Kwa mara ya kwanza nimeona mwanaume analia kwa sababu isiyohusisha msiba wala mapenzi

Kwa mara ya kwanza nimeona mwanaume analia kwa sababu isiyohusisha msiba wala mapenzi

Nimehuzunika..
Sijui ni kwasababu na mimi nina yangu yanayonisibu au??.

Ila mwambie mshkaji wao aondoke hapo home. Sema sasa kama ana shida ya pombe hapo ndio hatar inapokuja atakufa huko mtaani.
Kwel mshua wake hayuko fair ila pia asilaumiwe, huwa inauma kama.mzaz unapojitahid kutimiza majukumu yako kimalezi na mahitaji kwa watoto halaf wanakuja kuzingua, kama mzaZ pia anajeruhiwa sana maana tukubali tukatae, wazaz pia huwa na expectations kwa watoto wao, unapiga hesab ulivyomhangaikia il badae ajimudu ila matokeo yake anakua tegemezi inauma kiukwel.

Ila mshauri jamaa ajaribu kujiongeza, asiogope maisha, akafanye hata vibarua vya kupata hela ya daftar. Mtu mzima kununuliwa mpaka daftar za mtoto pia haiko sawa sana..akapige hata vijikaz vidogo vidogo angalau wazaz nao wafurah.
Hakuna furaha anayopata mzaz kama anapoona mwanae anapambana na maisha yale kivyake.

Polen sana.

NB
Kulia muhimu, kunaondoa uchungu na kikuepusha na sonona
 
Alinieleza kuwa mtoto wake ni matokeo ya uhusiano wake wa kifamilia na binamu yake, jambo ambalo linamletea changamoto nyingi. Pia alikiri kuwa alikuwa na tatizo la pombe ambalo linajirudia kila mara. Nilipomsikiliza, nilitambua kuwa mazingira aliyokuwa akiishi yalichangia kwa kiasi kikubwa hali yake. Baba yake alivyokuwa akimkandamiza kimaneno na kihisia, ni wazi kuwa alihisi kushindwa na maisha.
Mwambie huyo rafiki yake awe mwanaume aache kuwa mvulana atoke hapo nyumbani kwa baba yake akaishi mbali na mkewe ( binamu) na mtoto wake hiyo ndiyo bond yake . Pia mwambie maji yakisha mwagika hayazoleki na yakizoleka yana kua machafu na pungufu kikubwa akubaliane na matokeo ya upendo wao.

Mwambie huyo binamu yake ndiyo awe mke wake na ampende kwa dhati huko ughaibuni wawapo ila asiwachukie wazazi wake ( ila aongee nae kwa kina wakubaliane kuishi mume na mke) , pia mwambie huyo mtoto ndiye ndugu yake na ndugu zake wengine ni wadogo zake na mtoto wake atakao endelea kuzaa na binamu yake).. Mwambie asiamini kabisa kama binamu yake ni ndugu yake ajizime data haswa apambane na maisha hukumu ya mwanadamu ipo kwa Mungu amwombe Mungu toba na aamini amesamehewa alafu yeye asubirie siku ya kifo chake atahukumiwa au itakuaje..

NB. HUKO AENDAKO ASIWAAMBIE WATU KAMA MKEWE NI BINAMU YAKE NA MKEWE HIVYO HIVYO, PIA HATA WAZAZI NA NDUGU WAKIWALAANI YEYE AAMINI HALAANIKI IPO SIKU WATAMKUMBUKA
 
Mkuu,
Samahani Asante kwa ku share nasi touching story..

Soda haipunguzi mawazo 😊

Hayo masimango ayatumie kama catalyst siku moja aje kua mtu mbele za watu..

Naogopa Kuna njia naombaga nisizipite kabisa kabisa/ nisinge kua nafanya hiki nacho kifanya ningekua wapi now..
 
Nieleweshe,wewe na huyo rafikio ni wanawake au wanaume?
Alizalishwa au alimzalisha binamu?

Ila kama jamaa yako ni jobless, lazima uwa anapita humu JF,atajua ulivomsema.
 
Tena huyo ni wakupiga na makofi kijana wa 23+ unakaaje nyumbani unasubiri chakula cha wazee?
Tena huyo dingi ni mstaarabu sana.
 
Hapo mtaani akiona fundi ujenzi akaanze kuomba kazi ya saidia.
Atazoeleka na mafundi ataanza kupata pesa kidogo ya kuanzia maisha.
Aende hata kijiwe Cha madalali akaanze kazi ya udalali wa nyumba , magari, Viwanja na mashamba.
Tatizo vyeti vyetu vya shule wengi wanawapa aibu ya kufanya kazi flani.
Mkuu kuna vijana ni wazembe sana,nakumbuka mie ile nimemaliza form 6 nilizunguka viwanda vilivyoko Ilala na Temeke kupiga day worker hapo nipo na 20 yrs.Chuo mwaka wa kwanza nikawa nasoma na kufanya bishara ya kuuza dagaa.Namaliza nina 23 yrs nikajikita kwenye biashara ya dagaa na kupanga chumba.
 
Back
Top Bottom