Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Hiyo kawaida kabisa kwa sisi tunao safiri safari kila mkoa mara nyingine unamkuta bibi tena yule unaemfaham lakini alishakufa au mbabu na bakora mkononi wakati mwingine unaona picha ya jeneza kabisa limefunguliwa na sanda ipo au mtoto mdogo anatambaa yaani tushazoea wala hofu ile haipo tena.
Onyo.ukiona vitu kama hivyo usijaribu kukwepa au kushika break inakula kwako.
Mi kukna siku naenda dodoma niko na ford new model kuna kizee kilitokea vichakani kikasimama ghalfa barabarani haki ya (mungu mungu nisamehe)nilikaza mikono kushika steling vizuri nilimpa nikafumba macho ili nisione ninavyoua huwezi amini nilimpita na sikusikia kishindo chochote na nilienda mbele kama 4 klmtrs nikapaki gari kuangalia sikuona tatizo kwenye gari na niliendekea nabsafari yangu bila presure.
Kosa ulilifanya, ila Mungu alikunusuru na ajali tu.
Utafumbaje macho wakati umelenga kuua? Target yako utaimaintain vipi kupatia kuipiga?
Ndiyo maana huyo kibwengo ulimkosa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi msafara wa kigwangala si dereva nae anasema aliona twiga,wachawi hawana chama hahahahah aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ajari mpaka leo siielewi
Lile gari la kigwa lina teknolojia ya ku detect any moving object mbele yake pamoja na auto brake
Yani kwa mfano uko speed then mbele ghafla gari lingine hili hap
Lile gari litakutaadharisha usimame na baada ya sekunde kadhaa linasimama lenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa yangu amenipigia simu anasema, Kuna siku alikua anarudi Nyumbani Area C, saa sita usiku. alikua taxi driver, kufika eneo la round about ya kuelekea Area C akasimamishwa na mdada amevaa ijabu, jamaa anasema alimpa maelekezo sehemu anapotaka kwenda. jamaa anasema alipo fika maili mbili aliuliza ni njia Ipi ili afahamu mapema pa kuingilia, lakini aliona kimya akamuuliza tena akaona kimya, ikabidi apaki pembeni akageuka nyuma akakuta siti tupu. jamaa anasema alifungua mlango na kukimbia, gari aliifuata asubuhi na kwenda kukabidhi kwa mwenye gari. Ndio ikawa mwisho wa yeye ku taxi driver. ni miaka ya tisini kwa mujibu wake. jamaa anaishi Dom.

Sent using Jamii Forums mobile app
2013 kuna jamaa alikua na cruiser usiku ndani yuko na binti amemuokota disco
Jamaa akawa anatoka town anaelekea sijui wapi speed hatari
Ghafla akapoteza uelekeo akagonga miti kama 3 akanyofoka nayo
Then kwa mujibu wa mmoja wa walinzi wa maemeo yale binti akatoka anakimbia
Jamaa akakutwa ubongo chini ushamwagika
Inasemekana yule binti alikua jini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu watakuambia uchawi haupo!
Waende kigoma siku 1 au Tarime
Wakati niko mdogo huko tarime nikiwa darasa la 4 au 5
Usiku mida ya saa nane.nilikua nimelala na kaka yangu ila mi niko ukutani
Ghafla nikastuka naona watu kama watatu wanaimba "hakuna hakuna"
(Kulikua na mwanga wa taa kidogo) nikapiga kelele wakapotea ila mmoja nilimtambua ni bibi fulani wa pale mtaani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwezi wa tano mwaka huu,natoka Dar naenda Lindi nilikuwa na gari ndogo.Mbele ya Njia nne(wakazi wa kilwa na kusini watapajua) kuelekea Nangurukuru kuna sehemu hapo katikati kuna pori kubwa kiasi,nikakutana na mtu mrefu hatari (Sioni mwisho wake kwenda juu) afu kavaa nguo nyeupe kama kanzu hivi amesimama pemben ya barabara *****! nilikuwa speed 100 lakn niliona gari haitembei na niliwasha ac ila nililoa jasho,kufika nangurukuru nikasema nipark mzani nisubir kukuche mweee nakutana na madere wawili wadangote wametokea dsm pia,kumbe nao walikutana na lile dubwana ***** sitosahau ilibdi nipumzike pale mzan mpk saa kum na mbili
Limesimama tu halifanyi kitu ? Na hukugeuka nyuma ?
Hii nyumba nilipo saivi kuna tetesi kuwa wapangaji waliotoka
Kuna siku mwanamke mmoja alikua hapa sebureni nilipo mimi mchana wa saa saba
Akasikia hodi ya sauti ya kike, kufungua mlango akakutana na kiumbe kama hicho
(Jirani yetu ni mganga)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi sekeke pale dalajani kila nikipita usiku huwa namuona bibi kizee anakatiza barabarani huwa huwa sisimami , pia kuna sehem inaitwa machinjioni ukiwa unakwenda Rwanda bibi huyo huyo huwa nakatiza road huwa sisimami yaan mpaka nimeshazoea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo maana wanasiasa wanadanganya watanzania kirahisi sana.
Yaani huu uongo umeandika kama vile unawaandikia watoto wa shule za chekechea.au umetoa kwenye movie. Eti ukatoa bastola 9mm ukawaoneshea dirishan huo usiku nao wakaiona, pia ukawasikia wakiongea,ukajua wapo wangap kwenye gari majambazi hata hawakuweka tinted? Walifungua tu vioo uwaone nadhan waliwasha na taa kabisa uwahesabu, ulipunguza sana mwendo nao wakapunguza wakuoneneshe wapo wangap, na pia wakusikie... Na waone una bastola...

Huu uongo wa kitoto muwe mnaambiana huko shuleni wakati wa break au vijiweni. Anyway watu huwa mnatafuta jukwaa la kuuzia chai.uliona ukisema mauza uza hutaweza sema nliyaonesha bastola ukaona uje na version yako.

Haya baadaye ukakutana na mengine kwenye lorry, hayo ukayaonesha mabomu hand grenades au machine gun yakasema ...tusepe tu.
Acheni utoto na kutafuta sifa za kijinga
Kweli kabisa mimi sina chale wala chanjo, na nasafiri sana usiku.
Tatizo kubwa ni majambazi.
Mi nina kisa cha ukweli, majambazi, au highway robbers.

Nimetoka Dar saa nne na nusu usiku.
Ni miaka takriban 15 iliyopita.
Mwendo ni wa kawaida Dar Chalinze, ile naingia Mdaula magari sasa machache na full light unaona hadi kilometa mbili.
Baada ya njia panda kwenda Ngerengere kwa mbali naona taa nyekundu, dalili ya gari.
Kwa vile sasa mwendo wangu ni kama 130~140km/hr nikalipita gari lile, na naliona Toyota Mark II.
Ile sijaenda kilometa tano naona kwa nyuma kuna gari, full light linakuja wangu wangu, tena likanipita, gari lilelile Mark II, NA LINA WATU WAWILI niliowaona.
Mda hiyo saa usiku, tano na nusu!
Nikaendelea na mwendo wangu ila nikaongeza mwendo.
Wale jamaa nafikiri nia ni kunisimamisha, lakini nikaongeza mwendo sasa 165~170km/hr!
Nikalipita!
Do, jamaa nikaanza kufikiria, jambazi lazima kumsurprise, akikuwahi yeye, basi bahati yako mbaya.
Ikaja kona tukapunguza mwendo, ila nami nikatoa 9mm mguu wa kuku.
Nikasubiri ili sasa jamaa anipite.
Kweli jamaa akakanyaga mafuta, wakati ana nipita , nikaongeza spidi kidogo ili tuwe sambamba, nikafungua dirisha na kumwelekeza mtutu.
Ee bwana kabla sijakamua, nikasikia kabisa abiria akimwambia mweziwe... twende... twende ...twende!
Mark II ili paa, na sikuiona tena hadi nafika Morogoro.
Usafiri kafiri!
 
Hii haina part two yake?

Nilikuwa natokea Dar nikiwa na pikipiki aina ya Honda Benly 250 niliyokuwa natoka kuichukua Bandarini ,sikutaka kuipandisha kwenye Lori,niliamua kuendesha mwenyewe kwenda mwanza ili nipate kutalii,safari ni ndefu mno ilikuwa,nilichoka sana hasa mikononi na begani,Nilipofika Singida niliamua kulala,lakini ilipofika saa 3 Usiku nikaamua kuendelea na safari na nikaghairi kulala kwa Sababu nilihisi mwili umepata nguvu.
Nilipoanza kuteremka mlima Sekenke niliona mwanamke mrembo mno kwenye ile misitu usiku wa saa 5 eneo pweke lile lisilo na makazi ya watu zaidi ya mashimo marefu kando ya barabara ,mwanamke yule alikuwa akinisimamisha,nilipunguza mwendo na kuwasha full light ili nimwone vema,hakika alikuwa mzuri hasa,alivaa mtandio kichwani na gauni refu jekundu,alikuwa kama shombe wa kiarabu nilipomkaribia zaidi mwili wote ukasisimka ndo nikajikuta nazidisha mwendo kwa hofu,niliendesha kwa spidi ya kifo hadi Igunga,sikuendelea na safari nililala igunga ,hadi Leo huwa najiuliza sana juu ya mwanamke huyo wa ajabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utingo alikuja kukanyaga brake wewe ukiwa umetoka kwenye kiti cha udereva au ukiwa pale pale?

Aisee... Gari ilinyooka tu sababu barabara ilikuwa imenyooka? Ha ha ha.... Wadau muwe hata mnatufikiria na sisi wasomaji.si kwamba ni wajinga sana. Sometime tunasoma ili tuburudike lakin haimaanishi kuwa ni wajinga sana .


nakumbuka nilipokuwa dreva wa basi moja linaitwa Tanganyika bus kule MWANZA nilipokuwa ktk route za kwenda Mara ipo siku njiani majira ya saa 3 nikiwa ktk shughuli zangu za udereva nilionana ghafla na jamaa akiwa ana Ng'ombe wawili akikatisha katkati ya barabara tena ni babu kavaa lubega,nilichosema ni kwa jina la Yesu ,Mungu wangu nisaidie sikuwa hata na akili ya kushika breki niliachia mikono na gari ilivuka pale,shukrani kwa utingo jirani yangu baada ya kuona ile hali utingo yule alikanyaga breki huku tukiwa tumevuka lile eneo,baada ya hapo sikuweza tena kuendesha,gari liliendehswa na utingo hadi tukafika nahc ni Mungu tu alisaidia si mimi,tokea siku ile sijaedesha tena gari usiku mwisho ni saa 12 jioni
 
Chai chai chai... Kikombe sh ngapi? Acheni fix madogo...

Hiyo ajari mpaka leo siielewi
Lile gari la kigwa lina teknolojia ya ku detect any moving object mbele yake pamoja na auto brake
Yani kwa mfano uko speed then mbele ghafla gari lingine hili hap
Lile gari litakutaadharisha usimame na baada ya sekunde kadhaa linasimama lenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utingo alikuja kukanyaga brake wewe ukiwa umetoka kwenye kiti cha udereva au ukiwa pale pale?

Aisee... Gari ilinyooka tu sababu barabara ilikuwa imenyooka? Ha ha ha.... Wadau muwe hata mnatufikiria na sisi wasomaji.si kwamba ni wajinga sana. Sometime tunasoma ili tuburudike lakin haimaanishi kuwa ni wajinga sana .
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna sehemu, ukitoka Mombo naenda mazinde, kuna eneo lina kosa kali sana, nilikutana na madude ya ajabu mpaka niliogopa kuendelea na safari na usiku ule sikupata usingizi kabisa.

sipo hapa kumfurahisha mtu. Over.
Kweli umefanikiwa kutokutufurahisha maana hata hujatuambia ni madude gani
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2] wakija wavuvi na stori zao wanayoyaona baharini usiku,, nyinyi mtajihisi mnaona midoli tu barabarani. kote nime experience najua udereva mpaka uvuvi,, maana kwetu ni karibu na bahari tangu nina miaka kumi na tatu nilikua navua samaki baharini,, nikaanza kwenda na usiku pia na makarabai,, tunayoyaona huko baharini usiku,, nafkiri barabarani tunaona tom n jery[emoji2] tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaseme hayo mnayoyaona huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo maana wanasiasa wanadanganya watanzania kirahisi sana.
Yaani huu uongo umeandika kama vile unawaandikia watoto wa shule za chekechea.au umetoa kwenye movie. Eti ukata bastola 9mm ukawaoneshea dirishan huo usiku nao wakaiona, pia ukawasikia wakiongea,ukajua wapi wangap kwenye gari majambazi hata hawakuweka tinted? Walifungua tu vioo uwaone nadhan waliwasha na taa kabisa uwahesabu, ulipunguza sana mwendo nao wakapunguza wakuoneneshe wapo wangap, na pia wakusikie... Na waone una bastola...

Huu uongo wa kitoto muwe mnaambiana huko shuleni wakati wa break au vijiweni. Anyway watu huwa mnatafuta jukwaa la kuuzia chai.uliona ukisema mauza uza hutaweza sema nliyaonesha bastola ukaona uje na version yako.

Haya baadaye ukakutana na mengine kwenye lorry, hayo ukayaonesha mabomu hand grenades au machine gun yakasema ...tusepe tu.
Mtu wa kupanda nabasi daima dumu utamjua tu.
Najua kwako its too good to be true!
Kwa taarifa yako mkuu na hilo si tukio la kwanza, na tembea sehemu hizo HATA LEO, na wewe uje na hadithi yako.
 
Kuna jamaa yangu amenipigia simu anasema, Kuna siku alikua anarudi Nyumbani Area C, saa sita usiku. alikua taxi driver, kufika eneo la round about ya kuelekea Area C akasimamishwa na mdada amevaa ijabu, jamaa anasema alimpa maelekezo sehemu anapotaka kwenda. jamaa anasema alipo fika maili mbili aliuliza ni njia Ipi ili afahamu mapema pa kuingilia, lakini aliona kimya akamuuliza tena akaona kimya, ikabidi apaki pembeni akageuka nyuma akakuta siti tupu. jamaa anasema alifungua mlango na kukimbia, gari aliifuata asubuhi na kwenda kukabidhi kwa mwenye gari. Ndio ikawa mwisho wa yeye ku taxi driver. ni miaka ya tisini kwa mujibu wake. jamaa anaishi Dom.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulimwambia kuna uzi wa mauzauza ya barabara ndo jamaa akakupigia kukusimlia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom