Kwa maneno ya Rais Samia nyaraka zilizovuja mtandaoni kuhusu tuhuma za Ufisadi ni za kweli

Ni muda sasa umefika tushikamane kumtoa mkoloni mweusi madarakani.
 
Simuoni hata mmoja mwenye viashiria vya uzalendo jeshini zaidi ya uchawa.
Kwenye suala la utawala wa kijeshi, suala si uzalendo.

Suala ni kanuni ya civilian control of the military. Hii ni sehemu ya utawala bora.

Hata kama wangekuwa na uzalendo leo, unajuaje wakichukua nchi kijeshi wataendelea na uzalendo?

Mfumo wa kijeshi hauwajibiki kidemokrasia, sasa mtu akishapata kuwa na madaraka kijeshi utajuaje kuwa ataendelea kuwa mzalendo?

Afrika imejaa mifano ya watawala wa kijeshi walioanza kwa gia ya uzalendo, lakini walipopata madaraka wakaonekana wanacheza mpira kukwepa utawala bora kupita Maradona.
 
Kwa hiyo Mkuu ni nini kifanyike ili huu uongozi wetu wa kiraia uweze kutawala kwa kuserve interests za wananchi?
 
Anaongea hayo hajui nchi yetu ina Sheria kabisa ya kuwalinda watoa taarifa za siri za Ufisadi. Sheria hiyo ni Whisleblower and Witness Protection Act na ilitungwa na kupitishwa kabisa na Bunge.
Sasa we unaona yule zinamtosha?
 
Mwenye nguvu ya kufanya maamuzi sio mzalendo halafu anataka asiye na nguvu awe mzalendo ? Mbona kama Rais sikuelewi ? Labda wanajamii wanisaidie?
 
JWTZ huko hakuna kitu kinaitwa uzalendo mkuu. Taifa hili kila mmoja anaangalia anapata nini kwa wakati uliopo basi. Sasa hivi kila kitu kwenye hii nchi ni mali ya ccm mpaka hao jwtz
 
JWTZ huko hakuna kitu kinaitwa uzalendo mkuu. Taifa hili kila mmoja anaangalia anapata nini kwa wakati uliopo basi. Sasa hivi kila kitu kwenye hii nchi ni mali ya ccm mpaka hao jwtz
Ndo mana nimewalaumu
 
Uko sahihi mkuu,jeshi utalilaumu Bure,kikubwa wananchi tuamke ,sasa kama wananchi hatuchukui hatua unadhani kweli tutafika.

Mimi naamini katika nguvu ya umma,na hatua itakayotupelekea kumuondoa ofisini huyu mzanzibar ni kususia uchafuzi(uchaguzi) wake na baadae kuingia barabarani,hawawezi kutuua wote
 
A Alishatoa amri kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
 
Kwa hiyo Mkuu ni nini kifanyike ili huu uongozi wetu wa kiraia uweze kutawala kwa kuserve interests za wananchi?
Kitu cha kwanza hao wananchi waelimike kuhusu haki zao na wazidai.

Hakuna utawala utakaowapa watu haki zao kwa utawala huo kupenda tu.

Haki zinadaiwa.

Sasa Watanzania hawa wanaoona wanafanyiwa hisani na "Mama Samia" kwa kupewa haki zao za kikatiba hawawezi kuuweka uongozi kaymyika mstari.

Watanzania hawa waoga hawawezi kunyoosha mambo.

Hatuwezi kuepuka kazi ngumu ya kubadili fundamentals. Hatuwezi kuepuka kazi kubwa ya uchambuzi wa kina wa matatizo ya jamii yetu.

Hizi habari za kutafuta shortcuts za kuwatwika wanajeshi wajibu wa kunyoosha mambo ni jitihada za jamii kukimbia kazi yake na kutafuta jibu rahisi kwa swali gumu.

Yani ni hivi, hata mkiwaondoa CCM na kuwaweka CHADEMA. Au mkiwaondoa CCM na kuwaweka wanajeshi, au mkiwaondoa CCM mkawaweka techocrats tu wasio na chama, kama wananchi wenyewe wasipojiongeza kuelimika, kufuatilia uongozi na kuusimamia ukae kwenye mstari, wananchi watapigwa tena vile vile tu.
 
Sababu anajua enzi JPM waliucheza sana huo mchezo wa kumpa mange nyaraka
 
Ndugu mtumishi usijifanye wewe ni mzalendo eti unatoa taarifa za siri watakaoteseka ni wewe na familia yako hakuna lingine
 
Hapo hata ukiliweka jeshi, kama wananchi hawajajiongeza kufuatilia mambo, hata hilo jeshi nalo baada ya miaka michache utakuja kulilaumu vile vile tu.
 
Luteni Jerry Rawlings aliweza kuiweka Ghana kwenye njia sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…