Kwa maisha yalivyo, nimewawekea wanangu Asset hii ije iwasaidie baadaye

Kwa maisha yalivyo, nimewawekea wanangu Asset hii ije iwasaidie baadaye

Habari wanajamvi,

Kwa maisha yalivyo na yanavyoelekea huko mbeleni nimeamua kuwaandalia wanangu mali hii ije iwasaidie baadae
Nina watoto wawili wa kiume mmoja Miaka mitano na mwengine Miaka miwili. Nimeamua kila mmoja ninmnulie Ardhi ekari 2
Kila mmoja nitampandia minazi 400

Kwa nini minazi
Nimepanda minazi kwa sababu nategemea mavuno baada ya miaka 7

Mavuno ya nazi
Kama mnazi utavuna kila baada ya miezi mitatu utaweza kuvuna minimum nazi 30 kwa kila mnazi

Hesabu ikoje
Nazi 30 * minazi 400 nitapata nazi 12000. Kama nitauza kwa bei ya 500 kwa kila nazi nitapata TSH 6000000
Hapo nitavuna kila baada ya miezi mitatu yaani mara nne kwa mwaka nitapata million 24 kwa kila ekari 2
Najua kipindi kama tupo hai hiko wanangu watakua sekondari
Najua nitawasomesha bila ya pressure na pia nitakua na uwezo wa kuwapa hata mitaji.

Nimeshaanza hizi hatua na ndio ninayoendelea nayo

NB: wazazi wa Sasa tuandae kitu cha kuja kusaidia watoto wetu mbeleni ili tusije kuumiza kichwa huko mbeleni. Nb soko la nazi ni la uhakika na linakua siku hadi siku.
Tatizo ukifa tu wajanja wanakuja nyuma na kuwadhulumu Aridhi watoto wako,na wazulumishi huwa hawatoki mbali na familia yako!!
 
Unaweza kushangaa, wakikua watakata hiyo minazi, kugawa viwanja na kuviuza.

Hicho ni kizazi cha motoooo!
Hili linawezekana kabisa. Mitoto ya cku hizi! acha kabisa. Halafu kwa kuwa hajasotea mali hiyo, hataona ugumu na fedha atakayoipata anaweza kwenda kula bata na vijana wenzake au kujitumbukiza kwenye mihadarati. Inasikitisha sana. Kwa mantiki hiyo kuna kazi tena kazi kubwa ya kuwawezesha hao watoto kutunza na kuithamini mali hiyo.
 
Basi wapandie miti ya kudumu
1. Miti ya mbao/nguzo/karatasi
2. Mikorosho
3. Miti ya matunda kama machungwa,maembe, limao, parachichi
4. Miti ya viungo kama karafuu, mdalasini
5. Miti ya kuzalisha mafuta kama michikichi
Vyote hivyo 👆 👆 ni kwenye ekari mbili (2) tu za ardhi au unamshauri awaongezee maeneo? Mm naona hilo wazo lake la minazi liko vizuri zaidi kwani hajasema kuwajengea nyumba i.e watajenga wenyewe nyumba ya fashion waipendayo. Hiyo minazi unaendelea kuvuna na unabaki na miti yako tofauti na miti ya mbao ambayo unavuna mara moja halafu unabaki na sifuri -unaanza tena moja. Miti ya mbao ina changamoto nyingi zikiwamo za moto kichaa, magonjwa,soko na ushindani kati ya mbao halisi na zile za "Mchina" i.e. maganda/pumba ya mchele.
 
Back
Top Bottom