Kwa Mara ya Kwanza nimeroga mtu

Kwa Mara ya Kwanza nimeroga mtu

Vyovyote vile nafsi yangu inaamani
Ukute hata huo mkono kuuma haihusiani na wewe kumroga. Pengine hata usingeenda kwa mganga huo mkono ungemsumbua tu ila kwa sababu umesharoga unahisi ni majibu.
 
Shida moja ya kuroga ni vita isiyoisha nae ana ndugu watahangaika mpaka watakujua na wewe utarushiwa kombora mdomo uende upande .
MaMbo ya mdomo yamenifanya niandike hii,
Kuna Jirani KaLaLa night kasikia anaitwa sauti ya mtu anaemfahamu kutoka nje aoni mtu...
Ile kurudi ndani apige miayo mdomo ukaganda mpaka asubuh Huku uvimbe ukiwa umejaa shingoni..
Haya maisha SI poa ase
 
Safi Sana uchawi ni silaha yetu wanyonge!! Mm Kuna mmoja namsubiri yupo china!! Nimeshapata mganga wakuuwa !! Tatizo mganga anauwa watu watu tuu Kwa mwaka!! Sasa mwaka Jana alishauwa watatu.
Mwaka huu 2024 niliwahi Kwa mganga January jamaa nimesha msajili!!
Dawa ya mtu mshenzi unakuwa mshenzi mara mbili yake!! Namuondoa tuu
 
Bado hasira imekujaa moyon ndio maana hujutii ila ni suala la muda tu utamuonea huruma sanaa, binadamu wa kawaida yuko hivyo. Hata yeye alivyokupiga baada ya ajali endapo ungeamua kumuacha na kumshtakia Mungu ingefika hatua tu ange feel guilt na kujutia sana hata kama asingerud kuomba msamaha..Binadamu asiye na darkness inside their hearts hu feel this way mara zote.

Anyway , mimi siwez kukulaumu wala kukiinga mkono maana hata mimi sijui ningefanya nini but binafsi naamin katika kisas cha mwenyez Mungu na muda kama hakimu wa haki.

Iliyo yangu ni yangu na nitaipata tu regardless of the circumstances.
 
Kwa Mara ya Kwanza nimeroga mtu!

Sikuwahi kufikiria Kama kunasiku nitakuja kufanya uchawi, ila wiki ya Kwanza ndani ya mwaka mpya nimefanya. Nimemroga mtu na amerogeka. Na katika Hilo Wala sijutiii. Maana huyu jamaaa alinikera Sana.

Ugomvi wetu ulikuwa hivi, Mimi Baada ya kupigika Sana na maisha niliamua kujikita kwenye bodaboda Kama kazi yangu rasmi. Kwakuwa elimu yangu Ni kubwa na darasani wakati nasoma nilikuwa kipanga uamuzi huu umenifanya ninyoshewe vidole Sana. Wengi hasa wale niliosoma nao ambao wamenizidi kipato wamekuwa wananikebehi Sana. Nimekuwa nikiumia moyoni lakini Sina jinsi zaidi ya kupuuzia.

Sasa tarehe 24 mwezi wa 12,nikiwa kwenye heka heka zangu na boda boda,kuna gari ilinisukuma nikaanguka pembeni ya barabara. Nikiwa chini nimeumia na boda boda baadhi ya vitu vimevunjika mwenye ile gari alishuka na kuanza kunitukana.

Kilichonikera huyu jamaaa nimesoma nae, na form two ni Mimi ndie niliyemsaidia akafaulu, maana tulimkuta karudia darasa.Huyu jamaa Ni mwanajeshi lakini toka aingie jeshi amekuwa na tabia za unyanyasaji Sana. Mtaani anaskendo kibao za kupiga watu.

Basi bana bila ya kujali Mimi Ni classmate wake, pia bila kujali kuwa ni yeye ndie aliyenisukuma na gari yake alinishushia matusi ya nguoni na kunipiga vibao . Nilijitutumua nirudishie lakini boda boda wenzangu walinisihi nimwache. Waliniambia nikijibu mapigo ataenda kuota askari wenzake na watakuja kupiga kijiwe kizima.

Kwa Hali hio sikuwa na chakufanya. Nilivumilia matusi yote na kipigo juu. Alipoondoka nami kinyonge nilirudi nyumbani. Kwa Siku tano nilikaa ndani pasipokutoka nje, kila nilipofikiria lililotokea nilikosa nguvu. Kiukweli Niliumia Sana.

Nikiwa kwenye Hali hio jamaa yangu mmoja alifika na kunipa wazo la kulipa kisasi. Alinitaka twende kwa mganga, mwanzo nilikataa lakini Baada ya kufikiria Sana niliamua kwenda. Nilimweleza mganga Nia yangu ya kulipa kisasi akaniambia nimpelekee picha ya jamaa, mawe ya makobo na mavi ya mbuzi.

Chap ndani ya Siku mbili nilivipata hivyo vitu nikapeleka.Mganga aliniuliza nataka kisasi Cha aina gani nikamwambia chochote atakachokiona yeye kinafaaa.Aliniitaka niondoke na kuniahidi ndani ya wiki kadhaa nitapata majibu.

Leo nipo kijiweni nimepewa taarifa jamaa anawiki Moja mkono wake kulia ambao aliutumia kunipiga haufanyi kazi. Taarifa hiii imekuwa njema Sana kwangu. Kesho nimeoaga kwenda kwa mganga kumuongezea hela ila ahakikishe mkono ule usifanye kazi milele.

Sijutiii


Mmesoma shule moja, mtaani mpo pamoja, akupige n mkofi, acha uongo basi?
 
................ila kuna mwamba anafirst class ya mzumbe ni bodaboda tabata so inawezekana pia, mzumbe walimbakisha akakataa akidhani huku nje atatoboa kirahisi na makaratasi yake,alipojaribu kurudi mzumbe wakamwambia imeisha huyo
 
Back
Top Bottom