Kwa maisha yalivyo, nimewawekea wanangu Asset hii ije iwasaidie baadaye

Kwa maisha yalivyo, nimewawekea wanangu Asset hii ije iwasaidie baadaye

Habari wanajamvi,

Kwa maisha yalivyo na yanavyoelekea huko mbeleni nimeamua kuwaandalia wanangu mali hii ije iwasaidie baadae
Nina watoto wawili wa kiume mmoja Miaka mitano na mwengine Miaka miwili. Nimeamua kila mmoja ninmnulie Ardhi ekari 2
Kila mmoja nitampandia minazi 400

Kwa nini minazi
Nimepanda minazi kwa sababu nategemea mavuno baada ya miaka 7

Mavuno ya nazi
Kama mnazi utavuna kila baada ya miezi mitatu utaweza kuvuna minimum nazi 30 kwa kila mnazi

Hesabu ikoje
Nazi 30 * minazi 400 nitapata nazi 12000. Kama nitauza kwa bei ya 500 kwa kila nazi nitapata TSH 6000000
Hapo nitavuna kila baada ya miezi mitatu yaani mara nne kwa mwaka nitapata million 24 kwa kila ekari 2
Najua kipindi kama tupo hai hiko wanangu watakua sekondari
Najua nitawasomesha bila ya pressure na pia nitakua na uwezo wa kuwapa hata mitaji.

Nimeshaanza hizi hatua na ndio ninayoendelea nayo

NB: wazazi wa Sasa tuandae kitu cha kuja kusaidia watoto wetu mbeleni ili tusije kuumiza kichwa huko mbeleni. Nb soko la nazi ni la uhakika na linakua siku hadi siku.
Hata mimi nimeshawaza kulima.zao la nazi.

Bado nawaza eneo gani zinastawi zaidi ktk mikoa karibu na Dar.

Zao la nazi linazidi kupotea siku hadi siku
 
Write your reply...Wazo nzuri.
Tumia kanuni hii
Idea Plan Action.
 
mkuu unajua nasisitiza hivi kwa sababu nilipata kipeperushi cha wale jamaa wa tari nikaona wao wameandika hii nazi 40 kwa mwaka
Hapana sio kweli ni kwa muangusho mmoja na kwa mwaka unaweza kuangusha mara nne au zaidi
Unaweza kitembelea mikoa inayolima mazi ukajifunza zaidi
 
mkuu unajua nasisitiza hivi kwa sababu nilipata kipeperushi cha wale jamaa wa tari nikaona wao wameandika hii nazi 40 kwa mwaka
Hata mim nilijua hivyo kwamba ni nazi 40 kwa mwaka. Na niliplani niwe na ekari hata moja ya minazi. Ila itabidi niongeze moja nipige chini kupanda miembe ya kisasa. Bora nazi tukilitazama soko
 
Utakuja kukuta umeuza mwenyewe.

Watoto wape elimu mengine watafanya wenyewe.
 
Back
Top Bottom