Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Nikisema sijawahi panda basi ntakuwa muongo na mpuuzi kama wengine. Nmetumia kila usafiri uliopo tanzania.but tu sipend sifa za kijinga na kitoto.uongo usio na maana.unaona movie unakuja kusimulia humu ukidhan wote ni watoto kama wewe. Muwe mnatuheshimu hata kusema uongo kunataka uwe na akili ikiwa unatka kudanganya wenye akili.

Ulichoongea ni uongo wa wazi kabisa yaan kuna hoja zako hazijakaa sawa na nmeziweka wazi hapo. Mimi nmekwambia sababu nafaham kwenye speed kubwa barabaran tena usiku huwez pata muda wa kufanya iliyoyasema ni uongo.na pia huwez jua kwenye gari jiran wapo wangap ni uongo, huwezi wasikia watu wakiongea sababu ya upepo mkali ni uongo.

Kabla hujasema uongo tumia akili hata kidogo

Mtu wa kupanda nabasi daima dumu utamjua tu.
Najua kwako its too good to be true!
Kwa taarifa yako mkuu na hilo si tukio la kwanza, na tembea sehemu hizo HATA LEO, na wewe uje na hadithi yako.
 
Hiyo ajari mpaka leo siielewi
Lile gari la kigwa lina teknolojia ya ku detect any moving object mbele yake pamoja na auto brake
Yani kwa mfano uko speed then mbele ghafla gari lingine hili hap
Lile gari litakutaadharisha usimame na baada ya sekunde kadhaa linasimama lenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi ya hivi nayo yapo?yanauzwaje...kwa hiyo hayapatagi ajali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha ha ha...jamaa yangu mmoja anasema na yeye jana tu amekutana na hayo majambazi na gari lile lile akayaoneshea SMG ndo yakakimbia yeye alikuwa anaendesha gari Cadillac SUV ya mwaka 2017.alikuwa speed 170. Baadaye akayaacha alipokanyaga mpaka speee 190.

Ha ha ha ha.... Achana na hao wanaopanda mabasi sisi wenye magari na silaha za moto tutoe stories zetu.

Mtu wa kupanda nabasi daima dumu utamjua tu.
Najua kwako its too good to be true!
Kwa taarifa yako mkuu na hilo si tukio la kwanza, na tembea sehemu hizo HATA LEO, na wewe uje na hadithi yako.
 
Ndo maana wanasiasa wanadanganya watanzania kirahisi sana.
Yaani huu uongo umeandika kama vile unawaandikia watoto wa shule za chekechea.au umetoa kwenye movie. Eti ukatoa bastola 9mm ukawaoneshea dirishan huo usiku nao wakaiona, pia ukawasikia wakiongea,ukajua wapo wangap kwenye gari majambazi hata hawakuweka tinted? Walifungua tu vioo uwaone nadhan waliwasha na taa kabisa uwahesabu, ulipunguza sana mwendo nao wakapunguza wakuoneneshe wapo wangap, na pia wakusikie... Na waone una bastola...

Huu uongo wa kitoto muwe mnaambiana huko shuleni wakati wa break au vijiweni. Anyway watu huwa mnatafuta jukwaa la kuuzia chai.uliona ukisema mauza uza hutaweza sema nliyaonesha bastola ukaona uje na version yako.

Haya baadaye ukakutana na mengine kwenye lorry, hayo ukayaonesha mabomu hand grenades au machine gun yakasema ...tusepe tu.
Acheni utoto na kutafuta sifa za kijinga
Na hatupigi stori za kufurahisha jamvi, sasa kitu hicho 9mm Mrusi, na ninacho kisheria.
Mtoko wake sawa na mzinga.
Saa mbili, tar 1 leo.
Somo: usisafiri kama bibi Tereza
 
Ha ha ha...jamaa yangu mmoja anasema na yeye jana tu amekutana na hayo majambazi na gari lile lile akayaoneshea SMG ndo yakakimbia yeye alikuwa anaendesha gari Cadillac SUV ya mwaka 2017.alikuwa speed 170. Baadaye akayaacha alipokanyaga mpaka speee 190.

Ha ha ha ha.... Achana na magari na silaha za moto tutoe stories zetu.
Mkuu AK47 SMG kisheria hairuhusiwi kwa matumizi ya raia.
 
Mimi hii imenitokea Handeni-Tanga nikiwa naendesha gari nimewapakiza ndugu zangu watatu ghafla ikatokea pikipiki ikiwa na watu watatu (mshikaki) wakiwa wamejaa upande wangu niliwakwepa marambili bila mafanikio wakajaa kwenye ngao nikasimama chaajabu ngao haitamaniki lakini pale chini hakuna pikipiki wala majeruhi.....niwiki yapili sasa bado sijapata majibu ya kilichotokea
 
Kuna siku natoka Mtwara nakuja Dar,,,kibabu kimoja,kikiwa na tenga kimeweka bata wawili,Akatuomba lifti anashuka mbagala,,tukamchukua,,chakushangaza ndio safari pekee ambayo nimesafiri bila kukaguliwa hata mara moja,na mbaya zaidi nilikuwa nimebeba MBAO NA Magunia ya Mkaa,,na hii njia yakusini,,ndio inaongoza kwa ukaguzi ,,hasahasa mageti ya maliasili,tulikuwa tukifika kwenye geti la maliasili,tunafunguliwa geti kama waheshimiwa,,,,tunaruhusiwa tu,,,natamani sana huyu babu niwe nambeba kila siku,,,mwisho wa safari babu akatuambia,,msiwe mnazarau watu,,hamjui wanamsaada gani kwenu,,haya safari njema,
,[emoji23][emoji23]mkuu hukuchukua namba za huyo mzee tuwasiliane nae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
9mm ilikusaidia kaka
Kweli kabisa mimi sina chale wala chanjo, na nasafiri sana usiku.
Tatizo kubwa ni majambazi.
Mi nina kisa cha ukweli, majambazi, au highway robbers.

Nimetoka Dar saa nne na nusu usiku.
Ni miaka takriban 15 iliyopita.
Mwendo ni wa kawaida Dar Chalinze, ile naingia Mdaula magari sasa machache na full light unaona hadi kilometa mbili.
Baada ya njia panda kwenda Ngerengere kwa mbali naona taa nyekundu, dalili ya gari.
Kwa vile sasa mwendo wangu ni kama 130~140km/hr nikalipita gari lile, na naliona Toyota Mark II.
Ile sijaenda kilometa tano naona kwa nyuma kuna gari, full light linakuja wangu wangu, tena likanipita, gari lilelile Mark II, NA LINA WATU WAWILI niliowaona.
Mda hiyo saa usiku, tano na nusu!
Nikaendelea na mwendo wangu ila nikaongeza mwendo.
Wale jamaa nafikiri nia ni kunisimamisha, lakini nikaongeza mwendo sasa 165~170km/hr!
Nikalipita!
Do, jamaa nikaanza kufikiria, jambazi lazima kumsurprise, akikuwahi yeye, basi bahati yako mbaya.
Ikaja kona tukapunguza mwendo, ila nami nikatoa 9mm mguu wa kuku.
Nikasubiri ili sasa jamaa anipite.
Kweli jamaa akakanyaga mafuta, wakati ana nipita , nikaongeza spidi kidogo ili tuwe sambamba, nikafungua dirisha na kumwelekeza mtutu.
Ee bwana kabla sijakamua, nikasikia kabisa abiria akimwambia mweziwe... twende... twende ...twende!
Mark II ili paa, na sikuiona tena hadi nafika Morogoro.
Usafiri kafiri!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikuwa Jini
Nilikuwa natokea Dar nikiwa na pikipiki aina ya Honda Benly 250 niliyokuwa natoka kuichukua Bandarini ,sikutaka kuipandisha kwenye Lori,niliamua kuendesha mwenyewe kwenda mwanza ili nipate kutalii,safari ni ndefu mno ilikuwa,nilichoka sana hasa mikononi na begani,Nilipofika Singida niliamua kulala,lakini ilipofika saa 3 Usiku nikaamua kuendelea na safari na nikaghairi kulala kwa Sababu nilihisi mwili umepata nguvu.
Nilipoanza kuteremka mlima Sekenke niliona mwanamke mrembo mno kwenye ile misitu usiku wa saa 5 eneo pweke lile lisilo na makazi ya watu zaidi ya mashimo marefu kando ya barabara ,mwanamke yule alikuwa akinisimamisha,nilipunguza mwendo na kuwasha full light ili nimwone vema,hakika alikuwa mzuri hasa,alivaa mtandio kichwani na gauni refu jekundu,alikuwa kama shombe wa kiarabu nilipomkaribia zaidi mwili wote ukasisimka ndo nikajikuta nazidisha mwendo kwa hofu,niliendesha kwa spidi ya kifo hadi Igunga,sikuendelea na safari nililala igunga ,hadi Leo huwa najiuliza sana juu ya mwanamke huyo wa ajabu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waende kigoma siku 1 au Tarime
Wakati niko mdogo huko tarime nikiwa darasa la 4 au 5
Usiku mida ya saa nane.nilikua nimelala na kaka yangu ila mi niko ukutani
Ghafla nikastuka naona watu kama watatu wanaimba "hakuna hakuna"
(Kulikua na mwanga wa taa kidogo) nikapiga kelele wakapotea ila mmoja nilimtambua ni bibi fulani wa pale mtaani

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lete visa ulivyokutana navyo baharini
[emoji2] [emoji2] [emoji2] wakija wavuvi na stori zao wanayoyaona baharini usiku,, nyinyi mtajihisi mnaona midoli tu barabarani. kote nime experience najua udereva mpaka uvuvi,, maana kwetu ni karibu na bahari tangu nina miaka kumi na tatu nilikua navua samaki baharini,, nikaanza kwenda na usiku pia na makarabai,, tunayoyaona huko baharini usiku,, nafkiri barabarani tunaona tom n jery[emoji2] tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom