Asante Mungu wewe huna choyo. Jina lako lipewe sifa, baba bariki na wengine ambao hawana kazi wapate hata kidogo.
Baba wakumbuke wote wasio na kazi wanaangaika bila msaada , kwa wakati huu ambapo hawawezi kuhudumia wazazi baba wewe simama walinde na maradhi na majanga ya aina yeyote.
Baba hata wale walio na kazi bariki hicho kidogo wanachokipata lakini pia wakumbuke kusaidia wazazi pia wengine.
Baba na nakuomba sala hii nakuomba uipokee kwa niaba ya wote tuliosoma hapa, najua kabisa sijui kuomba ipasavyo ila pokea pokea maombi haya hivyo hivyo.
Mungu baba kubwa kuliko yote, ninakuomba utulindie wazazi waone mafanikio yetu. Amina.