Kwa maisha yalivyo, nimewawekea wanangu Asset hii ije iwasaidie baadaye

Tatizo ukifa tu wajanja wanakuja nyuma na kuwadhulumu Aridhi watoto wako,na wazulumishi huwa hawatoki mbali na familia yako!!
 
Nimeandaa hivi ili kama niko hai nisije umiza kichwa kuja kuwahudumia kama sitakuwepo wakija kuuza ni ujinga wao kwani mimi sitashuhudia mateso yao pindi wakipigwa na maisha
KunA mipango mji wanaweza kupapima viwanja hapo...nenda na moja kichwani
 
Unaweza kushangaa, wakikua watakata hiyo minazi, kugawa viwanja na kuviuza.

Hicho ni kizazi cha motoooo!
Hili linawezekana kabisa. Mitoto ya cku hizi! acha kabisa. Halafu kwa kuwa hajasotea mali hiyo, hataona ugumu na fedha atakayoipata anaweza kwenda kula bata na vijana wenzake au kujitumbukiza kwenye mihadarati. Inasikitisha sana. Kwa mantiki hiyo kuna kazi tena kazi kubwa ya kuwawezesha hao watoto kutunza na kuithamini mali hiyo.
 
Basi wapandie miti ya kudumu
1. Miti ya mbao/nguzo/karatasi
2. Mikorosho
3. Miti ya matunda kama machungwa,maembe, limao, parachichi
4. Miti ya viungo kama karafuu, mdalasini
5. Miti ya kuzalisha mafuta kama michikichi
Vyote hivyo πŸ‘† πŸ‘† ni kwenye ekari mbili (2) tu za ardhi au unamshauri awaongezee maeneo? Mm naona hilo wazo lake la minazi liko vizuri zaidi kwani hajasema kuwajengea nyumba i.e watajenga wenyewe nyumba ya fashion waipendayo. Hiyo minazi unaendelea kuvuna na unabaki na miti yako tofauti na miti ya mbao ambayo unavuna mara moja halafu unabaki na sifuri -unaanza tena moja. Miti ya mbao ina changamoto nyingi zikiwamo za moto kichaa, magonjwa,soko na ushindani kati ya mbao halisi na zile za "Mchina" i.e. maganda/pumba ya mchele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…