Kwa maslahi mapana ya taifa, Zitto ungana na Tundu Lissu tuchukue nchi

Najua kuna watu wapo kazini kuhakikisha Membe anagombea urais kupitia ACT lakini siyo kwa maslahi ya taifa bali ni kwa maslahi ya CCM.

Nashauri ZittoTundu Lissu wapitie bandiko ili wafanye kitu kwa maslahi mapana ya upinzani kwa ujumla,nawahakikishia mtashinda.

Membe hawezi kushinda urais hata siku moja maana hatakuwa na back-up ya nguvu ya umma kama itakavyokuwa kwenu.

Najua kuna vijana wa Makumbusho wanakufata wakikwambia umchukue Membe ila nakuhakikishia wanakuingiza mtegoni kama ilivyokuwa kwa Lowassa na chadema. Lissu na wewe ndio mna % kubwa ya kushinda urais mwaka huu. Kubali uwe waziri mkuu, Lissu awe Rais.

Nyaraka zinawabeba otherwise msije kuwalaumu Watanzania.

Mkuu. Umeona ujumbe wa Zitto kuhusu Prof Janabi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna vitu huwa vinachekesha sana. Kama hii thread
 
Waziri Mkuu anatokana na chama kinachokuwa na wabunge wengi. Hivyo kushinda urais si guarantee ya kuunda serikali.

Kwa hii katiba ilivyo mbovu ukiwa rais unafanya chochote hata kinyume cha sheria, na hakuna atakayekufanya chochote. Ukiona rais wa nchi hii anaitii katiba ujue ni muungwana tu, na sio kuwa anaiheshimu katiba. Ushahidi wa hilo umepatikana sasa baada ya Magufuli kuwa rais, kiasi kwamba Mwinyi, Mkapa na Kikwete wanasikitika kwanini hawakufanya lolote wapendalo, huku katiba ikiwa haina meno yoyote dhidi ya rais.

Ukishakuwa rais hata ukiwa na mbunge mmoja, unaunda serikali, na watu wanahama vyama vyao kisha wanaigiza kukuunga mkono, halafu wewe unatumia madaraka yako kuwapa ubunge kwa ubabe. Haya tuneyashudia sasa kwenye nchi hii. Nadhani umeona uchaguzi wa SM za mitaa na kile kilichotokea, kwenye nchi ambayo kabisa katiba inafuatwa ule uhuni wa wazi ungeuuona?
 
Najua kuna watu wapo kazini kuhakikisha Membe anagombea urais kupitia ACT lakini siyo kwa maslahi ya taifa bali ni kwa maslahi ya CCM.

Nashauri ZittoTundu Lissu wapitie bandiko ili wafanye kitu kwa maslahi mapana ya upinzani kwa ujumla,nawahakikishia mtashinda.

Membe hawezi kushinda urais hata siku moja maana hatakuwa na back-up ya nguvu ya umma kama itakavyokuwa kwenu.

Najua kuna vijana wa Makumbusho wanakufata wakikwambia umchukue Membe ila nakuhakikishia wanakuingiza mtegoni kama ilivyokuwa kwa Lowassa na chadema. Lissu na wewe ndio mna % kubwa ya kushinda urais mwaka huu. Kubali uwe waziri mkuu, Lissu awe Rais.

Nyaraka zinawabeba otherwise msije kuwalaumu Watanzania.

Mkuu naona unapendekeza jambo zuri, lakini hujui kwamba ni zuri kinadaharia kuliko hatari itakayotokea huko mbeleni. Kwangu mimi sasa hivi siamini tena katika ushirikiano wa vyama, nadhani unaona kinachoendelea kwa Mbatia baada ya juzi kukutana na Magufuli. Ni vyema ACT ikamsimamisha mgombea wake, na cdm ikamsimamisha mgombea wake. Tatizo la ccm inafahamika ni nguvu ya cdm, haya mambo ya kujichanganya na vyama vingine, ni kukaribisha hatari ya ccm kuja kuivuruga cdm. Nadhani umeona ni jinsi gani ccm imewatumia wanaccm walijiunga cdm, kwa kuwarubuni kurejea ccm kwa gharama ya kuichafua cdm. Huo ushauri unaoutoa utakuja kuivuruga sana cdm huko mbeleni. Pls stop this ASAP.
 
..Katiba hairuhusu hicho ulichopendekeza.

..Raisi na Makamu wanatakiwa watoke pande tofauti za muungano.

..Raisi akitoka Tanganyika / Tz bara Makamu anatakiwa atoke Zanzibar. And vice versa.

..Zitto na Juma Duni wanaweza kugombea kama Raisi na Makamu.

..Tundu Lissu na Juma Duni pia wanaweza kugombea.

NB.

..Waziri Mkuu atatokana na chama chenye wabunge wengi.

..Waziri Mkuu pia anaweza kuwa ni mbunge anayeungwa mkono na wabunge wengi. Nadhani framers waliangalia mazingira ambapo hakuna chama chenye clear majority bungeni.

..Spika anaweza kuchaguliwa miongoni mwa wabunge, au anaweza kutoka nje ya bunge ilimradi apigiwe kura na wabunge wengi.
Mbona jamaa kasema zito akubali kuwa waziri mkuu, which means jamaa kajua hawezi gombea umakam raisi. Amesema zito na lissu waungane just kutia nguvu, kutogawa kura nk, ko inaweza ikawa chama cha zito kikatoa mgombea mwenza, then baada ya kushinda zito anakuwa waziri mkuu. Mbona jamaa yupo clear halafu mna mbully kwamba haelewi katiba mara nini, kumbe nyie ndio hamjasoma vizuri.

..alikosea mwanzo ndiyo maana unaona kuna jamaa wa ccm wanamtukana.

..baada ya hapo amebadilisha kimyakimya na wewe umekuja kusoma wakati ameshabadilisha uzi wake.

..walau ungenipongeza kwa kutumia lugha ya kistaarabu na kuchukua muda wangu kumuelekeza.
 
Na 'back-up ya nguvu ya umma' unamaanisha ww mwenyewe ndio umma! Kuna watu mnaota ndoto za mchana eeh! Wasaliti hao wa nchi yetu na makuadi wa mabeberu na mashoga wapewe nchi gani? Au unamaanisha kipande cha ardhi cha ekari moja cha kulima huko kijijini kwenu eeh!?
😀😆😀watu mmefuzu kozi za kukatisha tamaa wenzenu
 
Kwa hii katiba ilivyo mbovu ukiwa rais unafanya chochote hata kinyume cha sheria, na hakuna atakayekufanya chochote. Ukiona rais wa nchi hii anaitii katiba ujue ni muungwana tu, na sio kuwa anaiheshimu katiba. Ushahidi wa hilo umepatikana sasa baada ya Magufuli kuwa rais, kiasi kwamba Mwinyi, Mkapa na Kikwete wanasikitika kwanini hawakufanya lolote wapendalo, huku katiba ikiwa haina meno yoyote dhidi ya rais.

Ukishakuwa rais hata ukiwa na mbunge mmoja, unaunda serikali, na watu wanahama vyama vyao kisha wanaigiza kukuunga mkono, halafu wewe unatumia madaraka yako kuwapa ubunge kwa ubabe. Haya tuneyashudia sasa kwenye nchi hii. Nadhani umeona uchaguzi wa SM za mitaa na kile kilichotokea, kwenye nchi ambayo kabisa katiba inafuatwa ule uhuni wa wazi ungeuuona?

Nikwasababu ana wabunge wengi. Lakini huwezi fanya chochote kama una wabunge wachache. Katiba siyo nzuri kwa nchi za Afrika ikitokea chama kinatoa rais na kingine kina wabunge wengi na waziri mkuu ncho haitatawalika.
 
..kuvunja muungano wa serikali 2 na kuunda muungano wa serikali 3.
Basi humjui babu duni wewe, Duni anaamini katika Zanzibar yenye mamlaka kamili (Kama ilivyokuwa kabla ya mwaka 1964 April)
swali ni Je kuwa na Zanzibar yenye mamlaka kamili Kuna muungano hapo
nb: duni ana misimamo isiyoyumba
 
Tumaini pekee la upinzani nchini ni ushirikiano wa kiapo cha damu, kama MAUMAU, kati ya CHADEMA na ACT!💥

NB: SIO ULE UNAFIKI WA UKAWA WA WENGINE ETI KUJIONA WANA POWER ZAIDI YA WENZAO!
👊 ✌✌✌💥
 
Najua kuna watu wapo kazini kuhakikisha Membe anagombea urais kupitia ACT lakini siyo kwa maslahi ya taifa bali ni kwa maslahi ya CCM.

Nashauri ZittoTundu Lissu wapitie bandiko ili wafanye kitu kwa maslahi mapana ya upinzani kwa ujumla,nawahakikishia mtashinda.

Membe hawezi kushinda urais hata siku moja maana hatakuwa na back-up ya nguvu ya umma kama itakavyokuwa kwenu.

Najua kuna vijana wa Makumbusho wanakufata wakikwambia umchukue Membe ila nakuhakikishia wanakuingiza mtegoni kama ilivyokuwa kwa Lowassa na chadema. Lissu na wewe ndio mna % kubwa ya kushinda urais mwaka huu. Kubali uwe waziri mkuu, Lissu awe Rais.

Nyaraka zinawabeba otherwise msije kuwalaumu Watanzania.
I agree

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom