Kwa Lomalisa na Bigirimana Pesa ya Tajiri imepotea, na nilichokiona kwa Aziz Ki ni 'Domo Kubwa Kuvimba' lake tu na Kukosea Kwingi

Kwa Lomalisa na Bigirimana Pesa ya Tajiri imepotea, na nilichokiona kwa Aziz Ki ni 'Domo Kubwa Kuvimba' lake tu na Kukosea Kwingi

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] msifie wee bas, vipi ni amekuoa wee??
Samahan shost, mumeo namsifia kiuchezaji sio vinginevyo, kuwa na amani mwayaaaaa.
Ungejua pahali ilipo kambi ya fisi usingeropoka hivyo, hujui leo hii utavamiwa na fisi wewe, Chunga domo lako binti
 
Hivi nyinyi mnashabikia ufundi uliooneshwa au vipaji binafsi. sasa sisi watanzania tulio nje ya nchi na ambao tunataka kujua ufundi wa timu , je tuzidi kumlilia kocha aongeze ufundi wake au wachezaji wawajibishwe. jamani acheni mzaha chambueni kiukweli kuhusu Yanga ili marekebisho ya ufundi yafanyike.sisi tulitaka kisomo cha kocha kichambuliwe jinsi midfilders wanavyo link na offence dept uwanjani.

kama wewe unajua mpira wa kisayansi kumchambua mchezaji mmoja mmoja hakuna tija angalia ufundi wa timu ambao midfiders wanavyo link na makeki na washambuliaji. hapo sasa chokoza ili tumsute kocha. amin amin nawaambieni hata ukimweka pele wa 19580 na maradona na robeto bagio kama midfiders hawana kisomo cha link ya kuwatafutia vyumba basi utawaona hawawezi soka. hivyo tuchambue ufundi ulikuwaje jana ili nasi tuelimike na kuweka hoja ya kumdai kocha. get ma point amigos
 
Me sio shabikii wa yanga but hao watu ulowataja haswa bigrimana umemkosea heshima kabisaa wewe acha ushabiki me MWenyewe nimeona mpira wa gaeL nkasema kweLii funDii
 

Attachments

  • IMG_20220722_090202.jpg
    IMG_20220722_090202.jpg
    46.6 KB · Views: 14
Yassin Mustafa ana uwezo mkubwa kuliko Joyce Lomalisa Mutambala kwa Beki ( Mbavu ) ya Kushoto.

Zawadi Mauya ana uwezo mara 100 kuliko Mchezaji wa Newcastle United ya katika Photoshop ya Mitandaoni Bigirimana.

Saido Ntibanzokinza na Yacouba Sogne ni Wazuri mara Milioni kuliko Domo Kubwa Kuvimba Stephanie Aziz Ki.

Mchezaji pekee ambaye amecheza vyema, ameonyesha Kipaji Kikubwa na Uwezo wa hali ya Juu ( japo haimbwi, anadharaulika na alitaka hata Kuachwa ) ni Farid Mussa.

Fiston Mayele sasa hivi Sifa zimemzidi Kiwango na Kawekeza zaidi katika Style yake ya Kushangilia badala ya Kubuni Mbinu mpya za Kufunga Magoli ( Mabao )

Kama kuna Golikipa ambaye Yanga SC wanae sasa ila ni Mbovu ( isopokuwa analindwa na Mabeki wake ) na atakuja Kuigharimu pakubwa Yanga SC ni Kipa Guigui Diara.

Kama kuna Beki wa Yanga SC ambaye kwa Kiwango chake Kibovu cha sasa hana Hadhi Kuichezea ( na nashangaa bado ni Nahodha ) ni Bakari Nondo Mwamnyeto.

Kama kuna Beki ambaye namkubali Yanga SC kutokana na Kutumia Akili nyingi japo ana Umbile Dogo ni Dickson Job na nawashauri Yanga SC wamrumie mno huyu kuliko Mzee wa Kuchomesha Beki Bakari Nondo Mwamnyeto.

Kiraka Yannick Bangala kwa Kiwango chake, Confidence yake na Football Commanding Skills zake ile Tuzo ya NBC Premier League 2021 / 2022 ilimstahili na aliistahili kabisa kwani Jamaa anajua na napenda anavyokichafua Uwanjani.

Pamoja na Kufungwa na Vipers FC bado nawaona Yanga SC kuwa ni League Title Contender Msimu ujao ( Unaokaribia Kuanza tena ) kwani wana Wachezaji wengi Wakubwa, Wazuri na wa Kuamua Matokeo muda wowote ule.

Kufungwa na Vipers FC wala Kusiwavunje Moyo bali wajjtathmini, wajirekebishe na wajipange zaidi kwa Mechi za Ligi na za Kimataifa pia kwani nawaona wakifika mbali Kimashindano.

Yangu leo GENTAMYCINE ni haya tu!!!
Mamaeeeee aahaaaaa
 
Back
Top Bottom