Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]kuna kampuni moja ha kukopesha.sasa hivi hawakopeshi wanasubiri walipwe Kwanza.
Na kila siku wanafungua ofisi ila hela ya kukopesha HAWANA ZOTE ZIPO KWA RAIA
Katika biashara kichaa ni ya kumkopesha mmbongo! Bora mkopeshane kwa dhamana ya mali ambayo ukiiuza unàrudisha chako mfano aweke bond simu 😁 hapo atalipa ila kwa maneno matupu tu eti tumekubaliana hivi!

Tena na kukuita msumbufu atakuita mbele za watu,,,utaskia "Eh bana huyu mxng msumbufu kweli yani ef 10 anapijapija simu kila saa 😂!" Lipa deni uone kama utasumbuliwa 😝
 
Mimi kumkopesha mtu aweke Bondi tuu ili awe anakumbuka kua Kuna hela ya watu anayo na anatakiwa kuilipa sio mtu unamkopesha alafu anasahau kua anadaiwa
 
Mimi kumkopesha mtu aweke Bondi tuu ili awe anakumbuka kua Kuna hela ya watu anayo na anatakiwa kuilipa sio mtu unamkopesha alafu anasahau kua anadaiwa
Hahah tena ya kitu muhimu ambacho hawez kubali kukipoteza. Unampa na grace period kabisa akifeli unasebenza. Uone kama hatapambana aje kukomboa haraka 😂
 
Hahah tena ya kitu muhimu ambacho hawez kubali kukipoteza. Unampa na grace period kabisa akifeli unasebenza. Uone kama hatapambana aje kukomboa haraka 😂
lazima atairudisha ndani ya Muda husika kwasababu inamuuma,sio mtu unamtafuta wewe Kama wewe ndo mwenye shida bana
 
Mkuu ungekuwa karibu tungejoin tufanye collable mana zile 5000+ zimeota mbawa🤣🤣🤣
 
Habar wapenzi msaada tutani Nina mtaji

wa Million 1 , naomba idea za biashara

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu nipo kimara Dar es Salaam
Nahitaji kufanya biashara ili niweze kukuza mtaji, je nifanye biashara gani?
 
Dah, huwa tunatofautiana sana, huu ujasiri wa kuuliza idea ya biashara baada ya kupata mtaji huwa mnaupata wapi wakuu, wengine plan zipo za miaka 10 mbele na kila hatua na strategies zake kufikia lengo kuu na hakuna pesa itakayoingia ikose pa kwenda au ndio ianze kutafuta pa kwenda.

Idea za bishara za ndoto zangu huwa naandika hatakama sina hata mia na nimeshindia uji ila siachi kuandika idea za biashara.

Mkuu hapa utapata idea nyingi, uza nguo na viatu vya kike, fungua genge la matunda na mbogamboga, tafuta computer used ufungue biashara ya kuweka nyimbo na movie, tafuta eneo zuri choma mishkaki na mengine pia

Tatizo huwa linakuja.

1. Utayari wako (moyo wako utaridhia na hiyo biashara kiasi kwamba hata ukipata hasara hutojilaumu?)

2. Uelewa wa kutosha kuhusu biashara husika (lazima kuna muda wa kutenga kupata dondoo muhimu za biashara husika na hapa usipotilia maanani lazima utakula hasara).

3. Pesa yako kweli ni ya mtaji au umekusanya na ukaamua iwe mtaji kwakuwa unaona inaweza kupotea tu bila kufanyia chochote cha maana? Hiyo pesa unaweza itunza mwezi mzima ukifanya research ya biashara utakayoipenda au ndiyo ile pesa ya matumizi ndani ikiisha huwezi lala njaa huku una laki 7 ndani ?? Ukipata emergency yoyote utakuwa mwepesi kuitoa hiyo pesa ?.

Najaribu tu kuonyesha namna gani ilivyo muhimu kuwa na mpango mzima kabla hata hujapata pesa ya kutekeleza mpango huo ili pesa ikiingia tu basi hushajua wapi inaenda. Pesa haikai mkuu.

Vuta subira ila jitahidi ufanye utafiti wa kutosha kuhusu biashara utakayoamua kuifanya kabla ya kuanza ili ukiingia ukubaliane na matokeo yoyote kiroho safi kabisa.
 
Mkuu PM namba yako ya WHAT'SAPP please [emoji120][emoji120], nna maswali mawili mafupi... thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…