Kwa mara ya kwanza nimeona mwanaume analia kwa sababu isiyohusisha msiba wala mapenzi

Kwa mara ya kwanza nimeona mwanaume analia kwa sababu isiyohusisha msiba wala mapenzi

Kama ili ujue rafiki yako alilala na binamu wakapata mtoto inabidi uende kwao ushuhudie akisemwa huyo siyo rafiki yako.

Ndiyo sababu umeweza kuja kumuanika humu.

Wanaume ambao tuna urafiki ishu kama hizo hua tunaambiana hata kwenye simu, kama mzee ni tatizo tunasema. Tunajua pia mshkaji sasa hivi anatembelea chaki.

Umeenda pale imekua kama vile kila kitu unakiona hapo, siyo rafiki yako
 
Kama ili ujue rafiki yako alilala na binamu wakapata mtoto inabidi uende kwao ushuhudie akisemwa huyo siyo rafiki yako.

Ndiyo sababu umeweza kuja kumuanika humu.

Wanaume ambao tuna urafiki ishu kama hizo hua tunaambiana hata kwenye simu, kama mzee ni tatizo tunasema. Tunajua pia mshkaji sasa hivi anatembelea chaki.

Umeenda pale imekua kama vile kila kitu unakiona hapo, siyo rafiki yako
au ni yeye mwenyewe
 
Nilikuwa katika pitapita zangu za kawaida pale Ubungo Kibangu, lengo likiwa kumtembelea rafiki yangu wa zamani ambaye tulisoma naye sekondari. Ni kijana wa miaka 28, mcheshi na mwenye kipaji kikubwa katika mambo ya filamu. Hata hivyo, kwa sababu ambazo sikuwahi kujiuliza, hakufanikiwa kumaliza chuo kikuu, na maisha yake kwa sasa yamejikita nyumbani kwa wazazi wake.

Nilipofika kwake, tulikaa sebuleni tukibadilishana mawazo huku tukitazama runinga. Rafiki yangu alinitambulisha kwa mtoto wake mdogo, ambaye pia anaishi naye hapo nyumbani. Kwa muda, kila kitu kilionekana kuwa sawa—starehe ya kawaida ya marafiki waliokuwa wanapoteza muda pamoja. Lakini mambo yalibadilika ghafla baada ya kusikia honi ya gari ikilia getini.

Baba yake aliingia ndani kwa haraka. Hakuwa na muda wa kusalimiana nasi. Alitupita moja kwa moja bila hata tabasamu, hali iliyomfanya rafiki yangu kuonekana mwenye huzuni. Nilijaribu kuhamisha mawazo kwa kujadili muziki uliokuwa ukiimba kwenye runinga, lakini hali ya ukimya ilikuwa nzito.

Dakika chache baadaye, baba yake alirudi sebuleni akiwa tayari kuondoka. Rafiki yangu alijaribu kumfuata ili kuzungumza naye faragha, lakini kwa hasira baba yake alimkemea na kumtaka azungumze hapo hapo. Maneno yaliyofuata yalikuwa kama kisu kilichochanua majeraha ya ndani kwa rafiki yangu:
"Rafiki yako anajua kuwa nakulisha wewe na mwanao? Najua unataka hela ya madaftari, lakini tayari nimemwachia bibi yako."

Nilihisi aibu na huzuni kwa niaba ya rafiki yangu. Baba yake aliongea mambo mengi yasiyostahili mbele ya wageni, mambo ambayo hakika hayakuwa ya lazima. Niliona jinsi rafiki yangu alivyokuwa akijaribu kudhibiti hali, lakini baba yake hakumpa nafasi. Mwisho wa yote, baba yake aliondoka kwa hasira, na rafiki yangu alikaa kimya, akiwa ameinamisha kichwa huku mikono ikishika uso wake.

Niliamua kuondoka, lakini nilipokuwa napanga safari ya kurudi nyumbani, nilimsikia rafiki yangu akilia kimya kimya. Ilikuwa huzuni ya ndani, kilio cha mtu mzima aliyefika mwisho wa uvumilivu wake. Niliamua kumpeleka kwenye baa iliyo jirani, walau kunywa soda na kupunguza mawazo.

Tulipokuwa tukizungumza, alifunguka mambo mengi. Alinieleza kuwa mtoto wake ni matokeo ya uhusiano wake wa kifamilia na binamu yake, jambo ambalo linamletea changamoto nyingi. Pia alikiri kuwa alikuwa na tatizo la pombe ambalo linajirudia kila mara. Nilipomsikiliza, nilitambua kuwa mazingira aliyokuwa akiishi yalichangia kwa kiasi kikubwa hali yake. Baba yake alivyokuwa akimkandamiza kimaneno na kihisia, ni wazi kuwa alihisi kushindwa na maisha.

WALEZI NA WAZAZI, JIFUNZENI NAMNA YA KUDEAL NA VIJANA WENU

Sio kila mzazi anaelewa uzito wa maneno yake kwa watoto wake, hasa wale ambao bado wanahangaika kujipambania maishani. Kukatisha tamaa, kuwadhalilisha hadharani, au kuwaonyesha dharau kunaweza kuwa sababu kuu ya tabia zinazokufedhehesha. Walevi, watukutu, au wavivu mara nyingi wanakuwa hivyo kutokana na mzizi wa tatizo ambao unahusisha jinsi walivyolelewa.

Mara nyingi, tunahitaji huruma na ushirikiano zaidi na watoto wetu. Kama baba wa rafiki yangu angekuwa na uvumilivu na kujenga uhusiano wa karibu na kijana wake, pengine angempata rafiki badala ya mzigo. Tatizo si pombe tu, bali ni maisha yanayompelekea kijana huyo kushikilia pombe kama kimbilio lake pekee.

Siku hiyo, niliondoka nikiwa nimechanganyikiwa na huzuni. Mwanga uliokuwa machoni mwa rafiki yangu alipokuwa kijana umeshapotea. Sasa anaishi maisha yaliyojaa majuto, aibu, na matumaini yaliyoyeyuka. Wazazi, msisahau kuwa wakati mwingine unachohitaji kufanya kuokoa maisha ya kijana ni kumwelewa na kumpa nafasi ya kuzungumza. Mwisho wa siku, maisha ni mchanganyiko wa mapambano na msaada—hata kutoka kwa familia.
Nanukuu: " Ni kijana wa miaka 28,.......Hata hivyo, kwa sababu ambazo sikuwahi kujiuliza, hakufanikiwa kumaliza chuo kikuu, .... alinitambulisha kwa mtoto wake mdogo, ambaye pia anaishi naye hapo nyumbani. ...mtoto wake ni matokeo ya uhusiano wake ...na binamu yake, jambo ambalo linamletea changamoto nyingi. Pia alikiri kuwa alikuwa na tatizo la pombe ...... na maisha yake kwa sasa yamejikita nyumbani kwa wazazi wake."
Sasa vijana hebu jiulizeni: Je, mzazi hakuwahi kumuonya dhidi ya tabia na mwenendo wake tangu akiwa anakua, anaenda shuleni na kujiepusha na mambo ya wakubwa kabla ya wakati????
Wahenga alisemaga "Majuto ni mjukuu huja kinyume". Hapo kijana /rafiki yako anavuna alichopanda. Kijana ameharibika. Ni ngumu sana kumrekebisha kwani ilitakiwa Samaki mkunje akingali mbichi. Huyo ni mtu mzima ameshakomaa sana.
Mzazi/Mlezi labda alichelea au hakuzingatia "Spare the rod; spoil the child"
naye kwa wakati wake anavuna alichopanda kwa kijana wake huyo. Hakumsimamia kidete, hakuona umuhimu wa kutembeza kichapo kwa huyo kijana wake pale alipokuwa ana anza kuzembea au anapotoka au kutotii na ujeuri dhidi ya maelekezo kutoka kwake kama mzazi au mlezi (hilo ni kasoro iliyopo kwa wazazi wengi wa kisasa). Halafu hatujasikia lalamiko au kero kutoka kwa mama yake huyo kijana rafiki yako au mama hayupo?? na mambo yamekaaje -pengine mama ana mchango mkubwa sana kwenye hali iliyopo.
Hayo niliyobold ni kuonesha udhaifu uliokuwepo kwa kijana- rafiki yako.
 
Hiyo kijana anatakiwa apigwe na makonzi mbele ya wageni mpuuzi sana hiyo,amekaa nyumbani kwa babaye na mtoto wake halafu anatetewa na watu humu,halafu kazaa na binamu yake ambaye ni dada yake hiyo analeta laana kwenye familia
 
Hujamaliza ulimshauri nini rafiki yako?
Na kwanini lawama zote umeelekeza kwa baba ake je kitendo cha rafiki kuzaa na binamu yake na bado kuishi na mtoto wake hapo nyumbani huku na yeye akimtegemea baba ake sio kibaya?
Kwanini asitoke akatafute maisha kwingine kuliko kukaa hapo home?

Nina hakika ungesikia upande wa pili wa baba ake ungestaajabu sana na usingeamini kama rafiki yako ndie huyo anayezungumziwa.
Nilimshauri ahame apange somewhere maana akiweza kumudu majukumu ya kodi basi hata mengine yataenda vizuri
 
Nilimshauri ahame apange somewhere maana akiweza kumudu majukumu ya kodi basi hata mengine yataenda vizuri
Kuhama ni sawa lakini nadhani angeenda kwa hatua kama ifuatavyo:
1. Amwombe sana msamaha mzazi/mlezi wake; ikibidi atafute hata mtu mzima wa kumsaidia. zingatia alifanya kosa kubwa sana kuzaa na binamu i.e. dada wa baba yake. It is a shame - unamwonesha baba yako kwamba ww bingwa unajua kuliwasha rungu??
2. Amwombe baba yake Mzazi mkopo ili akaanzie maisha mahali pengine - kupanga.
3. Asichague kazi. Kazi yoyote halali itakayomjia mbele yake yy afanye.
 
Kuhama ni sawa lakini nadhani angeenda kwa hatua kama ifuatavyo:
1. Amwombe sana msamaha mzazi/mlezi wake; ikibidi atafute hata mtu mzima wa kumsaidia. zingatia alifanya kosa kubwa sana kuzaa na binamu i.e. dada wa baba yake. It is a shame - unamwonesha baba yako kwamba ww bingwa unajua kuliwasha rungu??
2. Amwombe baba yake Mzazi mkopo ili akaanzie maisha mahali pengine - kupanga.
3. Asichague kazi. Kazi yoyote halali itakayomjia mbele yake yy afanye.
Haya ndiyo mashauri ya kumshauri mtu,siyo kumlaumu mzazi kwa ujinga wa mtoto,kongole sana ndugu
 
Back
Top Bottom