mayalla, makala zako huwa zinakuwa kwenye magazeti yapi maana magazeti mengi ya Tanzania contents zao hata hazivutii kabisa ukiacha THE CITIZEN, ukilinganisha na Magazeti ya Kenya kama DAILY NATION, THE STANDARD, FINANCIAL TIMES na mengine wapo very investigative na flow ya news zao zinavutia sana. Mfano wakati huu wa sakata la bandari huoni hili suala likipewa kipaumbele kwenye magazeti yetu ili kuongeza pressure kwa serikali.
 
Back
Top Bottom