Kwa maneno ya Rais Samia nyaraka zilizovuja mtandaoni kuhusu tuhuma za Ufisadi ni za kweli

Natamani watanganyika wote tuache kupiga kura aaisee. Maana njia ya direct confrontation na hawa watu zinaogopeshwa wengi bora tutumie hii ya boycott kwenye kupiga kura tu
Ni kama vile tumelala kabisa tumekuwa majinga kupitiliza
 
Kweli kabisa maana hata wanaolalamikiwa sasa hivi ni watu kutoka katika jamii yetu. Hakuna tunda linaloanguka mbali na mti. Jamii ikibadilika na uongozi wa nchi utabadilika eventually.
 
General Al-Sisi wa Misri amejitahidi kuiweka Misri katika muenendo angalau mzuri kuliko wa Mubarak na Morsi baada ya kukosena utawala wa kiraia wa kueleweka.
 
Wananchi watajiongeza vipi kuelimika wakati Mfumo wa elimu yetu haupo sawa? Na hiyo elimu yenyewe ni gharama kwa wengi kuimudu?

Pia huoni sisi watanzania naturally tu ni waoga wa asili? Kwasababu hata wachache waliojiongeza wakaelimika ni waoga na wameamua kuabudu na kusifia.
 
Sijui ni ujinga au ni upumbavu au ni nini hasa!

JWTZ halina wajibu wa kushughulika na ufisadi.
 
General Al-Sisi wa Misri amejitahidi kuiweka Misri katika muenendo angalau mzuri kuliko wa Mubarak na Morsi baada ya kukosena utawala wa kiraia wa kueleweka.
Al-Sisi kaondoka kwenye utawala wa kijeshi na kapata mandate ya wananchi kwenye kura za kuchaguliwa kidemokrasia.
 
Sijui ni ujinga au ni upumbavu au ni nini hasa!

JWTZ halina wajibu wa kushughulika na ufisadi.
Waafrika wengi ni wavivu.

Wanapenda kutumia nguvu kuliko akili.

Hivyo wanaona jeshi ndiyo jibu.

Wanapenda kuwaachia wachache kazi ya kunyoosha mambo, kazi ambayo ni ya watu wote.

Hivyo wanawaachia kazi wanajeshi.

Wengine wanapenda magwanda ya jeshi tu.

Ndiyo maana hata viongozi wa kiraia washawajulia wanavaa magwanda ya kijeshi kuwavutia tu.

Afrika watu wajinga na wavivu wengi sana bado.

 
Kwanini unataka kufanya Marekani iwe ndiyo topic wakati hatuzungumzii Marekani hapa?

Huoni kuwa hii ni "whataboutism"?

Unaelewa "whataboutism" ni nini?
Whataboutism or whataboutery (as in "what about ...?") is a pejorative for the strategy of responding to an accusation with a counter-accusation instead of a defense against the original accusation. Whataboutism.

Whataboutism - Wikipedia​

 
Ndugu mtumishi usijifanye wewe ni mzalendo eti unatoa taarifa za siri watakaoteseka ni wewe na familia yako hakuna lingine
Mandela na wenzake wangeogopa kuteseka wao na famikia zao Afrika Kusini ingekuwa wapi?

Nyerere na wenzake wangeogopa kuteseka wao na familia zao Tanzania ingekuwepo?
 
Hawajui hawa wajinga
Rawlings alileta hyperinflation na debt crisis Ghana.

Ujinga ni kumsifia rais aliyeleta hyperinflation na debt crisis.

Na hata huyo Rawlings alijiondoa jeshini na kupata mandate ya wananchi kwenye ballot box.
 
Mandela na wenzake wangeogopa kuteseka wao na famikia zao Afrika Kusini ingekuwa wapi?

Nyerere na wenzake wangeogopa kuteseka wao na familia zao Tanzania ingekuwepo?
Sio kila mtu ni Mandela, sio kila mtu ni Nyerere...kwenye mtandao tupo vizuri kujazana upepo lakini kwa ground yakikukuta ndio utaelewa. Hauwezi kupambania watu waliolala.
 
Hizi data wamezifeed mabeberu kuonyesha kuwa hajafanya kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…