Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wamama wa hivi ndio wanafuga vibaka, panya road na majambazi. Hongera mshua wako kukukazia huenda ungekuwa kipanya road kikuu sasa hiviHawa wazazi ukifanikiwa ndio wanakupenda
Wazazi wachache sana hasa wakina mama ndio wanampenda mtoto ata akiwa situation gani, wazee wanazinguaga sana. Yalishanikuta
Kina mama ndio wanaoharibu vijana wao kwa kuwatetea na kuwafichia Siri, Tena baba akisema mama anapanda juu ya meza kumtetea mtoto mavuno ndio hayo, miaka 28 nyumbani anatafuta nini?Hawa wazazi ukifanikiwa ndio wanakupenda
Wazazi wachache sana hasa wakina mama ndio wanampenda mtoto ata akiwa situation gani, wazee wanazinguaga sana. Yalishanikuta
Anapanda juu ya meza😃😃Kina mama ndio wanaoharibu vijana wao kwa kuwatetea na kuwafichia Siri, Tena baba akisema mama anapanda juu ya meza kumtetea mtoto mavuno ndio hayo, miaka 28 nyumbani anatafuta nini?
In chimakeke voice.Atoke magetoni
unataka ukasagane na mariposa ee?pm kwake unaenda kufanya nini?Kuna namna umeandika kiutu uzima🤔,
Wewe, huyo jamaa and the like .. ndiyo mnazingua.Hawa wazazi ukifanikiwa ndio wanakupenda
Wazazi wachache sana hasa wakina mama ndio wanampenda mtoto ata akiwa situation gani, wazee wanazinguaga sana. Yalishanikuta
Huyo mzazi wake ana busara sana. Alikubali kusimama na kumsikiliza huyo kijana mfedhuli na kumwambia hela ameiacha wapi. Kijana hana hata aibu kumkimbilia mzazi (at the age of 28yrs) kuomba hela kama mtoto wa chekechea.Rafiki yako aliyataka hayo. Mtu kaja na hasira zake na anaondoka kwa haraka akiwa na hasira unamsimamisha unamuomba hela ya penseli ya mwanao kweli? Kichwani hayupo vizuri, umri miaka 28
Situation ya kuwa bulled na kunyanyapaliwa na mzazi wengi tumepitia, na wakati mwingine Kwa kutuhumiwa vitu vya kusingiziwa, nakumbuka na mm nilisingiziwa kupitan na binamu yangu ambae tulikuwa karibu sana..Solution ni kunyanyuka na kwenda kusaka maisha mbali, hiyo misamaha wataombana baada ya muda hasira zikitulia na mhanga akiwa tayari ameshajitegemea kimaisha.Kuhama ni sawa lakini nadhani angeenda kwa hatua kama ifuatavyo:
1. Amwombe sana msamaha mzazi/mlezi wake; ikibidi atafute hata mtu mzima wa kumsaidia. zingatia alifanya kosa kubwa sana kuzaa na binamu i.e. dada wa baba yake. It is a shame - unamwonesha baba yako kwamba ww bingwa unajua kuliwasha rungu??
2. Amwombe baba yake Mzazi mkopo ili akaanzie maisha mahali pengine - kupanga.
3. Asichague kazi. Kazi yoyote halali itakayomjia mbele yake yy afanye.
Unaendaje kusaka maisha hauna kianzio mjomba? Halafu huyo hakutuhumiwa bali alikiri mwenyewe hata akazaa na huyo binamu yake.Situation ya kuwa bulled na kunyanyapaliwa na mzazi wengi tumepitia, na wakati mwingine Kwa kutuhumiwa vitu vya kusingiziwa, nakumbuka na mm nilisingiziwa kupitan na binamu yangu ambae tulikuwa karibu sana..Solution ni kunyanyuka na kwenda kusaka maisha mbali, hiyo misamaha wataombana baada ya muda hasira zikitulia na mhanga akiwa tayari ameshajitegemea kimaisha.
Kabisa mkuu akiondoka akaenda kujitafuta hata mzee hasira inapungua maana amuoni badae anakuja kuomba msamaha tu.Situation ya kuwa bulled na kunyanyapaliwa na mzazi wengi tumepitia, na wakati mwingine Kwa kutuhumiwa vitu vya kusingiziwa, nakumbuka na mm nilisingiziwa kupitan na binamu yangu ambae tulikuwa karibu sana..Solution ni kunyanyuka na kwenda kusaka maisha mbali, hiyo misamaha wataombana baada ya muda hasira zikitulia na mhanga akiwa tayari ameshajitegemea kimaisha.
Hapo mtaani akiona fundi ujenzi akaanze kuomba kazi ya saidia.Unaendaje kusaka maisha hauna kianzio mjomba? Halafu huyo hakutuhumiwa bali alikiri mwenyewe hata akazaa na huyo binamu yake.
Ni kweli na ni sahihi utekelezaji ufanyike hasira zikitulia - Kwani hasira hasara
Sikuwa nimeona aisee Dr. Mariposaunataka ukasagane na mariposa ee?pm kwake unaenda kufanya nini?
wakati huyo nimsagaji na analea mashoga
Vijana wajifunze kuchakarika na kujitafutia maisha.Nilikuwa katika pitapita zangu za kawaida pale Ubungo Kibangu, lengo likiwa kumtembelea rafiki yangu wa zamani ambaye tulisoma naye sekondari. Ni kijana wa miaka 28, mcheshi na mwenye kipaji kikubwa katika mambo ya filamu. Hata hivyo, kwa sababu ambazo sikuwahi kujiuliza, hakufanikiwa kumaliza chuo kikuu, na maisha yake kwa sasa yamejikita nyumbani kwa wazazi wake.
Nilipofika kwake, tulikaa sebuleni tukibadilishana mawazo huku tukitazama runinga. Rafiki yangu alinitambulisha kwa mtoto wake mdogo, ambaye pia anaishi naye hapo nyumbani. Kwa muda, kila kitu kilionekana kuwa sawa—starehe ya kawaida ya marafiki waliokuwa wanapoteza muda pamoja. Lakini mambo yalibadilika ghafla baada ya kusikia honi ya gari ikilia getini.
Baba yake aliingia ndani kwa haraka. Hakuwa na muda wa kusalimiana nasi. Alitupita moja kwa moja bila hata tabasamu, hali iliyomfanya rafiki yangu kuonekana mwenye huzuni. Nilijaribu kuhamisha mawazo kwa kujadili muziki uliokuwa ukiimba kwenye runinga, lakini hali ya ukimya ilikuwa nzito.
Dakika chache baadaye, baba yake alirudi sebuleni akiwa tayari kuondoka. Rafiki yangu alijaribu kumfuata ili kuzungumza naye faragha, lakini kwa hasira baba yake alimkemea na kumtaka azungumze hapo hapo. Maneno yaliyofuata yalikuwa kama kisu kilichochanua majeraha ya ndani kwa rafiki yangu:
"Rafiki yako anajua kuwa nakulisha wewe na mwanao? Najua unataka hela ya madaftari, lakini tayari nimemwachia bibi yako."
Nilihisi aibu na huzuni kwa niaba ya rafiki yangu. Baba yake aliongea mambo mengi yasiyostahili mbele ya wageni, mambo ambayo hakika hayakuwa ya lazima. Niliona jinsi rafiki yangu alivyokuwa akijaribu kudhibiti hali, lakini baba yake hakumpa nafasi. Mwisho wa yote, baba yake aliondoka kwa hasira, na rafiki yangu alikaa kimya, akiwa ameinamisha kichwa huku mikono ikishika uso wake.
Niliamua kuondoka, lakini nilipokuwa napanga safari ya kurudi nyumbani, nilimsikia rafiki yangu akilia kimya kimya. Ilikuwa huzuni ya ndani, kilio cha mtu mzima aliyefika mwisho wa uvumilivu wake. Niliamua kumpeleka kwenye baa iliyo jirani, walau kunywa soda na kupunguza mawazo.
Tulipokuwa tukizungumza, alifunguka mambo mengi. Alinieleza kuwa mtoto wake ni matokeo ya uhusiano wake wa kifamilia na binamu yake, jambo ambalo linamletea changamoto nyingi. Pia alikiri kuwa alikuwa na tatizo la pombe ambalo linajirudia kila mara. Nilipomsikiliza, nilitambua kuwa mazingira aliyokuwa akiishi yalichangia kwa kiasi kikubwa hali yake. Baba yake alivyokuwa akimkandamiza kimaneno na kihisia, ni wazi kuwa alihisi kushindwa na maisha.
WALEZI NA WAZAZI, JIFUNZENI NAMNA YA KUDEAL NA VIJANA WENU
Sio kila mzazi anaelewa uzito wa maneno yake kwa watoto wake, hasa wale ambao bado wanahangaika kujipambania maishani. Kukatisha tamaa, kuwadhalilisha hadharani, au kuwaonyesha dharau kunaweza kuwa sababu kuu ya tabia zinazokufedhehesha. Walevi, watukutu, au wavivu mara nyingi wanakuwa hivyo kutokana na mzizi wa tatizo ambao unahusisha jinsi walivyolelewa.
Mara nyingi, tunahitaji huruma na ushirikiano zaidi na watoto wetu. Kama baba wa rafiki yangu angekuwa na uvumilivu na kujenga uhusiano wa karibu na kijana wake, pengine angempata rafiki badala ya mzigo. Tatizo si pombe tu, bali ni maisha yanayompelekea kijana huyo kushikilia pombe kama kimbilio lake pekee.
Siku hiyo, niliondoka nikiwa nimechanganyikiwa na huzuni. Mwanga uliokuwa machoni mwa rafiki yangu alipokuwa kijana umeshapotea. Sasa anaishi maisha yaliyojaa majuto, aibu, na matumaini yaliyoyeyuka. Wazazi, msisahau kuwa wakati mwingine unachohitaji kufanya kuokoa maisha ya kijana ni kumwelewa na kumpa nafasi ya kuzungumza. Mwisho wa siku, maisha ni mchanganyiko wa mapambano na msaada—hata kutoka kwa familia.