Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Nasikia lile Ringi kama kuna hatari linabana pale kwenye gap.
 
Mimi ni mzoefu wa safari za usiku na sikuwahi kuona maluelue yoyote! Mimi nadhani ni imani tu. Wengi wanakutana na watu kama walevi, viziwi au vichaa wakivuka barabara na kuoanisha na imani za kishirikina. Hofu yangu ni kuona watu wanahamasishana kuua kwa kugonga bila kujali ni binadamu wenzetu.
 
Usiku una mengi sana. Mnaoendesha mna mioyo ya akajabu. Ikishafikaga saa sita usiku niko safarini sikai kwa amani kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi ni mzoefu wa safari za usiku na sikuwahi kuona maluelue yoyote! Mimi nadhani ni imani tu. Wengi wanakutana na watu kama walevi, viziwi au vichaa wakivuka barabara na kuoanisha na imani za kishirikina. Hofu yangu ni kuona watu wanahamasishana kuua kwa kugonga bila kujali ni binadamu wenzetu.
 
Kwendaaa! Kuna dereva anaanza kufuatilia alomgonga kweli? Seriously???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu. Nina uhakika wengi ni ama vichaa au walevi au walemavu (hawaoni au kusikia vizuri) na watu kwa imani zao za kishirikina wanahasishana kuua kwa kukusudia. Kweli ukifikiri elimu ni gharama basi jaribu ujinga!
 
Hakika nisiwe mwongo, nasafiri sana usiku tena pekeyangu sijawahi kuona chochote kitu. Haya ni maneno ya waafrika wenye uoga moyoni na imani za kujumlisha.
Kuna habari iliwahi kurushwa redioni, kule kishapu shinyanga wakati huo, mkuu wa wilaya alisimamishwa na babu mmoja ili amsaidie kusogeza matofali, na mkuu akasema huyu babu anasemaje huyu, aka akili sawasawa ? Akamwamuru dereva wake waondoke. Babu akakaa. Wakaingia kwenye gari wakawasha wakajiona wanaenda kwa masaa zaidi ya manne hawakuwa wamefika na no mahali pa kwenda kwa nusu saa,. Walipo simamisha gari kutoka nje wakajikuta wapo pale pale hawajaondoka. Ilibidi wamwombe mzee wampe na hela ya kuweka kibarua mtu abebe. Ndipo babu akawaruhusu wakaondoka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Malizia stori mkuu,ikawaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea kitu cha maana, at least nimepata mwanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahahhahahaaaa Huu uzi umenikumbusha kitu. Siko upande wa mauza uza ila nilifahamiana na dereva mmoja wa malori wa kukatiza nchi kama 4 hivi barani Africa. Siku moja tukiwa Bukoba akawa ananisimulia vitu anavyokutana navyo barabaeani kama dereva mchana na usiku.

Kikubwa wizi, majambazi na majangiri kuna eneo ukiacha kioo wazi wanakutupia kopo la nyuki au nyoka. Ndani ya Salina kadhaa lazima usimamishe gari kama so kulidondosha. Kifuatacho ni kupakua mizigo kisha wanakuacha uwe mzima ah umeumia hawana habari na wewe kisha wanapotelea maporini.

Kuna moja hiyo nilicheka nusura nijikojolee, naomba nisimulie kisa chenyewe kama alivonisimulia.

Jamaa yangu miaka hiyo aliajiriwa kwenye kampuni ya usafirishaji mizigo ya mwarabu mmoja wa mwanza japo alikuwa dereva tayari na alijua kuendesha. Wakiondoka na mzigo tajiri aliwaasa njiani kuna majambazi na majangiri na hawaishii kuiba tuu wanabaka pia aka kuwasodomise. Kweli wakaondoka na dreva wake kufika katikati ya pori wakawekewa kizuizi na majangiri dereva akashuka kujaribu kuwasihi wawaachie wapite na Yule utingo alibaki kwenye gari. Wakaja wakamshusha utingo wakawaambia mkitaka muende na mzigo tunachukua roba moja na tunambaka mmoja wenu. Daah wakiwa na hamaki wakasema tumshughulikie dereva utingo Rudi kwenye hadi fastaa. Kweli dereva akashughulikiwamaana aliendesha kwa tabu sana mzigo ukafika salama lakini hawakupata mzigo wa kurudi nao hivi hawakuwa na hela Yaani lori lilirudi tupu.

Siku wanarudi na mwanza yule dereva alimwambia utingo, endesha wewe mimi nipumzike kufika pori lilelile wakasimamishwa na majangiri walewale wakasema, mnarudi haya leo tumshughulikie utingo dereva pumzika, bila kusubiri wakaenda upande wa abiria wakamshusha yule jamaa na kumsodomise tena......(wakati ananisimulia nilicheka hatariii)

Yule dereva kufika kwa mwarabu akarudisha funguo kazi imemshinda.

Kisa kingine alichokutana nacho huyo jamaa yangu safari za mwanza bukoba hadi mpakani Uganda akiwa bado utingo alipata dereva ambae mkewe alikuwa na wivu balaa halafu mzigo na mtata. Maana siku majangiri wanaobaka wakiwepo kwenye pori mojawapo huwa malori wanaambiana na kukaa vituo eneo kabla ya pori na wakiondoka basi safari huendelea. Ilimpa wakati mgumu maana alimuaga mkewe naondoka jumatatu tunarudi alhamis Ila wakikutana na changamoto kama hizo za kuwakwepa majangiri wabakaji anakaa muda mrefu zaidi matokeo yake mkewe anahisi amepita nyumba ndogo. Akirudi hata na zawadi bado anakuwa na kibarua cha kumuelewesha mkewe kuwa kazi yao ni ngumu na mambo wanayokutana nayo barabarani hawezi kuelezea yote.

Siku ya siku mkewe akamwambia leo tutasafiri wote nione hizi changamoto mnazokutana nazo. Akamsihi sana mkewe bakii mkewe kagoma basi kishingo upande jamaa akakubali mkewe wasafiri wote. Hamad kati ya pori majangiri wabakaji hasa hapa, wakawashusha wote, wakasema leo mna mwanamke.... Basi nyie rudini kwenye gari leo acha tufaidi mbele na nyuma. Dereva machozi yalimtoka akiahidi day la hela kubwa Hata akope waapi sanasana aliambulia kupigwa na ubapa wa mapanga mgongoni. Mkewe kuona mmewe anataka kuuwawa, analogs kelele, basi muacheni navua nchi zote, walipomaliza mke karudi kwenye gari hoiii. Walipofika walikokuwa wanapeleka mzigo, mke akamwambia dereva, mume wangu nisamehe kweli kazi yenu in a changamoto, pole sana. Naomba nirudi na basi nyie hata mkikaa wiki mbili sina wivu tena. Alikuwa mpole maana alihisi jamaa atamuacha. Dereva akamwambia tulia tunarudi wote uzuri saa ya kurudi pori lilikuwa shwari.

Safari moja kwenye vilima vya iringa kuna maiti ya mwizi mmoja wa mizigo ya malori walimkamata wamapiga hadi akafa halafu wakamuweka kwenye kilima chenye kina kali yaani ukija na gari unastukia huyu hapa alikanywagwa na magari hadi akapotelea kwenye lami. Hilo eneo pakajaa mafuta meusiii.....

Kasinde.
 
hahahaaa,, kudadek walai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…