Kwa Mara ya kwanza Napongeza Ubunifu alioufanya Makonda Arusha

Kiwanda kingine?
.Si alisema kwa sasa zinatengenezwa Arusha na wanaziuza hadi Uingereza?
 
Oooh sawa. Ila hata kwa kulichukua na kulifanya liwe namna lilivyofanywa anastahili pongezi zetu.

Nategemea kuwaona Mawaziri wa Utalii na Habari wakishiriki kulipa publicity kubwa hili tukio ili liwe na manufaa tuliyoyasema humu.
Hivi unajua rushwa aliyovuta kulibeba hili swala? yule huwa haendi bure
 
Sidhani kama ni kiwanda cha Land Rover wenyewe. Nimezungumza kama kampuni husika wenyewe wataamua kufungua kiwanda chenyewe hapa nchini.
Uongozi wa Tanzania ni wa hovyo hakuna mtu atakuja kufungua kiwanda kikubwa hapa maana sera za hapa zinategemea matamko ya Rais aliyepo madarakani, alijaribu Dangote lakini mwisho anasua sua tu sababu ya sera mbovu na kodi za kijinga.
 
Hilo halina ubishi. Ila kama wameweza wale kiwanda cha ndege ndogo kule Morogoro hata hawa wanaweza kuja
 
Royal tour imeleta nini mpk leo na mabilioni iliyotumia? kila RC/DC ndiyo ilikuwa habari ya mjini
Sizingumzii Royal Tour kama Royal Tour. Ila kwa takwimu zilizopo kwenye ukanda wa Afrika sisi ni moja ya nchi zilizofanya vizuri sana kwenye sekta ya utalii kwa mwaka huu kama sikosei. Limerushwa sana kwenye blogs za kimataifa wiki kadhaa zilizopita.
 
Sidhani kama kiwanda cha Land Rover wenyewe. Nimezungumza kama kampuni husika wenyewe wataamua kufungua kiwanda chenyewe hapa nchini.
Lakini ulimsikia aliposema zinatengenezwa hapa Arusha na wanaenda kuwauzia Waingereza?
Hakusema zinakarabatiwa.
 
Hilo halina ubishi. Ila kama wameweza wale kiwanda cha ndege ndogo kule Morogoro hata hawa wanaweza kuja
Baadae kitakufa, wakati nakuwa nilikutana na kilimo kwanza ikafa, ikaja BRN ikafa, serikali ya viwanda ikafa(viwanda mia 3 kila mkoa ya Jafo), royal tour ikafa, leo maigizo ya land rover sijui hakuna lolote, ukiambiwa budget na kitakachopatikana ni mbingu na ardhi, TRA huwa wanasema wamekusanya 3T lakini huwezi kusikia wanasoma mapato na matumizi hata siku moja ni utapeli tapeli tu
 
Let's hope for the best!
 
Sizingumzii Royal Tour kama Royal Tour. Ila kwa takwimu zilizopo kwenye ukanda wa Afrika sisi ni moja ya nchi zilizofanya vizuri sana kwenye sekta ya utalii kwa mwaka huu kama sikosei. Limerushwa sana kwenye blogs za kimataifa wiki kadhaa zilizopita.
Broo nimezaliwa kaskazini Arusha haijawahi kushuka kiutali isipokuwa kipindi cha corona 2020-2021 na sera mbovu za Magu, ndiyo maana Arusha ina hoteli nyingi sn za kitalii kuliko mji wowote hapa EAC
 
Broo nimezaliwa kaskazini Arusha haijawahi kushuka kiutali isipokuwa kipindi cha corona 2020-2021 na sera mbovu za Magu, ndiyo maana Arusha ina hoteli nyingi sn za kitalii kuliko mji wowote hapa EAC
Takwimu zinaonesha mwaka jana na mwaka huu Tanzania ndo tumefanya vizuri na hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari na takwimu kutoka nje ya Tanzania.

So hata kama tulikuwa tunafanya vizuri ila hivi karibuni tumekuwa tunafanya vizuri zaidi.
 
Samia ajaleta impact yeyote kwenye utalii, hayo wanayasema ambao hawaujui utalii!
 
Takwimu zinaonesha mwaka jana na mwaka huu Tanzania ndo tumefanya vizuri na hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari na takwimu kutoka nje ya Tanzania.

So hata kama tulikuwa tunafanya vizuri ila hivi karibuni tumekuwa tunafanya vizuri zaidi.
Soma ripoti za kuanzia 2000-2016 ndiyo ulinganishe na leo, kumbuka nyuma matumizi ya internet, social media kwa Tanzania yalikuwa chini sn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…