Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Nina ringi la shaba nimenunua 5000 ...kuna mzee mmoja wa kinyakyusa siku moja akanitania niuzie mjukuu wangu hilo ringi?nadhani alijua mi nipo vizuri nikamwambia hili siuzi hata kwa milioni akacheka tu angejua mi mtupu tu nadhsni anngenijaribu...mi ubaya nauota tu na kwa mganga sijawahi kwenda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisikia busu la mwendokasi ndo hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshukuru Mungu kwa kuwa upo salama mkuu
Nilikuwa natokea Dar nikiwa na pikipiki aina ya Honda Benly 250 niliyokuwa natoka kuichukua Bandarini ,sikutaka kuipandisha kwenye Lori,niliamua kuendesha mwenyewe kwenda mwanza ili nipate kutalii,safari ni ndefu mno ilikuwa,nilichoka sana hasa mikononi na begani,Nilipofika Singida niliamua kulala,lakini ilipofika saa 3 Usiku nikaamua kuendelea na safari na nikaghairi kulala kwa Sababu nilihisi mwili umepata nguvu.
Nilipoanza kuteremka mlima Sekenke niliona mwanamke mrembo mno kwenye ile misitu usiku wa saa 5 eneo pweke lile lisilo na makazi ya watu zaidi ya mashimo marefu kando ya barabara ,mwanamke yule alikuwa akinisimamisha,nilipunguza mwendo na kuwasha full light ili nimwone vema,hakika alikuwa mzuri hasa,alivaa mtandio kichwani na gauni refu jekundu,alikuwa kama shombe wa kiarabu nilipomkaribia zaidi mwili wote ukasisimka ndo nikajikuta nazidisha mwendo kwa hofu,niliendesha kwa spidi ya kifo hadi Igunga,sikuendelea na safari nililala igunga ,hadi Leo huwa najiuliza sana juu ya mwanamke huyo wa ajabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jini hilo linawatokea wengi hapo sekenke hasa pale magari yanapoharibika
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] huyo jamaa aliyepatwa mara mbili Nimecheka mpaka basi
 
Huu mtindo wa kusimamisha gari na kushuka kwenda kushuhudia ndio mnajitafuutia matatizo, wakati unaenda kutafuta ushahidi kamili, unafungua mlango unaenda unatizama, huku jini na yeye anaingia kwenye gari. Unarudi unawasha gari mpaka kwako, jini lishaingia kwako na linaanza vitimbi!
 
Hukumuomba namba ya simu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nitaleta mrejesho wa kisa cha rafiki yangu wa karibu ambaye anendesha lory kuna mkasa uliwahi kumkuta wa kumpakia jini na kwenda kumshusha maeneo ya mahenge ya jirani na kitonga.

Huo ulitokea kama miaka mitano iliyopita
 
Ungesimama labda alikuwa malaika mahaba yule umepoteza Bahati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usibishe usibishe ndg vitu hivyo vipo, hata baharini... Dunia ni kubwa na ina mambo na viumbe tofauti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…