Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Biashara ya chips mnaionaje
Ni biashara nzuri ambayo inalipa sana kama utasimamia mwenyewe. Tatizo mtaji wake ni mkubwa kidogo kulingana na pesa ambayo unayo
1. Kabati la kioo 200,000/=
2. Jiko la kupikia 90,000/=
3. Vyombo vidogo vidogo 80,000/=
4. Meza pamoja na viti vya kukalia wateja 150,000/=
5. Viazi debe mbili nadhani sasa hivi ni 24,000/= mafuta ya kula kindoo kidogo 30,000/= kama sijakosea
6. Pesa ya dharura 100,000/= kwasababu lolote linaweza kutokea
Jumla hapo tunapata 674,000/= hapo ni mwanzo na ukumbuke hujapanga frem.
Ila ni biashara nzuri tafuta eneo lenye watu wengi halafu pia upate mtu ambae anajua kupika chipsi nzuri pamoja na lugha nzuri,unaweza kughairi kuajiliwa utakapomaliza masomo yako.
Usimamizi mzuri ndio msingi wa mafanikio kwenye hiyo biashara
 


duh..kwa siku kilo 1?hujawah fikiria km unapata hasara..!kwann usibadilishe biashara?
 
Hi, ni biashara gani. Naweza fanya yenye mtaji wa laki tano mpka sita na inalipa pia nitaianzisha katka mzingira gani??????
Gawa mtaji, fungua genge huwa linalipa sana. Weka mahitaji muhimu tu kama nyanya, vitunguu, limao n.k , achana na matunda ,yatakupa hasara na yatakuozea gengeni ,wabongo hatuna utaratibu wa kula matunda mpaka tuumwe
 
Habari ndugu zanguni,nina rafiki yangu ameniomba ushauri kuwa ana sh 800,000/= na ataka kufanya biashara.je ni biashara gani ya laki nane anaweza kuifanya katika wakati huu?
Ndiyo ametoka chuo ila kutokana na changamoto ya ajira ameona bora afanye biashara.
Asanten.
 
Anapatikana wapi huyo rafiki yako na biashara anataka kufanya maeneo gani?
 
Mama lishe center tu nzuri aanze kazi kwa laki nne tuu uku anajazia iyo laki nne nyingine ifike milion nimshauri tena
 
Anapatikana wapi huyo rafiki yako na biashara anataka kufanya maeneo gani?
 
Mama lishe center tu nzuri aanze kazi kwa laki nne tuu uku anajazia iyo laki nne nyingine ifike milion nimshauri tena
Sasa c umalizie tu mkuu huo ushauri? Ili kama litamfaa ajue anaelekea wapi
 
Kwanza kabisa inatakiwa.......................Itaendelea kesho
 
Achague biashara ambayo ni rahisi kuingia au na rahisi kutoka bila kumgharimu sana.
 
Nina Tsh 400,000/= (laki nne) nahitaji ushauri nifanye biashara gani ambayo inaendana na pesa hii ili nipate faida nzuri. Sio lazima iwe biashara, inaweza ikawa kitu kingine chochote kile cha kunipatia pesa (faida).
Nipo Ubungo Msewe, Dar Es Salaam
 
Fanya biashara ya zao la Chia seeds,hapo ulipo popote nchini, mi nitakuuzia kilo 40 za chia seeds alafu wewe utauza kilo moja kwa bei ya chini tsh 20,000.sawa na faida ya 400,000.kwa mzigo wote maana utapata tsh 800,000=.
Hizo chia seeds ni seeds za zao gani na naweza kuziona kwa picha?
 
Nina Tsh 400,000/= (laki nne) nahitaji ushauri nifanye biashara gani ambayo inaendana na pesa hii ili nipate faida nzuri. Sio lazima iwe biashara, inaweza ikawa kitu kingine chochote kile cha kunipatia pesa (faida).
Nipo Ubungo Msewe, Dar Es Salaam
Nunua balo la mitumba grade AA mwaga nje ya eneo unapoishi.....wanunuzi watazifuata wenyewe,within a week utakua umepata faida mara mbili ya mtaji.

NB: Nguo za kike(skirts na top) au watoto miaka 1_12 zinalipa zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…