Kwa mtaji wa milioni 12, nifungue hardware, nafaka au phone and accessories?

Kwa mtaji wa milioni 12, nifungue hardware, nafaka au phone and accessories?

Wakuu, nipo hapa napambania kujikwamua kwenye umaskini, nipo nachakata mawazo kwa ajili ya kufanya harakati, wengi walianzia chini sana na wakafanikiwa kupata pesa nyingi.

Mawazo yangu niliyonayo ni Nafaka, vifaa vya simu pamoja na umeme, mwisho ni hardware,

Nafaka nilitaka nideal na maharage, mchele pamoja na nafaka nyingine means nazitoa porini nakuja kuziuza mjini, changamoto Mimi ni Mwalimu kwahiyo muda wa kuzunguka porini nakua nimekosa, makazi Kwa Sasa nipo kigoma.

Vifaa vya simu, kigoma huku naona vitu ni bei kubwa sana mfano USB ni 7000, earphone 5000 na vitu vingine, nikatamani niingie kwenye hii biashara kwa sababu machimbo kariakoo ya bei rahisi nayafahamu.

Vifaa vya ujenzi, hii ni hobby yangu, naipenda sana na watu wamepata pesa kweli, kigoma mfuko wa cement ni 26,000/= pamoja na vifaa vingine changamoto mji ni mdogo na competition ni kubwa, hapa kwenye hardware nilitaka nijichanganye kwwnye kununua machine ya uchomeleaji pamoja na aluminum.

Wakuu, lengo langu nipate faida ya laki 5 tu kwa mwezi.

Asanteni
Ukitaka kufanya biashara yoyote Ile nilazima uijue na unaijuaje nikwakufanya utafiti je mbinu za utafiti unazijua
 
Kwa Pesa hiyo ikiwa kwenye maandishi ni nyingi sana ila ikianza kuingia kwenye biashara ni kidogo sana. Cha msingi kwenye biashara ya hardware itakuchukua muda sana kuanza kupata wateja wako mwenye coz big fish washawekeza na wengi wao wanachukua moja owa moja kutoka kiwandandi. Kama itasaidia tembea na hilo wazo la vifaa simu wekeza ingiza pesa kidogo zen unaendelea kusoma uelekeo wake kama utakuwa na faida na hakikisha pesa yote huiweki kwenye biashara unayotaka kuianzisha fanya discipline na utaratibu wa hali ya juu na usetegeme hiyo faida kwa unavyoanza. Ni mawazo tu
 
Ukitaka kufanya biashara yoyote Ile nilazima uijue na unaijuaje nikwakufanya utafiti je mbinu za utafiti unazijua
Mbinu za utafiti nazielewa kwa kiasi chake, maana naanzia sokoni kujua watu wanauzaje, pia kutafuta machimbo ambayo bidhaa nitazipata kwa bei nafuu, pia location ni muhimu, kuna nyingine zaidi ya hivyo
 
Kwa Pesa hiyo ikiwa kwenye maandishi ni nyingi sana ila ikianza kuingia kwenye biashara ni kidogo sana. Cha msingi kwenye biashara ya hardware itakuchukua muda sana kuanza kupata wateja wako mwenye coz big fish washawekeza na wengi wao wanachukua moja owa moja kutoka kiwandandi. Kama itasaidia tembea na hilo wazo la vifaa simu wekeza ingiza pesa kidogo zen unaendelea kusoma uelekeo wake kama utakuwa na faida na hakikisha pesa yote huiweki kwenye biashara unayotaka kuianzisha fanya discipline na utaratibu wa hali ya juu na usetegeme hiyo faida kwa unavyoanza. Ni mawazo tu
Ni kweli mkuu, najua mwanzo ni ngumu sana.
 
Na ili hii biashara ya spare za simu akimbize ni lazima awe na fundi wa simu au yeye mwenyewe ajifunzi ufundi simu hii itamrahisishia sana kuwa connected direct na wateja na mafund simu ambao hawa mafundi ndio wateja wakubwa wa spare za simu
 
Weka uoga pembeni kisha anza na ulicho nacho!

Usiogope comments za kutisha kama hizi "hiyo pesa ni ndogo" wewe komaa na comments za kujenga kama hizi "angalia location uliyopo na kisha ufanye research chap upate wazo la biashara" la sivyo utajiona huwezi fanya chochote ndugu!

Unajua inashangaza sana mtu anapokuambia 12M ni ndogo kwa hardware, lakini ukipiga mahesabu ya kawaida ya vitu kama vitasa vya milango, misumari, nyundo, plaizi, bisi bisi, misumeno, bawaba, sink za choo zipo kibao za 18,000 jumla, vi-soap dish, bomba za kuogea bei chee jumla, koki za kawaida 2,500 kibao tu! Yaani kiufupi ni kwamba unaweza kununua hata mzigo wa 5M kwa jumla na ukapeleka dukani kwako ukapata faida nzuri tu, unaenda kwa maduka makubwa ya jumla kama wa kina Kamaka.

Cha kuzingatia ni nidhamu ya biashara ndugu yangu, kama mkeo ndio atakuwa msimamizi, basi unamuwekea kijana mmoja wa kumsaidia, unaanza naye kwa malipo ya 140,000 kwa mwezi na kila wiki unampa 20,000 ambayo jumla inakuwa 200,000 kwa mwezi. Hiyo ya wiki itamsaidia kwa mambo madogo. kodi unafanya isizidi 250,000 kwa mwezi, hiyo ni kulingana na vitu utakavokuwa unauza kwa kuanzia.

Mkeo akiwa na nidhamu ya biashara akaweza kutunza faida na kukuza biashara yenu, sasa taratibu unaanza kuongeza vitu vikubwa kidogo kidogo kama cement hata mifuko 100 kwanza, bati pisi kadhaa, mbao, huku unaendelea kusikilizia. Lengo ni kubaki kwenye limit yako, yaani kama una akiba ya 4M unaagiza mzigo wa 2.5M na nyingine unaacha ya dharura, maana bishara siku zote ina pande mbili ambazo ni faida na hasara, kwahivyo ni lazima uwe na back-up capital walau kidogo ya kukulinda.

Ukiweza kuanza kidogo kidogo hivyo na kwa nidhamu, amini kwamba itafikia siku utakodi eneo la hadi 1M kwa mwezi kwasababu utakuwa na mzigo mkubwa sana! Na kijana wako uliyeanza naye kwa 140,000 atakuwa anapata 400,000 iliyonyooka kwa mwezi pamoja na bonus za kila siku! Uzuri ni kwamba ukishajenga jina na ukawa mteja wa jumla wa mara kwa mara, makampuni makubwa ya uzalishaji watakupa mzigo mkubwa na utawalipa kila utakaporudi kuchukua mzigo mwingine (kama bati, simtank, cement, nk), kwahivyo badae unaweza jikuta unazungusha mtaji mkubwa sana ikiwa utathubutu kuchukua hatua leo!

Kila la kheri ndugu!
 
Back
Top Bottom