Ndugu yanguuuuu! Temea mate chini.
Hivi ninavyoongea nimenuniwa Leo siku ya 5. Nilimpata Demu akawa na maelezo yeye ni tofauti na waawake wengine wanaoombaomba hela, yeye haombi Mwanaume akitaka amhudumie mwenyewe siyo kumsumbua na mizinga kila mara, kwanza yeye ni mjasiriamali anauza nguo za kike za kukopesha, yaani yalimtoka nikajua nimepata. Nimekaa naye mwezi mzima nanunua vitu vidogo vidogo maana formula yangu ni NOT MORE THAN 10. Siku moja ghafla anakuja na huzuni, Dear mzigo wangu umekwama Dar mwenye duka ananidai 540,000/- naomba unipush! Na kweli nimempush!