Kwa mara ya kwanza nimempata mwanamke asiyeomba pesa

Kwa mara ya kwanza nimempata mwanamke asiyeomba pesa

Kuna wakina dada wanachakalika mkuu, wanapiga kazi kama hawana akili nzuri. Nimeshuhudia wawili. Mmoja kwenye mgahawa, mwingine anaka shop kake tu ka uongo na ukweli. Nimefuatilia mahali wanapoishi, nimegundua ni wa kawaida sana kimaisha!

Huyu wa hotel nimejaribu kumtupia nyavu, kakubali, nikampatia elfu tano ya vocha akaikataa!

Kuna baadhi ya wanawake kama hawa wanatakiwa kusainiwa rasmi kwenye kundi la watu, tuwatoe kwenye kundi la vitafunwa!

Yaani umpe mtu buku tano utegemee apokee? Hizo ni dharau. Watu vocha wanatoa elfu 50 wewe unampa buku 5 kakataa halafu unaona hapendi hela?
 
Hao tunawaita "G/mboto land mines" siku litakapolipuka utajikuta kwa mkapa stadium na hujui umefikaje Mkuu
 
Wasikutishe mkuu! Mimi namaliza mwaka wa4 huu bila kuombwa hata hela ya vocha wala nauli na bado napendwa vizuri na nahudumiwa vizuri kwa nafasi yangu [emoji94] ( Neno ilo litaleta ukakasi kidogo kwa wazee wasio na dogo, NAHUDUMIWA NA MWANAMKE )
Sasa kama unahudumiwa na mwanamke unataka akuombe nini? Damu au?
 
Back
Top Bottom