Kwa mara ya kwanza nimejiunga Rasmi na Chama cha Siasa nchini

Kubwa zaidi kwa kuwa chama kilicho madarakani ni chama nyonyaji.

Mfano, niliachishwa kazi tokea 2019 mwezi wa pili, lakini mafao yangu yaliyokuwa yakipelekwa NSSF, mpaka leo tarehe 6/6/2021 sijawahi kupewa.

Ngoja niishie hapa kwanza.
Kweli hiki ni chama cha majahili
 
Hongera sana kwa kujikomboa kiakili
 
Ndugu yetu karibu sana kwenye kivuli na mahali salama tuipambanie cdm yetu ili hatimaye itupatie uhuru wa kweli.
 
Kubwa zaidi kwa kuwa chama kilicho madarakani ni chama nyonyaji.

Mfano, niliachishwa kazi tokea 2019 mwezi wa pili, lakini mafao yangu yaliyokuwa yakipelekwa NSSF, mpaka leo tarehe 6/6/2021 sijawahi kupewa.

Ngoja niishie hapa kwanza.
Kwa kujiunga na CHADEMA ndiyo itakuwa suluhisho la wewe kulipwa mafao yako na NSSF?
 
CCM ilimuondoa Mkoloni ikajisahau na kujisimika kuwa Wakoloni Weusi ikafikia Maraisi wastaafu kumuombea Bwana Dikteta atawale milele
CCM imejisahau CHADEMA pia ni Chama cha Kitanzania Kizalendo kwanini tusitusikipe Madaraka tujaribu Siasa mbadala.
 
EeeeNHeeee!

Siwezi kamwe kukupongeza mtu kama wewe kuwa mwanachama wa chama chochote. Bila shaka mwakani, wakati kama huu utatutangazia tena ulivyofanikiwa kuwa mwana CCM!

Sikulaumu, kwa maana ndivyo ilivyo hapa kwetu. Watu hawana jambo wanaloliamini na kulisimamia. Wanakwenda tu na upepo kadri unavyovuma.
 
Hayo ni maoni yako, hupaswi kupingwa, japo uko wrong.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…