Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Nimetuma link mkuu kwa PM pia naomba nitumie namba ya shipping company niwachek kujua price zao na vigezo.
 
nicheki kaka ukikutana na ugumu oote...naeza shauri,au kabla ujamlipa nipe link za uyo supplier nimcheki then nicheki kwa simu nikupe namba ya forwarder...! usisite kiongozi sina malipo,labda niwe busy tu nikiwa na muda,tutashare uzoefu.

Kwanza naomba nikushukuru sana kwa thread yako maana imenipa mwanga na ari zaidi, nilikuwa nina wazo la kuagiza bidhaa lakini nilikuwa sijui kwa kuanzia na pia nilikatishwa sana tamaa na bei nilizoona Alibaba na Aliexpress, uzi wako umenifumbua macho sana
MUNGU AKUBARIKI SANA

Naomba maelezo kuhusu haya yafuatayo
1. Nataka kuagiza bidhaa za vyakula kama toothpick, foil paper etc, naamini hapa TBS na TFDA wana husika kabla hizi bidhaa hazija ingia, kwenye maelezo yako umeongelea zaidi TRA lakini hawa jamaa hujaongelea, Je carrier atamalizana nao pia kama anavyo malizana na TRA au hawa itabidi nimalizane nao mimi?

2. Kama hautojali tuwekee hapa jukwaani contacts za silent ocean na Location ya ofisi zao za Dar

Natunguliza shukurani
 
Nimetuma link mkuu kwa PM pia naomba nitumie namba ya shipping company niwachek kujua price zao na vigezo.

Okay taicheki boss,lakini kama upo Dar nenda physically maofisini mwao, simu inaleta kidogo uzio na haipo friendly kwa hawa ma bwana. ..Kama upo mkoani inategemea na unachonunua kwani kama uzito wa mzigo ni mdogo basi tumia makampuni yanayotumia ndege kama aramex, skynet, DHL n.k so kabla hajatuma supplier wako atawauliza gharama watamjibu na atakufahamisha so utapima mwenyewe,kama kibiashara imekaa vizuri mpe go ahead lakini kama zigo kubwa basi usiumize kichwa peleka kwa wasafirishaji majini hapana shaka always gharama ni chini sana,so baada ya supplier wako kufanya delivery atakutumia risit ya ukubwa wa mzigo na watakuwa wameandika gharama ya kukomboa mzigo so mzigo ukiwa njiani uku unajiandaa na pesa yakuutolea mzigo.
 
Kwanza naomba nikushukuru sana kwa thread yako maana imenipa mwanga na ari zaidi, nilikuwa nina wazo la kuagiza bidhaa lakini nilikuwa sijui kwa kuanzia na pia nilikatishwa sana tamaa na bei nilizoona Alibaba na Aliexpress, uzi wako umenifumbua macho sana
MUNGU AKUBARIKI SANA

Naomba maelezo kuhusu haya yafuatayo
1. Nataka kuagiza bidhaa za vyakula kama toothpick, foil paper etc, naamini hapa TBS na TFDA wana husika kabla hizi bidhaa hazija ingia, kwenye maelezo yako umeongelea zaidi TRA lakini hawa jamaa hujaongelea, Je carrier atamalizana nao pia kama anavyo malizana na TRA au hawa itabidi nimalizane nao mimi?

2. Kama hautojali tuwekee hapa jukwaani contacts za silent ocean na Location ya ofisi zao za Dar

Natunguliza shukurani

Ni kweli sijagusia TBS na TFDA boss,sorry! Lakini hawa utakutana nao pindi tu utakapo amua kuingiza mzigo wewe mwenyewe bila kutumia wakala yani forwarder na sehemu nyingine utakayo kutaka na hawa mabwana ni dukani kwako pindi wanapofanyaga ukaguzi wao, so kwa kifupi mimi binafsi naweza kukili udhaifu wa hawa jamaa apa nchini kwetu kwa mtu mjanja mjanja zaidi hawatakaa mpata. ..kwani si kila mtu anaduka mtaani wapo wengi wenye store tu tena store za chimbo 'maficho' so kama utauza kwa Jumla Jumla ni ngumu sana kukubaini. ..labda itokeee siku katika watu wako mnaofanya biashara pamoja wakusemeee kwao.
Lakini pia ukitumia mawakala wa usafirishaji maanake wewe utakutana na mzigo wako godown yani stage ya ao mabwana bandarini kukukagua unakuwa ushaipita kwani msafirishaji wako anakuwa kaishamalizana nao so apa kuwa makini na msafirshaji makini hasa ambae amewamudu kwamba zigo lako litafika bila longolongo na msafirshaji ambae atafikisha kwa gharama nafuuu

Zaidi katika vitu ulivyotaja hapo juu tuliowengi tunavidharau sana na kuvisahau katika biashara lakini kama una mtaji mzuri amini nakwambia ni utajiri saaana coz kwa wenzetu ni chipu saaaaaaana, hongera umemeki choice nzuri sana.
Kuhusu namba na location ya silent naona kama hapa sasa itakuwa zaidi tunawatangazia biashara boss kazi, kuwataja kwa jina tu inatosha mwenye aja ya kweli atawatafuta,lakini kwa mwanga tu nenda IG wameweka kila kitu Chao.

Cheers.
 
tecno h6 inafaa mkuu?

Inafaaa saaana boss,kwani mbali ya kutumia simu katika mawasiliano kwa ndugu na jamaa itumie hivi

1 . KAMA JEMBE,yani iwe mahala ya chanzo cha uzarishaji kipato,fanya installation ya apps zote za masoko ambazo unaweza nunua bidhaa kwa jumla,mfano; aliexpress app,alibaba app,Amazon app etc
Hivyo itakusaidia kupata muda wakuona vitu/bidhaa mbalimbali mahali popote na sehemu yoyote katika io mtandao, so pakua picha za bidhaa unazopenda na mawasiliano ya muuzaji kadri uwezavyo,so download apps hizo na nyinginezo ziwepo katika simu yako;tumia email yako kusevu majina na hizo picha kwa usalama zaidi.

2.TUMIA KAMA DARAJA KUWAFIKIA WATEJA BILA JASHO,hivyo kimasoko ni nzuri pia coz badala ya kupanga sehem ya biashara fanya ofisi nyumbani unapoishi lakini huku ukiweka utaratibu jinsi ya kuhudumia wateja wako.

3.kwa mazingira yetu tumia masoko haya,amini nakwambia lazima uuze...facebook na magroup yake,IG,JF,WhatsAp na magroup yake,weka utaratibu wa kufanya delivery naamini utawafikia wengi zaidi...wanaoenda kwenye masoko kama kariakoo n.k ndio wanaoshinda humu humu na katika io mitandao,utauza tu meanwhile umetumia gharama ndogo na umekwepa gharama nyingi sana

4 . mengine wengine wataongezea boss maana wengi naamini ni wazuri saaana kwenye mambo haya,mimi nagusa tu juu juu lakini lengo upate mwanga
 
Mkuu naomba msaada jana katika pita pita zangu aliexpress nimekuta bei ya bidhaa zikiwa in PIECE OR LOT sasa hiyo per peice nimekuta Nivea ikiuzwa dola 17.33 sawa na kama elfu 33,000 za kibongo sasa swali najiuliza hiyo bei anaposema per PEICE anamaanisha Dozen au Cutton au ndo ka unit kamoja..???
 
Mara nyingi piece huwa ni unit moja, soma description zaidi kwa chini huwa wanatoa maelezo ya idadi ya lot, peace
 
Nashukuru mkuu. Ila kwa mwonekano ili uweze kununua bidhaa inahitaji upembuzi wa hali ya juu sana ili kupata bidhaa ambazo ni cheap ili utakapoagiza uweze kupata profit pia. Thank you very much.
 
mkuu mm mgeni. sana katika masoko ya mitandao. plz nisaidie naanzia wapi na niwe na nini na nini?
thanks
 
Jaribu kufuatilia thread hiyo tokea mwanzo jamaa ameeleza vizuri na kiuzalendo zaidi.
 
Mkuu naomba msaada jana katika pita pita zangu aliexpress nimekuta bei ya bidhaa zikiwa in PIECE OR LOT sasa hiyo per peice nimekuta Nivea ikiuzwa dola 17.33 sawa na kama elfu 33,000 za kibongo sasa swali najiuliza hiyo bei anaposema per PEICE anamaanisha Dozen au Cutton au ndo ka unit kamoja..???

mambo?Kiongozi...alibaba na aliexpress ni watoto wa baba mmoja,lakini mtoto alibaba ni maalumu kwa bidhaa za jumla jumla na mtoto aliexpress ni wa bidhaa za rejareja,so kibiashara tumia alibaba,kwani bei ni chini zaidi,lakini itumie aliexpress kujiupdate na new coming items yani kufaham nini kipo sokoni kwa wakati wa sasa...!
lakini all in all kuna siku ukipata suppliers wako sahihi unaweza kuwa unachukua picha aliexpress unawatumia wao then wao wanakutafutia kwa bei ya jumla n.k
 
Mara nyingi piece huwa ni unit moja, soma description zaidi kwa chini huwa wanatoa maelezo ya idadi ya lot, peace
xfactor umeeleza sahihi sana...naamini ndugu kakuelewa...labda nijazie mfano tu;muuzaji wa pen,dukani kwake pen moja anauza shilingi mia moja,lakini pen ioio kasema zikiwa tatu anauza mia mbili na hamsini...so lot ni fungu la pen tatu.
piece=1
lot=fungu
 
Inategemea boss...

1.wasafirishaji wa maji wanakupimia kadri ya ukubwa wa kiboksi chako,hivyo yawezekana...nenda kwa ao jamaa ofisini kwao town,au chukua namba yao kwa instagram chat na jamaa mueleze ukubwa wa mzigo wako atakwambia gharama (natumaini supplier wako kakueleza uzito wake na dimensions zake)
2.au kama kidogo saaana huna aja ya kusubiri mwezi mzima wakati kuna wabeba vifurushi,kikubwa kubalance gharama za manunuzi nunua vitu vizuri lakini kwa supplier amabe yupo cheap zaidi au ambae gharama zake zipo na free shipping,manake nini?lets say umenunua bidhaa zako chini ya dola moja so ata ukija piga hesabu baadae gharama za usafiri kwa ndege ni sawa na kila item umesafirisha si zaidi ya dola 2 au 3,bado unakaa vizuri,kikubwa nenda pugu road waone aramex au skynet...dhl weka pembeni kwanza,unaulizia tu kwamba unamzigo wa uzito fulani watakupa gharama,alafu pia nadhan kuna option yakuweza kulipia uku,so ktk ofisi yao ya uko wata confirm tu uzito wewe utalipa uku.
3.njia ya posta ambayo nayo ni uhakika...na ipo kawaida sio bei juu wala sio chini lakini naamini inafaida pia.

Nakuwekea screen shot apa nimepiga kwa simu yangu...kama mfano;

Nimekuwa kama nataka nunua bracelet pisi 50
ambazo jumla yake pamoja na usafiri imekuja dola 68.80
68.80×1840=126,592/- (dola 1=tshs 1840)...hivyo bracelet 50 ni sawa na Tshs 126,592/-
126592÷50=2531.84,hivyo ni sawa na kusema kila bracelet moja ni Tshs 2531.84
Kumbuka kuna makato yakutuma io pesa wakati wa malipo,lets say kutuma io dola 68.80 utachajia dola 8-10,hii nayo lazima iingie katika manunuzi,so 10×1840=18400...18400÷50=368,hivyo ni sawa na kila moja ulilipia 368,so gharama za jumla ni 368+2531.84 =2899.84...hivyo adi inafika dar io bracelet takuwa nimenunua 2899.84 sasa wewe ukiuza kila moja elfu 8 adi 12 apo umekosa nini? ioio bracelet angalia watu apa bongo wanauza bei gani?adi elfu 15...okay poa boss

NB:kumbuka uo ni mfano tu,jewels za kike zipo nyingi sana.

Yaaaaani nimekuelewa kupita maelezo.. Thanks boss
 
Back
Top Bottom