nicheki kaka ukikutana na ugumu oote...naeza shauri,au kabla ujamlipa nipe link za uyo supplier nimcheki then nicheki kwa simu nikupe namba ya forwarder...! usisite kiongozi sina malipo,labda niwe busy tu nikiwa na muda,tutashare uzoefu.
Kusoma
Dah nimejikuta nakesha nkisoma hii thred. Asante mkuu
Nimetuma link mkuu kwa PM pia naomba nitumie namba ya shipping company niwachek kujua price zao na vigezo.
Kwanza naomba nikushukuru sana kwa thread yako maana imenipa mwanga na ari zaidi, nilikuwa nina wazo la kuagiza bidhaa lakini nilikuwa sijui kwa kuanzia na pia nilikatishwa sana tamaa na bei nilizoona Alibaba na Aliexpress, uzi wako umenifumbua macho sana
MUNGU AKUBARIKI SANA
Naomba maelezo kuhusu haya yafuatayo
1. Nataka kuagiza bidhaa za vyakula kama toothpick, foil paper etc, naamini hapa TBS na TFDA wana husika kabla hizi bidhaa hazija ingia, kwenye maelezo yako umeongelea zaidi TRA lakini hawa jamaa hujaongelea, Je carrier atamalizana nao pia kama anavyo malizana na TRA au hawa itabidi nimalizane nao mimi?
2. Kama hautojali tuwekee hapa jukwaani contacts za silent ocean na Location ya ofisi zao za Dar
Natunguliza shukurani
tecno h6 inafaa mkuu?
Mkuu naomba msaada jana katika pita pita zangu aliexpress nimekuta bei ya bidhaa zikiwa in PIECE OR LOT sasa hiyo per peice nimekuta Nivea ikiuzwa dola 17.33 sawa na kama elfu 33,000 za kibongo sasa swali najiuliza hiyo bei anaposema per PEICE anamaanisha Dozen au Cutton au ndo ka unit kamoja..???
Mh! Mwalimu mwenyewe hata kuandika hajui. Kaaaazi kweli kweli!
insha-Allah...baraka na iwe nawe pia!Mwasalemba umenikuna mnoooo big up......
Allah akulipe
Mkuu naomba msaada jana katika pita pita zangu aliexpress nimekuta bei ya bidhaa zikiwa in PIECE OR LOT sasa hiyo per peice nimekuta Nivea ikiuzwa dola 17.33 sawa na kama elfu 33,000 za kibongo sasa swali najiuliza hiyo bei anaposema per PEICE anamaanisha Dozen au Cutton au ndo ka unit kamoja..???
xfactor umeeleza sahihi sana...naamini ndugu kakuelewa...labda nijazie mfano tu;muuzaji wa pen,dukani kwake pen moja anauza shilingi mia moja,lakini pen ioio kasema zikiwa tatu anauza mia mbili na hamsini...so lot ni fungu la pen tatu.Mara nyingi piece huwa ni unit moja, soma description zaidi kwa chini huwa wanatoa maelezo ya idadi ya lot, peace
Inategemea boss...
1.wasafirishaji wa maji wanakupimia kadri ya ukubwa wa kiboksi chako,hivyo yawezekana...nenda kwa ao jamaa ofisini kwao town,au chukua namba yao kwa instagram chat na jamaa mueleze ukubwa wa mzigo wako atakwambia gharama (natumaini supplier wako kakueleza uzito wake na dimensions zake)
2.au kama kidogo saaana huna aja ya kusubiri mwezi mzima wakati kuna wabeba vifurushi,kikubwa kubalance gharama za manunuzi nunua vitu vizuri lakini kwa supplier amabe yupo cheap zaidi au ambae gharama zake zipo na free shipping,manake nini?lets say umenunua bidhaa zako chini ya dola moja so ata ukija piga hesabu baadae gharama za usafiri kwa ndege ni sawa na kila item umesafirisha si zaidi ya dola 2 au 3,bado unakaa vizuri,kikubwa nenda pugu road waone aramex au skynet...dhl weka pembeni kwanza,unaulizia tu kwamba unamzigo wa uzito fulani watakupa gharama,alafu pia nadhan kuna option yakuweza kulipia uku,so ktk ofisi yao ya uko wata confirm tu uzito wewe utalipa uku.
3.njia ya posta ambayo nayo ni uhakika...na ipo kawaida sio bei juu wala sio chini lakini naamini inafaida pia.
Nakuwekea screen shot apa nimepiga kwa simu yangu...kama mfano;
Nimekuwa kama nataka nunua bracelet pisi 50
ambazo jumla yake pamoja na usafiri imekuja dola 68.80
68.80×1840=126,592/- (dola 1=tshs 1840)...hivyo bracelet 50 ni sawa na Tshs 126,592/-
126592÷50=2531.84,hivyo ni sawa na kusema kila bracelet moja ni Tshs 2531.84
Kumbuka kuna makato yakutuma io pesa wakati wa malipo,lets say kutuma io dola 68.80 utachajia dola 8-10,hii nayo lazima iingie katika manunuzi,so 10×1840=18400...18400÷50=368,hivyo ni sawa na kila moja ulilipia 368,so gharama za jumla ni 368+2531.84 =2899.84...hivyo adi inafika dar io bracelet takuwa nimenunua 2899.84 sasa wewe ukiuza kila moja elfu 8 adi 12 apo umekosa nini? ioio bracelet angalia watu apa bongo wanauza bei gani?adi elfu 15...okay poa boss
NB:kumbuka uo ni mfano tu,jewels za kike zipo nyingi sana.