Kwa maslahi mapana ya taifa, Zitto ungana na Tundu Lissu tuchukue nchi

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Najua kuna watu wapo kazini kuhakikisha Membe anagombea urais kupitia ACT lakini siyo kwa maslahi ya taifa bali ni kwa maslahi ya CCM.

Nashauri ZittoTundu Lissu wapitie bandiko ili wafanye kitu kwa maslahi mapana ya upinzani kwa ujumla,nawahakikishia mtashinda.

Membe hawezi kushinda urais hata siku moja maana hatakuwa na back-up ya nguvu ya umma kama itakavyokuwa kwenu.

Najua kuna vijana wa Makumbusho wanakufata wakikwambia umchukue Membe ila nakuhakikishia wanakuingiza mtegoni kama ilivyokuwa kwa Lowassa na chadema. Lissu na wewe ndio mna % kubwa ya kushinda urais mwaka huu. Kubali uwe waziri mkuu, Lissu awe Rais.

Nyaraka zinawabeba otherwise msije kuwalaumu Watanzania.
 
Lissu na Zitto yupi ni Mzanzibari kati yao?
 
Hawawezi kugombea pamoja kwa katiba hii ya sasa. Mmoja anapaswa kuwa mzanzibar.
 
Na 'back-up ya nguvu ya umma' unamaanisha ww mwenyewe ndio umma! Kuna watu mnaota ndoto za mchana eeh! Wasaliti hao wa nchi yetu na makuadi wa mabeberu na mashoga wapewe nchi gani? Au unamaanisha kipande cha ardhi cha ekari moja cha kulima huko kijijini kwenu eeh!?
 
Wewe ni shida au niseme ni zaidi ya mbumbumbu wa Katiba ya TZ. Ni wakukuignore tu!
 
 

..Katiba hairuhusu hicho ulichopendekeza.

..Raisi na Makamu wanatakiwa watoke pande tofauti za muungano.

..Raisi akitoka Tanganyika / Tz bara Makamu anatakiwa atoke Zanzibar. And vice versa.

..Zitto na Juma Duni wanaweza kugombea kama Raisi na Makamu.

..Tundu Lissu na Juma Duni pia wanaweza kugombea.

NB.

..Waziri Mkuu atatokana na chama chenye wabunge wengi.

..Waziri Mkuu pia anaweza kuwa ni mbunge anayeungwa mkono na wabunge wengi. Nadhani framers waliangalia mazingira ambapo hakuna chama chenye clear majority bungeni.

..Spika anaweza kuchaguliwa miongoni mwa wabunge, au anaweza kutoka nje ya bunge ilimradi apigiwe kura na wabunge wengi.
 
Labda nchi ya kusadikika

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo kweli mkuu, hivi unajua kwamba, Zito anaweza kuleweka mapema zaidi ya Membe?

Membe ni garasa mkuu, akiwekwa Membe Ngoma itakuwa ni ya Asubuhi na mapema CCM wakaibuka washindi!!
 
Kama lisu atagombea urais kwa katiba yetu ilivyo zitto hawezi kuwa mwakamu wa rais labda kuwa waziri mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…