Hakuna sehemu hata moja Africa ambako jeshi limefanikiwa kufanya hivyo.
Kila sehemu jeshi lilipochukua madaraka kwa minajili ya kuondoa uongozi mbovu liliharibu zaidi.
Angalia Zaire ya Mobutu.
Angalia Nigeria tangu Johnson Aruiyi-Ironsi.
Angalia Liberia tangu Samuel Doe.
Hata pale tawala za kijeshi ziliposifiwa, muziki ni ule ule.
Angalia Misri na Gamal Abdel Nasser. Matatizo ya uongozi wa kijeshi yanaiandama mpaka leo.
Angalia Burkina Faso na Thomas Sankara. Matatizo ya uongozi wa kijeshi yanaiandama mpaka leo.
Tatizo letu Waafrika wengi, tunapenda majibu ya mkato, utatuzi rahisi kwa maswali magumu.
Badala ya ku focus kuwa na jamii inayojitambua, tunataka viongozi fulani watufanyie kazi ya kujitambua kwa ajili yetu.
Ndiyo maana wengi tunapenda uongozi wa kijeshi. Uongozi ambao mtu anayejitambua hatakiwi kuushabikia.
Najua uongozi wetu mbovu unatushawishi tupende njia ya mkato ya kupata uongozi wa kijeshi. Lakini uongozi wa kijeshi hauna guarantee ya kuwa mzuri. Worse still, historia inatuonesha uongozi wa kijeshi umeiharibu sana Africa.
Kuanzia mapinduzi ya kwanza ya kijeshi yaliyomuondoa Sylvanus Olympio Togo January 13 1963.
Sasa, kwa rekodi hiyo, kwa nini mtu yeyote mwenye akili atake uongozi wa kijeshi?