Kwa mfano ungekuwa wewe ndio kiongozi mwenye dhamana ungechukua hatua zipi kuhusu Rufiji

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Tunatafuta solutions juu ya hali inayo endelea RUFIJI.




Kwa mfano ungekuwa wewe ndio kiongozi mwenye dhamana ungechukua hatua zipi juu ya hali inayo endelea RUFIJI?

Tiririka mawazo yako yanaweza kuonekana.

Unaweza kusimama kama waziri, injinia, mkurugenzi wa TANESCO, meneja wa bonde la RUFIJI, mkuu wa wilaya vyovyote toa mawazo yako tuyapime.
 
Nawahamisha wakaazi wote wa Rufiji Handeni,halafu Rufiji nawakodishia Waarabu miaka mia moja.
 
Kwanza ningekuwa mkweli tu kwa kuwaambia chanzo cha mafuriko haya ni...... Ili tusiendelee kusumbuana kila mala nikuwahamisha wote hilo eneo limeshakuwa muache muache
 
1. Kuhamisha watu wote toka eneo hilo huku wakilipwa fidia.

2. Chakata upya uwepo wa bwawa na mwl Nyerere. tujue kwa sasa faida na hasara zake ni zipi.
 
Wananchi wamelifuata bwawa na kujenga makazi. Waondoke.
 
Nawalipa fidia na kuwahamishia msomera wakakae na wamasai. Kimsingi bwawa halina tatizo ila utekelezaji wake ndio umefanyika kienyeji.
 
Hapo hakuna cha kufanya zaidi ya kupeleka misaada na special rescue team..

Hakuna siasa ktk jambo kama hilo then NEXT sasa ni kuweka mikakati.

Ngj niulize kidg hivi huko si naskia kuna MAMBA?
 
Hapo hakuna cha kufanya zaidi ya kupeleka misaada na special rescue team..

Hakuna siasa ktk jambo kama hilo then NEXT sasa ni kuweka mikakati.

Ngj niulize kidg hivi huko si naskia kuna MAMBA?
Ahsante kwa mchango wako
 
Ningekua mimi ndio Rais.

Ningemfuta Kazi Mkurugenzi wa Mipango miji nchini.
Kufuta kazi afisa Ardhi Rufiji

Futa kazi DED Rufiji.
Ningepima maeneo mengine Rufiji ni kubwa kuweka ukomo wa shuguli na maisha ya binadamu kutoka bonde la Mto Rufiji.

NINGECHIMBA mabwawa mengine pembeni yenye uwezo wa kubeba maji lita bili 500 ili Rufiji ikijaa itapikie huko iwe Reserve.

NINGEANZISHA kilimo cha umwagiliaji kikubwa mazao ambayo Dar na mikoa jirani wangefaidi..Organic Agriculture no mbolea...
 
ni kupewa tu fidia na ilo eneo kubaki tu la shuhuli husika ,,ila kwa makazi apana aseee
 
Ningewahamisha kila mtu sehemu anayotaka na kuwajengea nyumba zao upya na kuwapa mtaji ili angalau wawe kama walivyokuwa kabla ya mafutiko kutokea.halafu eneo Lao lililo athurika ningegeuza bwana la samaki mamba kiboko nk
 
Kuwapa mbegu za mazao kama wazee wapumbav machawa walivyotaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…