Kwa mara ya kwanza nimeona mwanaume analia kwa sababu isiyohusisha msiba wala mapenzi

Kwa mara ya kwanza nimeona mwanaume analia kwa sababu isiyohusisha msiba wala mapenzi

Seems na wewe umesapoti rafiki yako kuzaa na binamu yake

Mshauri atoke hapo akatafute kazi
Akiwa na pesa itafuta aibu zake zote
Anakaa hapo anaendelea kulia Lia itamsaidia nini
 
Hawa wazazi ukifanikiwa ndio wanakupenda

Wazazi wachache sana hasa wakina mama ndio wanampenda mtoto ata akiwa situation gani, wazee wanazinguaga sana. Yalishanikuta
Wamama wa hivi ndio wanafuga vibaka, panya road na majambazi. Hongera mshua wako kukukazia huenda ungekuwa kipanya road kikuu sasa hivi
 
Hawa wazazi ukifanikiwa ndio wanakupenda

Wazazi wachache sana hasa wakina mama ndio wanampenda mtoto ata akiwa situation gani, wazee wanazinguaga sana. Yalishanikuta
Kina mama ndio wanaoharibu vijana wao kwa kuwatetea na kuwafichia Siri, Tena baba akisema mama anapanda juu ya meza kumtetea mtoto mavuno ndio hayo, miaka 28 nyumbani anatafuta nini?
 
Kina mama ndio wanaoharibu vijana wao kwa kuwatetea na kuwafichia Siri, Tena baba akisema mama anapanda juu ya meza kumtetea mtoto mavuno ndio hayo, miaka 28 nyumbani anatafuta nini?
Anapanda juu ya meza😃😃
 
Hawa wazazi ukifanikiwa ndio wanakupenda

Wazazi wachache sana hasa wakina mama ndio wanampenda mtoto ata akiwa situation gani, wazee wanazinguaga sana. Yalishanikuta
Wewe, huyo jamaa and the like .. ndiyo mnazingua.
Wazazi wametimiza wajibu wao wamekuzaa, kukulea na kukusomesha, umefikisha 25yrs bado unataka wakubebe?
Mbaya zaidi unawaongezea mzigo kuwapa mtoto wako wamlee wakati Sasa ni wakati wao wa kupumzikia na kula pesa zao.
 
Sometime hali ngumu vijana wanazitafutaga wenyewe.

Wala wasitafute huruma, wakomae na matatizo yao yaliyotokana na ujinga pamoja na uzembe wao.

Tena huyo mzee akaze kabisa hadi huyo jamaa atoke hapo.

Ningekuwa mimi ndio huyo mzee, Ningemfurumusha huyo jamaa.
 
Rafiki yako aliyataka hayo. Mtu kaja na hasira zake na anaondoka kwa haraka akiwa na hasira unamsimamisha unamuomba hela ya penseli ya mwanao kweli? Kichwani hayupo vizuri, umri miaka 28
Huyo mzazi wake ana busara sana. Alikubali kusimama na kumsikiliza huyo kijana mfedhuli na kumwambia hela ameiacha wapi. Kijana hana hata aibu kumkimbilia mzazi (at the age of 28yrs) kuomba hela kama mtoto wa chekechea.
 
Dah,Nampa pole mshkaji..Kuzaa na binamu na hata kumuoa sio tatizo kwa watu wengi tu,labda tamaduni za kabila la jamaa yako ndio makosa.
Kwangu Mimi hio sio laana.
Jamaa yako Angekuwa na misuli ya kipato Wala kusingekuwa na tatizo.
Mshauri aondoke nyumbani,akapambane.Akawe hata saidia fundi kwanza,akifanya kwa muda naye anaweza akawa fundi mzuri tu.
Unasema hakumaliza chuo,kwa maana hiyo Hana fani,atafute fani afanye kazi zake,alee mtoto wake.
Mambo ya kung'ang'ania kukaa home tu na huna kipato dharau lazima zitakuwepo tu.
Hata mbwa wenu wataanza kukubwekea!
Saidia fundi anakula 15k-18k per day,jamaa yako akiipata hii anaenda kupanga chumba mbande Cha 20k anafanya Maisha!
Mwambie aache uoga,atajiua Bure!
 
Kuhama ni sawa lakini nadhani angeenda kwa hatua kama ifuatavyo:
1. Amwombe sana msamaha mzazi/mlezi wake; ikibidi atafute hata mtu mzima wa kumsaidia. zingatia alifanya kosa kubwa sana kuzaa na binamu i.e. dada wa baba yake. It is a shame - unamwonesha baba yako kwamba ww bingwa unajua kuliwasha rungu??
2. Amwombe baba yake Mzazi mkopo ili akaanzie maisha mahali pengine - kupanga.
3. Asichague kazi. Kazi yoyote halali itakayomjia mbele yake yy afanye.
Situation ya kuwa bulled na kunyanyapaliwa na mzazi wengi tumepitia, na wakati mwingine Kwa kutuhumiwa vitu vya kusingiziwa, nakumbuka na mm nilisingiziwa kupitan na binamu yangu ambae tulikuwa karibu sana..Solution ni kunyanyuka na kwenda kusaka maisha mbali, hiyo misamaha wataombana baada ya muda hasira zikitulia na mhanga akiwa tayari ameshajitegemea kimaisha.
 
Unaendaje kusaka maisha hauna kianzio mjomba? Halafu huyo hakutuhumiwa bali alikiri mwenyewe hata akazaa na huyo binamu yake.
Ni kweli na ni sahihi utekelezaji ufanyike hasira zikitulia - Kwani hasira hasara
 
Kabisa mkuu akiondoka akaenda kujitafuta hata mzee hasira inapungua maana amuoni badae anakuja kuomba msamaha tu.
 
Vijana nao watuelewe wazazi wao....sio unaona tuna mood mbaya unaanza kituongelesha kwani kulikuwa na ulazima gani kuongea nae muda huo kama wewe tu mgeni ulihisi mzee kaingia kwa makasiriko,angemlia ganzi tu
 
Unaendaje kusaka maisha hauna kianzio mjomba? Halafu huyo hakutuhumiwa bali alikiri mwenyewe hata akazaa na huyo binamu yake.
Ni kweli na ni sahihi utekelezaji ufanyike hasira zikitulia - Kwani hasira hasara
Hapo mtaani akiona fundi ujenzi akaanze kuomba kazi ya saidia.
Atazoeleka na mafundi ataanza kupata pesa kidogo ya kuanzia maisha.
Aende hata kijiwe Cha madalali akaanze kazi ya udalali wa nyumba , magari, Viwanja na mashamba.
Tatizo vyeti vyetu vya shule wengi wanawapa aibu ya kufanya kazi flani.
 
Nilikuwa katika pitapita zangu za kawaida pale Ubungo Kibangu, lengo likiwa kumtembelea rafiki yangu wa zamani ambaye tulisoma naye sekondari. Ni kijana wa miaka 28, mcheshi na mwenye kipaji kikubwa katika mambo ya filamu. Hata hivyo, kwa sababu ambazo sikuwahi kujiuliza, hakufanikiwa kumaliza chuo kikuu, na maisha yake kwa sasa yamejikita nyumbani kwa wazazi wake.

Nilipofika kwake, tulikaa sebuleni tukibadilishana mawazo huku tukitazama runinga. Rafiki yangu alinitambulisha kwa mtoto wake mdogo, ambaye pia anaishi naye hapo nyumbani. Kwa muda, kila kitu kilionekana kuwa sawa—starehe ya kawaida ya marafiki waliokuwa wanapoteza muda pamoja. Lakini mambo yalibadilika ghafla baada ya kusikia honi ya gari ikilia getini.

Baba yake aliingia ndani kwa haraka. Hakuwa na muda wa kusalimiana nasi. Alitupita moja kwa moja bila hata tabasamu, hali iliyomfanya rafiki yangu kuonekana mwenye huzuni. Nilijaribu kuhamisha mawazo kwa kujadili muziki uliokuwa ukiimba kwenye runinga, lakini hali ya ukimya ilikuwa nzito.

Dakika chache baadaye, baba yake alirudi sebuleni akiwa tayari kuondoka. Rafiki yangu alijaribu kumfuata ili kuzungumza naye faragha, lakini kwa hasira baba yake alimkemea na kumtaka azungumze hapo hapo. Maneno yaliyofuata yalikuwa kama kisu kilichochanua majeraha ya ndani kwa rafiki yangu:
"Rafiki yako anajua kuwa nakulisha wewe na mwanao? Najua unataka hela ya madaftari, lakini tayari nimemwachia bibi yako."

Nilihisi aibu na huzuni kwa niaba ya rafiki yangu. Baba yake aliongea mambo mengi yasiyostahili mbele ya wageni, mambo ambayo hakika hayakuwa ya lazima. Niliona jinsi rafiki yangu alivyokuwa akijaribu kudhibiti hali, lakini baba yake hakumpa nafasi. Mwisho wa yote, baba yake aliondoka kwa hasira, na rafiki yangu alikaa kimya, akiwa ameinamisha kichwa huku mikono ikishika uso wake.

Niliamua kuondoka, lakini nilipokuwa napanga safari ya kurudi nyumbani, nilimsikia rafiki yangu akilia kimya kimya. Ilikuwa huzuni ya ndani, kilio cha mtu mzima aliyefika mwisho wa uvumilivu wake. Niliamua kumpeleka kwenye baa iliyo jirani, walau kunywa soda na kupunguza mawazo.

Tulipokuwa tukizungumza, alifunguka mambo mengi. Alinieleza kuwa mtoto wake ni matokeo ya uhusiano wake wa kifamilia na binamu yake, jambo ambalo linamletea changamoto nyingi. Pia alikiri kuwa alikuwa na tatizo la pombe ambalo linajirudia kila mara. Nilipomsikiliza, nilitambua kuwa mazingira aliyokuwa akiishi yalichangia kwa kiasi kikubwa hali yake. Baba yake alivyokuwa akimkandamiza kimaneno na kihisia, ni wazi kuwa alihisi kushindwa na maisha.

WALEZI NA WAZAZI, JIFUNZENI NAMNA YA KUDEAL NA VIJANA WENU

Sio kila mzazi anaelewa uzito wa maneno yake kwa watoto wake, hasa wale ambao bado wanahangaika kujipambania maishani. Kukatisha tamaa, kuwadhalilisha hadharani, au kuwaonyesha dharau kunaweza kuwa sababu kuu ya tabia zinazokufedhehesha. Walevi, watukutu, au wavivu mara nyingi wanakuwa hivyo kutokana na mzizi wa tatizo ambao unahusisha jinsi walivyolelewa.

Mara nyingi, tunahitaji huruma na ushirikiano zaidi na watoto wetu. Kama baba wa rafiki yangu angekuwa na uvumilivu na kujenga uhusiano wa karibu na kijana wake, pengine angempata rafiki badala ya mzigo. Tatizo si pombe tu, bali ni maisha yanayompelekea kijana huyo kushikilia pombe kama kimbilio lake pekee.

Siku hiyo, niliondoka nikiwa nimechanganyikiwa na huzuni. Mwanga uliokuwa machoni mwa rafiki yangu alipokuwa kijana umeshapotea. Sasa anaishi maisha yaliyojaa majuto, aibu, na matumaini yaliyoyeyuka. Wazazi, msisahau kuwa wakati mwingine unachohitaji kufanya kuokoa maisha ya kijana ni kumwelewa na kumpa nafasi ya kuzungumza. Mwisho wa siku, maisha ni mchanganyiko wa mapambano na msaada—hata kutoka kwa familia.
Vijana wajifunze kuchakarika na kujitafutia maisha.
Unyoronyoro wa kuogopa kupambana na maisha , unadharulika na hata wazazi wako.
 
Back
Top Bottom