Kwa mnaotaka kuja Norway, ujipange kwa vyakula na vinywaji

Kwa mnaotaka kuja Norway, ujipange kwa vyakula na vinywaji

Ukitaka kwenda huko unafungasha kiroba chako cha mchele kilo 100, unga wa dona na michembe. Maisha safi.
Kwenye ndege unaweza kukwamna au kushindwa gharama
 
Sasa embu toa ufafanuzi kidogo uthamani wa hiyo hela ya huko dhidi ya kwetu, maana unazidi tu kunichanganya.

Wanatumia uero ama kitu gani na hudai kuwa inathamani sana kuliko yetu!

Sasa kwa mwendo huo wa kununua kilo ya nyama tisini elfu, hiyo hela inaizidije thamani shilingi ya Tz, kama kwenda kwenye manunuzi mpaka uwe na sandarusi la pesa, wakati Tz noti1 elfu10 unarudi na chenji?
Pesa yao Ina thamani kuliko ya Tz Ila sio sana
 
Hii thread iko kitapeli mnoo.
Kuna watu wanakwenda kutapeliwa hapa JF kiulaini sana.

Kwa kuwasaidia baadhi ya watu hapa JF ambao hawajawahi kufika ulaya, taarifa nzima ya gharama na mfumo wa maisha ya eneo lolote husika katika nchi ya Norway inaweza kuipata kwa usahihi wa karibu 99% kwenye mitandao ya taarifa rasmi za nchi ya Norway. Unaweza kujua hata bei ya kununua changadoa na ukapewa, huhitaji kuja kulishwa matango pori ya wajanja na matapeli wa hapa JF.

Kwa mfano kupitia websites za;
-numbeo.com
-fullsuitcase.com
Haina shida
 
Hizo hela ukibadili ki tsh ni shilingi ngapi?? Mfano 70000 huku ni sh ngapi?? Au 8500 kwa hela yabongo ni sh ngapi?
Nimeweka kwa tsh, hivyo wewe Soma Kama ilivyo
 
Hakuna kitu bei chee Ulaya kama chakula! Nchi nyingi za Ulaya hasa EU zina standard moja ya maisha,tofauti ni ndogo sana. Sijafika Norway ila sidhani kama kilo ya nyama inafika 70,000! Nakumbuka enzi tunapiga box nyama ya kuku tulikuwa tunanunua kwenye box unachagua mapaja au vidari na box kubwa sana tunakula wiki nzima watu watano na wageni wakitokea, box lilikuwa £12, mchele Basmati kg5 ilikuwa £12-15,nyama lamb kilo £3 hivi nyama ya ng'ombe iko juu kama £4 kwa kilo au zaidi kidogo, mazagazaga mengine mostly kwenye makopo kwenye supermarket majuisi,yoghurt,etc bei chee tu. Kwa mishahara ya kubeba box hata minimum wage huumizi kichwa kwenye kula,kuvaa,kulala ndio maana unaona watu wakitoka majuu kuja bongo wanang'aa sana hata kama hawana hela za kujenga magorofa.
Sawa kaka
 
katika pitapita zangu zote majuu, nilichowaapreciate na kuona wametupita mbali sana na hatutakuja kuwakuta ni tabia ya usafi, kila kitu kisafi kuanzia mazingira ya nje, makazi, vyakula, usafiri, magari yote mapya, watu wasafi, hukuti nzi hata sehemu moja utatafuta inzi hutamkuta, hadi hewa safi. ukifika kule hata ukila chakula cha kimasikini tu ile kukaa miezi miwili mitatu hadi ngozi inabadilika unanawiri, yaani Mungu kawabariki upako wa maisha mazuri hadi ya hewa inakunawirisha hata kama hali yako ya chini tofauti na bongo mtu ana mihela lakini kakomaa utafikiri anachuna ngozi za watu, ukitoka huko kushuka tu uwanja wa dsm, kuanzia harufu ni tofauti kabisa, mazingira tofauti, watu tofauti hafuru ya umasikini imetapakaa kila mahali. Mungu atusaidie waafrica.
🤣🤣🤣🤣 hatari sana.
 
Hivi siku hizi shule ya msingi na sekondari huko Bongo, akina Ndalichako wametoa topic ya punctuation?

Back
Top Bottom