Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

niliwahi kung'ata hirizi mdomoni hahahahah daah maisha haya
 
Hapo kuna siku eti saa saba usiku tulikuwa na landcruiser tumetoka arusha tumewasha full maana mbele kulikuwa kweupe hakuna gari linalokuja mara kwa mbalii naona bata na vifaranga vyake kibao vinacheza barabarani mi nikamwaambia yule mwenzangu pembeni imeona mambo hayo? Jamaa ananiambia mambo gani yaani kama hakuna kitu mbele mi dereva naona yeye eti haoni nilipita kwa speed ile ile wala sikusita ndipo jamaa ananiuliza kwani ni nini nikambia bata na vifanga vyake tushavipita yaani hakuamini kabisa
 
Dania tambala bovu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna sehemu, ukitoka Mombo naenda mazinde, kuna eneo lina kosa kali sana, nilikutana na madude ya ajabu mpaka niliogopa kuendelea na safari na usiku ule sikupata usingizi kabisa.

sipo hapa kumfurahisha mtu. Over.
 
niliwahi kung'ata hirizi mdomoni hahahahah daah maisha haya
Mi iliyonishtua mara ya kwanza kusafiri na gari usiku kama saa nane hivi niko speed gari nimeweka katikati ya chack (ule mstari mweupe katikati ya barabara) maeneo ya kijijibcha mchungwa hapo tanga mara akatokezea mtu eti kabeba jeneza kichwani akaingia ghafla pale barabarani aisee nili nyoosha bila huruma wala sijui kama nilimgonga au la maana sikusimama na wala sikusikia chochote ila wenzangu waliohisi kilichoendelea pale walikemea sana kwa maombi huku safari ikiendelea
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Hii chai umeweka hadi vitunguu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japo Mimi sio dereva wala makonda nakumbuka natoka Dar kuja Mbeya mjini nikiwa na IT za kwenda Tunduma tulipofika mbuyuni Ruaha basi akatokea paka mmoja katikati ya barabara akakatiza kwenda kushoto tukiwa Speed kama 100-110 ndani ya Noah basis dereva akajisemesha maneno kadhaa akasema ngoja turudi akageuza gari kurudi Dar akasema tusiporudi pale alipokatiza paka safari yetu hatutafika salama kabisa.mauzauza yapo sana barabarani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikua siamini pia, yaliyonitokea sijui niongee nini ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…