Kwa mfano ungekuwa wewe ndio kiongozi mwenye dhamana ungechukua hatua zipi kuhusu Rufiji

Kwa mfano ungekuwa wewe ndio kiongozi mwenye dhamana ungechukua hatua zipi kuhusu Rufiji

Ningewaletea tamasha kubwa la kina joti, mwijaku, baba levo na wengineo ili kuwakumbusha ni wapi wanatakiwa kupiga kura
 
Walipwe fidia ili wahame.
Nyumba ya chumba kimoja Tsh mil 7.
Chumba na sebule Tsh mil 15.
Vyumba viwili na sebule Tsh mil 20.
Vyumba vitatu na sebule Tsh mil 25.
Vyumba vinne (na zaidi) na sebule Tsh mil 35.
 
Natangaza Maafa na kuviagiza vyombo vyote vinavyo husikq kwenda kuokoa /Kuhamisha kuwapeleka temporarily camps salama zenye huduma muhimu za muda mfupi kama ....maji makadhi mobile health care nk
 
Bwawa lile ningelifutilia mbali maana limeingilia uasili wa hapo,pia pale mikokoni karibu na daraja la salander,yale mahekalu yaliyojengwa kwenye bonde lile ningevunjilia mbali na wahusika wangebeba costs zote,mafuriko ya maji kule jangwani,kigogo yanasababishwa na mavamizi hawa
 
Ningewachukua wakristo wote na kwenda kuwaweka kwenye safina.Waliobaki wangebaki kusaga meno
 
Ningekua mimi ndio Rais.

Ningemfuta Kazi Mkurugenzi wa Mipango miji nchini.
Kufuta kazi afisa Ardhi Rufiji

Futa kazi DED Rufiji.
Ningepima maeneo mengine Rufiji ni kubwa kuweka ukomo wa shuguli na maisha ya binadamu kutoka bonde la Mto Rufiji.

NINGECHIMBA mabwawa mengine pembeni yenye uwezo wa kubeba maji lita bili 500 ili Rufiji ikijaa itapikie huko iwe Reserve.

NINGEANZISHA kilimo cha umwagiliaji kikubwa mazao ambayo Dar na mikoa jirani wangefaidi..Organic Agriculture no mbolea...
Ahsante sana kwa mchango
 
Walipwe fidia ili wahame.
Nyumba ya chumba kimoja Tsh mil 7.
Chumba na sebule Tsh mil 15.
Vyumba viwili na sebule Tsh mil 20.
Vyumba vitatu na sebule Tsh mil 25.
Vyumba vinne (na zaidi) na sebule Tsh mil 35.
Unajua gharama yabujenzi wewe au unaongea tu?? Nyumba ya vyumba vitatu 25m puuuhhh
 
Ningewahamisha kila mtu sehemu anayotaka na kuwajengea nyumba zao upya na kuwapa mtaji ili angalau wawe kama walivyokuwa kabla ya mafutiko kutokea.halafu eneo Lao lililo athurika ningegeuza bwana la samaki mamba kiboko nk
Ahsante kwa mchango
 
Kubomoa bwawa la mwl nyerere na bila aibu alilikataa Leo pamepewa jinalake. Laaana hii
 
Wanawahoji wazee wenye vyeo vyeo na wajinga wajinga.....wangepiga tathmini wahamishe wote walio bondeni...ingawa nasikia huwa wanarudi......wana makazi sehemu tofauti hawakubali kuacha mabonde yao .....mafuriko kila baada muda fulani takribani miaka 4
 
Wanawahoji wazee wenye vyeo vyeo na wajinga wajinga.....wangepiga tathmini wahamishe wote walio bondeni...ingawa nasikia huwa wanarudi......wana makazi sehemu tofauti hawakubali kuacha mabonde yao .....mafuriko kila baada muda fulani takribani miaka 4
Ahsante kwa mchango wako
 
.......kimsingi lile bwawa halikutegemewa kuleta maafa, hata risk assessment zilizofanywa zililenga hasa mabadiliko ya tabia ya nchi kwa upande mmoja tu wa kuleta ukame na tabia za kijangwa, hivyo ziishaangaliwa, mind you kwa mvua za kawaida hili bwawa lilitegemewa kujaa kwa miaka miwili.........
.......tatizo limekuja kuwa kinyume na ilivyotegemewa mvua zimekuwa nyingi kupitia kiasi na hivyo kusababisha bwawa kujaa haraka na kusababisha mafuriko makubwa na sio ukame ambao ungesababishwa na kupotea kwa uoto wa asili na destruction of ecological set up.........
.........nini kifanyike, naamini hali ya mvua ikiendelea hivi lazima serikali itatangaza rasmi kuwahamisha wakazi na kuwalipa fidia, in fact hii ni kawaida kama vile kuingia gharama fulani ktk project ambazo hukuziwaza au hukuzipa uzito ktk project au biashara hiyo......
.......mvua zikipungua kiasi nashauri serikali itenge bajeti ya kuhakikisha kuwa inaestablish other project katika blonde la mto rufiji, panatakiwa pawe kama Nile valley na Tennessee valley authority ambapo projects za fishing, powe generation, transport na irrigation schemes zinaingizia pato kubwa inchi na at the same time environmental conservation iko well ensured.......
 
Tunatafuta solutions juu ya hali inayo endelea RUFIJI.


View attachment 2960810

Kwa mfano ungekuwa wewe ndio kiongozi mwenye dhamana ungechukua hatua zipi juu ya hali inayo endelea RUFIJI?

Tiririka mawazo yako yanaweza kuonekana.

Unaweza kusimama kama waziri, injinia, mkurugenzi wa TANESCO, meneja wa bonde la RUFIJI, mkuu wa wilaya vyovyote toa mawazo yako tuyapime.
Wahamishiwe HANDENI...
 
Back
Top Bottom