Kwa maslahi mapana ya taifa, Zitto ungana na Tundu Lissu tuchukue nchi

Kwa maslahi mapana ya taifa, Zitto ungana na Tundu Lissu tuchukue nchi

Mkuu bila kupinga maelezo yako mazuri, unasema kuwa Zito ndio anayefaa na iwapo Lissu atachaguliwa hatafika popote! Uko serious kweli. Ni kweli Zito ni mzuri, lakini sitaki kuamini eti ni mzuri sana, na Lissu hawezi kufika popote. Hapa naona kwako ni mahaba niue kwa Zito. Niliwahi kusema huko nyuma, kuwa Zito ni mzuri kwenye kujenga hoja, na hata akiwa rais atakuwa rais mzuri kwani amebalance kwenye uchumi, demokrasia na hata kijamii, ila chama chake kina ushawishi mdogo. Lissu ni mjenga hoja mzuri na ana mvuto mkubwa, ila tatizo lake naona atajikita zaidi kwenye mifumo ya kisheria, hatimaye tukajikuta tuna tatizo la sasa la rais anayejali miundombinu tu na kusahau mengine. Ifahamike Lissu yuko kwenye chama chenye mvuto na ushawishi mkubwa kwa wengi wanaopenda siasa za upinzani.

Kwa taarifa yako iwapo Lissu atagombea kupitia cdm, na Zito kupitia ACT, ni dhahiri Lissu atapata kura nyingi tena kwa mbali kuliko Zito, kutokana na nguvu ya vyama vyao. Ila kiukweli Zito anaweza kuwa rais mzuri kuliko Lisu kutokana na sababu nilizotaja hapo juu.

Nimeangalia hapo uliposema kuwa Membe ana ushawishi kuliko Zito + Lissu. Sijui umetumia kigezo gani. Ukitaka kujua Membe ana mvuto au hana, asiende cdm ambayo tayari ina uungwaji mkono mkubwa, aende ACT, TLP au TADEA kisha uje utoe mrejesho hapa jukwaani.
Ushawishi wa Membe dhidi ya Lissu na Zitto sio wakupapasa.Itizame CCM kisha tizama upepo wa Membe kwenye kinyang'anyiro cha 2015.
Ila sishauri ku change gia angani kwani kurudi kwa Lowasa CCM kumeacha jeraha kwa wananchi kiasi ambacho Membe hawezi kuaminika tena.
Hata hivyo mimi sijasema Zitto awanie uraisi,ila nimesema ZZK ni bora kuliko Lissu ila nivema akapatikana kiongozi makini zaidi kuufanya uchaguzi ujao kuwa mwepesi.
 
Soma paragraph ya 2 kutoka mwisho ya mleta hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa wewe naye usiwe mjinga! Watu tuko humu 24/7, mleta uzi amehariri post yake ya mwanzo, yaani ame-edit content ya maoni yake ya mwanzo.

Binafsi I have nothing personal against mleta uzi lakini ni kweli mwanzoni alisema mmoja agombee urais mwingine umukamu wa rais.

Sasa kwenye haya mambo kutokujua ni jambo la kawaida,binafsi najifunza mambo mapya kila mwaka. Pamoja na maisha magumu, siku zote huwa najitahidi kusoma vitabu na news articles, vinanijenga.
Halafu ni wazi, si kila mtu humu ni constitutional law expert au political scientist. Tukubali makosa, edit haisaidii.
 
Naunga mkono hoja,

Act waachiwe znz na ACT waiachie Tanganyika isopokuwa majimbo ya viongozi tu
 
Ushawishi wa Membe dhidi ya Lissu na Zitto sio wakupapasa.Itizame CCM kisha tizama upepo wa Membe kwenye kinyang'anyiro cha 2015.
Ila sishauri ku change gia angani kwani kurudi kwa Lowasa CCM kumeacha jeraha kwa wananchi kiasi ambacho Membe hawezi kuaminika tena.
Hata hivyo mimi sijasema Zitto awanie uraisi,ila nimesema ZZK ni bora kuliko Lissu ila nivema akapatikana kiongozi makini zaidi kuufanya uchaguzi ujao kuwa mwepesi.

Ushawishi wa Membe ni huko huko ccm, hivyo apambane akiwa huko huko ccm. Hana ushawishi wowote nje ya ccm. Ni kweli Zito ni bora kuliko Lisu kwa upana wake, hata mimi sina ubishi na hilo. Ila kwa ushawishi alionao Lissu, ana nguvu kuliko Zito. Zito bado yuko kwenye chama chenye ushawishi mdogo, ili Zito apate uungwaji mkono hasa huku bara, hana jinsi zaidi ya kuwapata washabiki wa wapiga kura wa cdm.
 
Najua kuna watu wapo kazini kuhakikisha Membe anagombea urais kupitia ACT lakini siyo kwa maslahi ya taifa bali ni kwa maslahi ya CCM.

Nashauri ZittoTundu Lissu wapitie bandiko ili wafanye kitu kwa maslahi mapana ya upinzani kwa ujumla,nawahakikishia mtashinda.

Membe hawezi kushinda urais hata siku moja maana hatakuwa na back-up ya nguvu ya umma kama itakavyokuwa kwenu.

Najua kuna vijana wa Makumbusho wanakufata wakikwambia umchukue Membe ila nakuhakikishia wanakuingiza mtegoni kama ilivyokuwa kwa Lowassa na chadema. Lissu na wewe ndio mna % kubwa ya kushinda urais mwaka huu. Kubali uwe waziri mkuu, Lissu awe Rais.

Nyaraka zinawabeba otherwise msije kuwalaumu Watanzania.

Why not Tundu Lisu aungane na zitto?

Tundu Lissu ana kipi cha raia kumpa kura? Au kura za huruma??

Acheni utani

We warnes you kufukuza wale watu CDM ndio lilikuwa kaburi, mkatetea na kujiona wanababe

CDM imwombe zitto, na sio zitto ajilete.
 
Huu ushauri ndio cdm waliuavaa mkenge wa Lowassa. Sikatai ACT kumchukua Membe maana bado inajijenga hivyo inaweza kujaribu lolote. Lakini sishauri wapinzani wengine hasa cdm kukubali Membe kuwa mgombea wa upinzani wote. Hao watu toka ccm hawana uwezo wowote wa kufanya siasa nje ya mbeleko za vyombo vya dola. Ni vyema tume huru ya uchaguzi ikadaiwa kwa nguvu zote, kisha wapinzani wachague mtu aliye kwenye upinzani na sio kuokota hao wachovu toka ccm.
Hapa nakubaliana na wewe, wanasiasa wengi wa CCM hawawezi kupambana nje ya mfumo wa dola! Dola kwao ndio kila kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninacho wapenda hu mnajitekenya wenyewe na kucheka wenyewe [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Najua kuna watu wapo kazini kuhakikisha Membe anagombea urais kupitia ACT lakini siyo kwa maslahi ya taifa bali ni kwa maslahi ya CCM.

Nashauri ZittoTundu Lissu wapitie bandiko ili wafanye kitu kwa maslahi mapana ya upinzani kwa ujumla,nawahakikishia mtashinda.

Membe hawezi kushinda urais hata siku moja maana hatakuwa na back-up ya nguvu ya umma kama itakavyokuwa kwenu.

Najua kuna vijana wa Makumbusho wanakufata wakikwambia umchukue Membe ila nakuhakikishia wanakuingiza mtegoni kama ilivyokuwa kwa Lowassa na chadema. Lissu na wewe ndio mna % kubwa ya kushinda urais mwaka huu. Kubali uwe waziri mkuu, Lissu awe Rais.

Nyaraka zinawabeba otherwise msije kuwalaumu Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani act ni chama cha upinzani? Tuanzie hapo kwanza
 
Wakiungana hao, mi nakuambia patachimbika, ushindi asbh tu. CCM wamegeuza Nccr ndio kichaka cha kujifichia Tume huru. .Nawashauri chadema na ACT waendelee kukaza hivyo hivyo
 
..Katiba hairuhusu hicho ulichopendekeza.

..Raisi na Makamu wanatakiwa watoke pande tofauti za muungano.

..Raisi akitoka Tanganyika / Tz bara Makamu anatakiwa atoke Zanzibar. And vice versa.

..Zitto na Juma Duni wanaweza kugombea kama Raisi na Makamu.

..Tundu Lissu na Juma Duni pia wanaweza kugombea.

NB.

..Waziri Mkuu atatokana na chama chenye wabunge wengi.

..Waziri Mkuu pia anaweza kuwa ni mbunge anayeungwa mkono na wabunge wengi. Nadhani framers waliangalia mazingira ambapo hakuna chama chenye clear majority bungeni.

..Spika anaweza kuchaguliwa miongoni mwa wabunge, au anaweza kutoka nje ya bunge ilimradi apigiwe kura na wabunge wengi.
Hivi huwa mnaona nini kwa huyo mzee Duni, uzanzibar tu au kuna kingine
 
Usiye mjinga, kama ameosha edit tatizo lako ni nini?

Back
Top Bottom