maishapopote
JF-Expert Member
- May 28, 2009
- 3,408
- 6,094
mleta mada mmbeya
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii siredi nayo unalipwa.Nimeshuhudia jana mbuzi anachinjwa huku amezibwa mdomo ili asilie.
Kwa ushinjaji huu hamu ya nyama ya mbuzi imeniishia kabisa bora kesho nirudi Dar.
Happy New Year!
Ndio bwashee!Hii siredi nayo unalipwa.
Sawa bwashemej piga kazi wapwa zangu waende chooni.Ndio bwashee!
CCM fursa kibao siyo hapo Ufipa hata kina Halima Mdee mnawabania wasiende kula posho bungeni!Sawa bwashemej piga kazi wapwa zangu waende chooni.
Hili lipo wazi mnyama akishagegedwa mimba lazimaNg'ombe hafai kwa mila mkuu hua ni mbuzi tu na wakati mwingine huwa ni mbuzi maalumu mfano kuna mila inataka mbuzi jike ambae hajazaa wala kugegedwa.
Mbona nimehudhuria shughuli kibao huko migombani na Ng`ombe walichinjwa? Au sio wa mila wale?Mkuu uchagani n'gombe hafai kwa mila
Mkuu hebu kaulize wazee wako watakwambia pia Ng`ombe ana namna yake ya kuchinjwa na kufanyiwa mila...Ng'ombe hafai kwa mila mkuu hua ni mbuzi tu na wakati mwingine huwa ni mbuzi maalumu mfano kuna mila inataka mbuzi jike ambae hajazaa wala kugegedwa.
Akishachinjwa mbuzi wa mila, n'ngombe huchinjwa kuongeaza kitoweo kwa wageni mkuu! Na tena ni kwa wale wenye uwezoMbona nimehudhuria shughuli kibao huko migombani na Ng`ombe walichinjwa? Au sio wa mila wale?
Wachaga wengi ni washirikina Sana , wengi wanatumia dumba kwenye biashara zao, wanafuga sana misukule kwenye nyumba zao za biashara, Cha kushangaza siku ya jumapili utawakuta wamebeba Bible na kuwahi kanisani utafikiri kweli ni waumini wa kweli kumbe wengi ni vigagula.
Mila zinatofautiana bhas mkuu, kuna wanachinja Ng`ombe, wengine Mbuzi na wengine Kondoo. Zote wanafanyia mila na pia zote ni mboga vile vile,Akishachinjwa mbuzi wa mila, n'ngombe huchinjwa kuongeaza kitoweo kwa wageni mkuu! Na tena ni kwa wale wenye uwezo
Ww umeona mbuzi akichinjwa ????Nimeshuhudia jana mbuzi anachinjwa huku amezibwa mdomo ili asilie.
Kwa ushinjaji huu hamu ya nyama ya mbuzi imeniishia kabisa bora kesho nirudi Dar.
Happy New Year!
1. HAKUNA NG'OMBE ANACHINJWA KWA MILA, MNYAMA WA MILA NI MBUZI TU, ILA KUNA WAKATI KONDOO NAE HUWA ANAHITAJIKA KUTEGEMEA NA AINA YA MILA.Mbona nimehudhuria shughuli kibao huko migombani na Ng`ombe walichinjwa? Au sio wa mila wale?
Mtoa mada inaonekana ni mgen uchinjaji huu kwa sie wachaga ulipotea sana kwasababu ukiona Mbuzi anachinja ujue kuna jambo la kimila linafanyika ndo wanamzibaga mbuzi mdomo kwakutumia lile jan la isale hizi mila zilipotea kwasababu makanisa mengi yalianza kupiga marufuku waumin wao kufanya matendo haya pili hizi mila zina mipaka yake ukikosea inakurudia wewe na familia yako sasa wale wazee wengi wa kimila hawapo Tena na vijana wengi hatujui mila so kila mtu anaogopa kabisa Ku practiseMkuu iyo ni moja ya mila na ina maana yake, anazibwa mdomo alaf anachomwa kisu kufuani hadi kinagusa moyo, siwezi kuelezea zaidi maana wahusuka wanalifahamu hilo.
Mleu umemaliza kila kitu sina lakuongeza1. HAKUNA NG'OMBE ANACHINJWA KWA MILA, MNYAMA WA MILA NI MBUZI TU, ILA KUNA WAKATI KONDOO NAE HUWA ANAHITAJIKA KUTEGEMEA NA AINA YA MILA.
2. MBUZI HULAZWA CHINI ANASHIKWA MIGUU NA WATU KILA UPANDE MTU MMOJA MKAKAMAVU (ANAYEJUA MILA KWELIKWELI) HUMZIBA MDOMO KWA NGUVU ASITOE PUMZI WALA SAUTI MPAKA ANAKATA ROHO. BAADA YA KUKATA ROHO NDIO HUKATWA KOROMEO.IKATOKEA AKATOA PUMZI AU SAUTI MILA IMEHARIBIKA INABIDI MHUSIKA AKALETE MBUZI MWINGINE.
3. BAADA YA KUCHINJA VIUNGO VYA NDANI (MAINI, MAPAFU, UTUMBO) HUSOMWA KUANGALIA KAMA KWENYE UKOO KUNA SHIDA YOYOTE, KUNA MAENEO YAKIONEKANA HYAKO SAWA WAHUSIKA HUITWA NA KUONYWA.
4. BAADA YA KUCHINJWA DAMU MBICHI HUCHANGAYWA NA SUPU YA MOTO NA KUNYWEWA NA WANAUME(WANAWAKE HAWARUHUSIWI KATIKA MATUKIO YOTE HAYA WAO HUKAA JIKONI WAKISUBIRI MGAO WAO NAO WAPIKE/WALE)
5. MILA NYINGI NI ZA KUOMBA BARAKA KWA WAZEE WALIOTANGULIA, KWA HIYO FINYANGO HUKATWA KWENYE KILA KIUNGO NA KUWEKWA KWENYE JANI BICHI LA MGOMBA (IDADI YA MAJANI HUTEGEMEA NA WATU GANI WANAOMBWA KUNA WA MABABU, MABIBI, MASHANGAZI etc) BAADAE HUPELEKWA SHAMBANI CHINI YA MGOMBA/MKAHAWA NA KUACHWA HAPO WAZI. KESHO YAKE ASUBUHI MNAANDAMANA KWENDA KUANGALIA KAMA ZILE FINYANGO ZIPO AU ZIMEONDOKA, KAMA ZIPO MILA IMEKATALIWA NA ITABIDI MRUDIE KAMA HAZIPO WAZEE WALIZICHUKUA.
6. HAPA NDIO UTAONA MAAJABU NA KAMA HUAMINI HIZI MILA ITABIDI UKIFIKIRIE MARA MBILI MBILI, KUNA WAKATI MNAKUTA FINYANGO ZOOTE KWENYE KILA JANI ZIPO KAMA MLIVYOZIWEKA JANA JIONI NA KULIKUWA KUNA MBWA WENGI TU WANAZENGEA WAKATI MNACHINJA NA MNAPOENDA KUWEKA CHINI YA MKAHAWA NI KARIBU TU NA HAPO KWENYE MBWA WENYE UCHU WA NYAMA. KWA NINI HAWAKULA PALE??
Kuna mbuzi wanatangulia huchinjwa pia wakati huo huo pamoja na ng'ombe na si kwamba ng'ombe hawafai kwa mila , Ng'ombe wa mila wanamuwekea vile vitoto vya migomba puani wakati anachinjwa.Mbona nimehudhuria shughuli kibao huko migombani na Ng`ombe walichinjwa? Au sio wa mila wale?
Kuna mbuzi wanatangulia huchinjwa pia wakati huo huo pamoja na ng'ombe na si kwamba ng'ombe hawafai kwa mila , Ng'ombe wa mila wanamuwekea vile vitoto vya migomba puani wakati anachinjwa.
Njoo ngorongoro uone ninavyochinja mbuzi,kondoo na ng'ombeHapa ndo umejidhihirisha kuwa wewe ni mwanaume mwoga...
Mwanaume gani unaogopa kuona mbuzi anachinjwa????
Nimestajaabu mnoo....