Kwa maslahi mapana ya TAIFA uchaguzi haupaswi kuwa HURU

Ni mjadala mzuri huu.
Unajuwa, Tanzania kama nchi haina tofauti kubwa na kitu kama jukwaa hili la JF; ambalo Machizi nao wanazo nafasi zao za kujitanua kichizi chizi kama ilivyo hapa na huyu mkuu 'Uwesu'; (sijui jin ndio hilo au nimekosea; maana nami bangi zimepanda hadi utosini)
 
Tatizo elimu yangu ni ndogo
Siyo elimu tu, hata akili nazo huna.

Kwa hiyo kwako wewe, taifa ni Ccm na viongozi wake ?!. Kuna watu nje ya Ccm ni wazalendo kuliko hawa waliogawa rasilimali zetu zote. Ccm hawa ni mafisadi siyo wazalendo.
 
Mimi ni paka kama wewe tu, ambaye unashadadia vitu usivyo vijua Mazala yake kwako taifa na vizazi vyako, tena wewe ndio paka shume kabisa
Ona kenge isiyojua hata kuandika hii, "MAZALA" ndio nini?
 
Siyo elimu tu, hata akili nazo huna.

Kwa hiyo kwako wewe, taifa ni Ccm na viongozi wake ?!. Kuna watu nje ya Ccm ni wazalendo kuliko hawa waliogawa rasilimali zetu zote. Ccm hawa ni mafisadi siyo wazalendo.
Tusio na akili tupo wengi ukiwemo na wewe mwenyewe. Nikwambie tu punguani mwenzangu kuongoza nchi sio kitu rahisi, hata tukimpa uraisi baba yako hawataweza furahi watu wate
 
Enheee. Nchi yetu imejaa machizi wengi sana mitaani, hivyo tukiruhusu mawazo yenu ya kichizi yachague rahisi tutakuja kupata maraisi machizi pia, ifikie siku moja uchaguzi mkuu uwe wa wenyeviti wa vijiji tu.
 
Hivi kwa akili yako wakati Kikwete anampendekeza Dr. Bilali kuwa Mgombea mwenza wake 2010 ,ulielewa sababu za uteuzi ule.
Ni kwamba yule alikuwa kikwazo haswa Zanzibar wakati wa kumteua Dr. Shein na ili kumziba mdomo akapewa huo umakamu. Naona ni kama walivyofanya Kwa Dr Nchimbi ambaye inajulikana haivi na Mzee Kikwete na misimamo yake CCM wanaihofia kwa hiyo wakaona dawa mpe umakamu atakaa kimya, zaidi ni kutembea na mkasi wa kukata utepe ya uzinduzi.
Sasa alivyomfanyia Kikwete kumuondoa Dr Bilali kwenye siasa za Zanzibar aliwahi kufikiri kama yangetokea kama 17/03/2021 Kwa Hayati JPM?
Ingetokea wakati wa huo,Dr waliyemkataa Zanzibar angekuwa President wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri jeshi mkuu!!
Kwa hiyo hata mama Samia waliomuweka hawakuwahi kufikiri ingetokea akawa Rais,ndio sababu yalipita masaa 60 hajaapishwa.
Na hii siyo hapa tu,hata huko Kenya Mzee Kenyatta alimuondoa makamu wake Mzee Kibaki wakati kama nakumbuka vizuri,akamteua Mzee Moi,na wakati wakikuyu ambao kiuhalisia walishiriki sana kuikomboa Kenya kupitia jeshi lao la Mau Mau,hivyo waliamini Rais wa Kenya lazima awe mkikuyu,lakini Mzee akakata moto usiku ghafla na Makamu yupo mkalenjini Mzee Moi. Na Moi alitumia mbinu za kimafia kuhakikisha yeye anakuwa Rais.
Kwa hiyo kuwa na tume huru kuna umuhimu wake na ulazima,kama tunataka kwenda mbele.
Tume huru ni kuwapa wananchi uwezo na mamlaka juu ya mstakhabari wa nchi yao. Maana yake siyo lazima Chadema ndio ishinde No hata CCM ikishinda ishinde kwa haki. Leo kuna derby kati Simba na Yanga, hizi timu ziko makini sana Na waamuzi haswa muamuzi wa Kati, kwa nini? Maana yake anayeshinda ashinde kwa haki.
Leo utashangaa viongozi wakubwa wa nchi wanajiondoa ufahamu eti tuilinde amani yetu,na ni amani ipi isiyoambatana na haki. Mbona Neno HAKI wanaliogopa sana hata kulitamka tu!!
Na siku zote weka kichwani mwako Haki huinua Taifa bali dhambi ni aibu ya watu wote.
Rafiki mkubwa wa Amani ni Haki Na kweli. Amani akiwakosa hao marafiki zake wawili mtamlazisha akae lakini atakuwa bandia.
Hivi nimewahi kusoma historia kuhusu aliyemuua Mzee Karume, aliitwa Luteni Humid,na huyu inasemekana baba yake aliuawa na utawala wa Mzee Karume,japo Mzee Karume hyu Humid alimsomesha mpaka Urusi, lakini hiyo haikuondoa roho ya kisasi cha baba yake. Hata waliopanga mpango huo walimtumia yeye walijua yupo tayari na anayo sababu.
Nchi ilindwe Kwa kutenda haki na amani itakuwepo automatically.
Haki ipatikane kwenye chaguzi zetu, mahakamani na zaidi polisi.
 
Wee jamaa kunywa soda nakuja kulipa.
 
Kama ni hivyo kwa nini basi uitishwe Uchaguzi unaosimamia general election na kupoteza hela za walipa Kodi?
Kwa nini watoke kwenye chama kimoja?
 
Duuuh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…