Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Habari zenu ndugu,Nipo dodoma , nina mtaji wa laki mbili (200000) nimefanya kazi ngumu hadi kuupata ikiwa ni pamoja na kubeba zege na kuchimba mitaro.
Kwa wale wajuzi wa maswala ya biashara nipeni msaada wa wazo la biashara .japo nipumzike na mimi na hizi kazi ngumu .
Na mungu awabariki
Kama upo Dodoma hivyo ni fursa kuwa Dodoma nakupa idea [emoji362] [emoji362] moja ambayo hutopata tena

Dodoma kuna chuo kikwubwa kinaitwa Udom sasa chakufanya tengeneza Karanga za mayai then utembeze chuoni apo college adi college, block adi block, room adi room, we akikisha unatengeneza Karanga sichini ya miatano (500) hivyo ukiuza Karanga moja kwa miatano jumla zote utapata 250000

NB: minimtumiaji wa karanga izo sana hivyo sehemu nazonunuaga zinaishaga fasta tu wakireta zinaisha tena fasta kwaiyo soko lipo kingine nilimuhoji Dada mmoja hivi ambaye anauza hizi bidhaa alinambia kwamba yeye anauzauza college moja tu anayosoma hivyo kwasiku anaweza pata ata elfukumi nahuyu dada ajaifanya hii kazi serious kwasabu sijawai muona akipitisha room napoishi mimi hii inamaana ukifanya serious hii shunguri ndani ya mda mchache utapata mtaji wa kutosha wakufanya bossiness zingine kubwa
 
Mimi niko Dar mbagara Nzasa (charambe) nina laki 6 nifanye biashara ipi...... Nilitegemea matunda haswa embe dodo ila mwaka huu embe hamna kabisaaaa.
 
Ngoja nitoe kaushuhuda kadogo.
Nakumbuka mwaka 2013. Kaka yangu alinifata home akaniambia mdogo wangu nina shida ya pesa ya mtaji.
Nilishangaa sana nikamwambia mimi sina pesa ya Mteja kaka.Akaniambia nina wazo la biashara mtaji wake ni sh 50,000/= Nipe leo ndani ya siku 3 nitakurudishia sh 60000/=.Niwe mkweli mimi ni muislam nikamwambia hiyo riba, nilipe sh 50,000/-= kama unanipa sh 60,000/= unanipa kama mdogo wako. Pia nikampa sharti hii pesa nimeiweka niongeze , kwa ajil ya kulipa kodi akaniambia usijali wazo langu nimelifanyia kautafiti.

Basi nikampa ile pesa. Jamaa ajafanya ajizi kaenda kufanya michakato ndani ya siku 3 akanilipa ile pesa na +10,000/=

Toka mwaka 2013 hadi leo jamaa amebadil maisha yake.
Mwaka 2015 mwezi january kanifata home kipindi iko nimekaa mtaani sina kazi nimemaliza chuo ( 2013).AKaniambia mdogo wangu kuna milion 3 kama unawazo la biashara njoo uchukue ufanye utarudisha kidokidogo.
Nikawa natafuta wazo la biashara ili nisipoteza pesa za bro.milion 3 kubwa sana nisikurupuke nitaipoteza.Mungu mkubwa ndani ya muda huu nikapata kazi.nikamwambia kaka ebu ngoja nikapambane na jasho langu.Yeye sasa ana nyumba ,nimesema nyumba ya maana usifikiria kajumba na ana biashara imara hata mimi namuogopa

KWA NINI NIMESIMULIA HILI JAMBO.
  • Unapotaka kuanza biashara usiwaze kuwa na mtaji mkubwa ndio utafanikiwa
  • Wazo la biashara ni jambo kubwa sana linakufanya uwe huru kuendesha biashara husika
  • Utayari na kujitoa huleta mafanikio makubwa sana
  • Tuwe wavumilivu na uaminfu ktk biashara
Ni hayo tu.
JF ni mahali salama kupita mitandao yote ya kijamii Tz.Mungu ibariki /wabariki JF, Uongozi wa JF na wajumbe wa JF.
INSPIRED
 
Naomba msaada kwa mwenye uelewa wa biashara ya nafaka hapa Dar anijuze kuhusu upatikanaji wake na usafirishaji
 
Mie ni mwanafunzi but niliomba msaada kuhusu kusaidiwa nianzishe biashara ipi kwa mtaji Wa laki moja kwakua naitaji kufanya biashara huku bado naendelea na masomo naombeni mnipe ujuzi jamani
Nenda mtumbani nunua vinguo vizuri vya wadada... Fua, ikibidi pasi, halafu uza chuoni. Pitisha kila chumba huko hostel

Ina faida sana. Unanunua nguo elfu 2 unauza kuanzia elfu 10.

Nunua na chupi bei ya jumla, uza pia
 
Back
Top Bottom