Kwa mfano ungekuwa wewe ndio kiongozi mwenye dhamana ungechukua hatua zipi kuhusu Rufiji

Kwa mfano ungekuwa wewe ndio kiongozi mwenye dhamana ungechukua hatua zipi kuhusu Rufiji

Ningewaambia Arab contractor wawape kazi TVA-Tennessee Valley Authority wafix makosa waliofanya na mitigation plan kuondoa mafuriko Rufiji.
 
Unajua gharama yabujenzi wewe au unaongea tu?? Nyumba ya vyumba vitatu 25m puuuhhh
By the way, watabomoa nyumba za zamani na kuhamisha material.
Pili hii ni hisani. Utaki unaacha uendelee kuishi kwenye bwawa.
 
Nawahamisha wananchi halafu nabomoa bwawa la jiwe
 
.......kimsingi lile bwawa halikutegemewa kuleta maafa, hata risk assessment zilizofanywa zililenga hasa mabadiliko ya tabia ya nchi kwa upande mmoja tu wa kuleta ukame na tabia za kijangwa, hivyo ziishaangaliwa, mind you kwa mvua za kawaida hili bwawa lilitegemewa kujaa kwa miaka miwili.........
.......tatizo limekuja kuwa kinyume na ilivyotegemewa mvua zimekuwa nyingi kupitia kiasi na hivyo kusababisha bwawa kujaa haraka na kusababisha mafuriko makubwa na sio ukame ambao ungesababishwa na kupotea kwa uoto wa asili na destruction of ecological set up.........
.........nini kifanyike, naamini hali ya mvua ikiendelea hivi lazima serikali itatangaza rasmi kuwahamisha wakazi na kuwalipa fidia, in fact hii ni kawaida kama vile kuingia gharama fulani ktk project ambazo hukuziwaza au hukuzipa uzito ktk project au biashara hiyo......
.......mvua zikipungua kiasi nashauri serikali itenge bajeti ya kuhakikisha kuwa inaestablish other project katika blonde la mto rufiji, panatakiwa pawe kama Nile valley na Tennessee valley authority ambapo projects za fishing, powe generation, transport na irrigation schemes zinaingizia pato kubwa inchi na at the same time environmental conservation iko well ensured.......
Mkuu mchango wako umeuleta kama kiongozi fulani hivi sijui tuseme ni waziri.
 
Hapo kuna wahuni wanataka wapige hela na watanzania tayari wameshaingia King.
 
Back
Top Bottom