Sijajua wewe familia yako unaiendeshaje mkuu, nimezaliwa kwenye familia ya biashara mzee wangu ana duka kubwa la nguo anatoa biadhaa zake Kenya au Uganda, anaesimama dukani ni Mama mzee yeye anasafiri jumatatu anarudi alhamis/ijumaa, kwahiyo mtu ambae anashida kwenye biashara ni Mama, na wamefanikiwa kwa kiasi chao na kumiliki asset nyingi tu hapo Mwanza, lakini kwa kipindi chote hicho tulipokua wadogo Mama alikua hawezi kutoa hata shilling 100 bila kumtaarifu mzee, hata tulipokua tunahitaji matumizi ya shule tulikua tunampigia simu mzee sio Mama, kwahiyo Mama ni kama msimamizi/mhasibu tu, sio kwamba nampa biashara Mwanamke alafu Mimi naenda kustarehe, biashara ni ya kwangu Mimi yeye anakua msimamizi kwa muda mchache tu nikitoka.