Kwa mshahara wa Tsh. 765,000/= nikizama benki naweza kopesheka kiasi gani?

wanasema mkopo ni chanzo. cha umasikini nilitegemea wamshauri mjuba alternative ili ajiendeleze vizur kifedha
Mikopo ni chanzo cha umaskini kwa maskini kwasababu wengi hawana financial education ila kwa matajiri hakuna kitu kinawatajirisha kama mikopo. Mataasisi mengi makubwa yanaendeshwa kwa mikopo humu duniani. Elimu za uchumi na uwekezaji zimetupitia kushoto kwa hiyo usitegemee kuwa utanufaika na mkopo
 
nini ushauri wako chief, nikakope wapi?
 
Usikalili mkuu,sio kila mtu aliyefanikiwa anaiba lakini pia sio kila aliye na mikopo na kubaki na 270K kama kipato cha mwezi ana maisha magumu,Tatizo mnajipa title za wasomi ila uwezo wa kupambanua mambo na kuyaweka katika uhalisia ni mdogo
Inawezekana huko kijijini mpingamiti,liwale upo kwenye shule yenye walimu wawili tu halafu ww ndie mwalimu mkuu..hivyo pesa za semina,posho mbalimbali na za miradi ya ujenzi zinapitia kwako, pia pesa za vikao na miradi ya Ccm pia zinakuangukia.
 
nini ushauri wako chief, nikakope wapi?
Bank nyingi ni pasua kichwa boss
Nenda kwa Afisa utumishi hata umshike mkono Akuweke kwenye list ile ya halmashauri, January hii ndio wanatoa kama sikosei.
Hutapewa Yote ila hio itakayobaki nenda Bank sasa, Bank Gani?
Nenda Stanbank, kwa nini? Hawa riba yao ni 13% lakini pia wana reducing rate, yaani riba inakatwa kwa kiasi kinachobaki kila unapolipa.
 
daah,najifunza mengi hapa
 
duuh ahsante chief ,napitia mengi hapa.
 
Nawishi kuchukua loan kozi life limekua likinichapa sana, wataalamu nipeni uzoefu sana.

Je, nitaweza kopesheka shingapi kwa benki ya CRDB kwa hio salary?
Mkuu samahani mimi nitaenda nje ya mada lakini ni kwa manufaa yako. Kwanza uelewe hakuna maisha marahisi huku duniani labda ushinde bahati nasibu. Kwa pesa uliyonayo hata kama ni take home usichukue mkopo labda kama una kipato kingine vinginevyo utaishi kwa aibu.

Sasa nashauri tafuta kitu cha ziada ufanye nje ya muda wa kazi au soma kozi fupi upate skills za kujiajiri nje ya muda wa mwajiri. Nakupa mifano ifuatayo.
1. Kuna rafiki yangu anafanya kazi CRDB mkoa X yeye wakati wa wiki end anafanya kazi ya landscaping kwenye nyumba za watu.
2. Nina rafiki yeye ni Mwalimu lakini alisoma kozi fupi ya hotel management kwa hivyo yuko hotel X anaingia usiku daily asubuhi yuko kwenye kazi ya umma ya serikali.
3. Nina mtu namfahamu aliwahi kufanya kazi kwenye kanisa X lakini usiku alikua Mlinzi kwenye Nyumba binafsi ya mgeni kutoka nje.
4. Soma graphic design tafuta digital marketing ujitangaze. Utafanya kazi zako baada ya muda wa mwajiri.
5. Mimi nilibahatika kusoma shahada ya pili enzi za ujana wangu kwa hivyo niliwekeza kwenye huduma ya research za shahada ya pili na ya tatu.

NB: usikope kama Huna kipato kingine utavaa kadeti iliyopauka hadi kwenye zipu.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Noted
 
shukrani chief
 
😜😜😜 kama huna pesa kuliko kuvaa kadeti bora utimbe zako Yale masulu kama ya wahindi yaliyokaa kama fuko la mashine yaani pajama sio pajama halafu chini raizoni,
Bora uonekane hamnazo.
 
Daah ukishaweka mambo ya Imani tena kwenye Riba ndio unachanganya hapo Mkuu ila unaowaona wengi kwenye gemu wali risk kukopa na wengine walifanikiwa wengine waliferi kutokana na sababu moja au nyingine...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…