mimi nina mchango mdogo tu
Watu waliosoma biashara wasisahau kukumbusha wajasiriamali wadogo angalau 4Ps , products,price,promotion and place
Ubora na uhitaji wa bidhaa zako (quality and need to be satisfied)
Bei ya bidhaa kama inaendana na uwezo wa wa watu , hua hapa ndo watu wengi wanakosea sana wanataka faida kubwa
Faida ya bei kubwa sana,utapata faida nyingi kwa kuuza vitu vichache
Hasara yake, utauza vichache mno maana budget za watu ni ndogo kwa hiyo wanunuzi utawapata wachache ,
Hapa ndo watu wanashindwa kujufanya makadirio yao na kuangalia mbele zaidi.
Na hua nimeona wafanyabiashara wengi wakicheza na wateja kama paka na panya ,so bad nani aweze kumshinda mwenzake ,tatizo wengi tunafanya biashara bila kujua malengo yetu ya faida .so bad hii
E.g.
Unauza blouse 2 kwa 6000 na mwingine atauza 3 kwa 4000,bidhaa ile ile
huyo wa anaeuza 4000, ataenda kuleta mzigo mwingine ww hujamaliza hata wa kwanza
watu wajifunze kujua wapi wata break-even especially unapouza uniform products
Kwenye biashara yako kumbuka inventory turn over ndo ita determine faida yako
Siku hizi watu wanafuga sana ,kwa nini watu wenye mitaji midogo wasiende vijijini wakalete pumba za mahindi , mashudu ya alizeti watauzia viwanda vya vyakula vya mifugo inalipa
Arusha najua watu wanaofanya hizo biashara ila ni wavivu tu, wakishusha mzigo wanapewa cash yao on the spot
Kwa nini usifanye