Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kanunue boat halafu piga ruti za ubungo zanzibar,chenji ikibaki tafuta ndugu yako mvumilivu mfungulie biashara ya kuuza matikiti na condomu
 
Mnaokejeli sio vema. Mtoa mada komaa na kilichokufanya upate hiyo laki sita endapo sio ya msaada, mkopo au dili za mjini.
 
Ukitaka pesa hiyo ikusaidie uza vitu vya akina mama vya bei rahisi
 
Tafuta sehemu ambayo frem rahisi fanya biashara ya vinywaji maji,soda na juice za cartoon anza na carton chache tu au uza duka la vyakula vibichi kama sembe,mchele,maharagwe kwa rejareja anza na gunia moja moja la kila nafaka
Kwa mtaji wake hii haitatosha
 
Nenda Ilala vizia wakifungua mitumba chagua mashati yaliyonyooka (sio Kwa kupiga pasi) piatia pitia watu wa maofisini...ndani ya miezi sita hiyo hela itakuwa imezunguka zaidi ya Mara kumi!
 
kama upo Dar na hauna aibu na una muda au mtu wa karibu mwaminifj,nunua zile ice box wanaita madeli mawili,kisha nunua mwamvuli na ununue vinywaji kama maji,soda na juice kisha umpe kijana carton moja kama faida yake.
jioni akuletee pesa ya hizo carton zilizobakia,
ni kabiashara kanakodharaulika ila ukiwa na nia unakuza mtaji,
Thadei Mushi
 
Last edited by a moderator:
Nenda Ilala vizia wakifungua mitumba chagua mashati yaliyonyooka (sio Kwa kupiga pasi) piatia pitia watu wa maofisini...ndani ya miezi sita hiyo hela itakuwa imezunguka zaidi ya Mara kumi!
Naunga mkono hoja
 
Nakuunga mkono. Ila tatizo vijana wanataka watajirike bila jasho. Napenda kumthibitishia mleta mada hiyo hela yake ni ndogo sana kwahiyo afanye mambo yanayowezekana na awe mvumilivu
 
Last edited by a moderator:
mkùu usiumize kichwa, hii ndio jf, fanya hivi, nunua tv ya chogo nch 21,ni laki na nusu, nunua deki simsung, inauzwa 50000, nunua mbao na chongesha mabench, tumia laki moja, utapata mabench kadhaa. zunguka mtaan, utaona tu kunanyumba nying tu zinauwanja wa wazi. omba kujenga banda la miti, huku ukiezeka kwa bati mbovu au makuti. mwambie mwenyenyumba utamlipa kod ya 20000 kwa mwezi. so kwa miez mitatu utamlipa 60000, jumla ya bajet kwa kadilio la chini utatumia laki nne.laki mbili nunua azam tv, inauzwa laki moja, na fundi akifuna atachukua 20000, so kwa jumla bajet itakuwa laki tano na nusu. anza kuonyesha video show, kwa siku onyesha mikanda mitano tu, kwa kila mkanda kiwango cha chini ni 2000, je ukionyesha mikanda mitano, unawakika wa 10000, kwa siku, so kwa mwez lakitatu kama tanesco hawajakata umeme. ni hayo tu
 

ushauri mbaya kabisa sijawahi ona,we unataka aishiwe na hicho kidogo alichonacho
 
kama upo karibu na madeleva wa bodaboda.

tengeneza kibox cha wavu wa chuma chenye ngazi tatu pamoja na myororo wa chuma ili kufungia akikisha unabagain na fundi chuma akutengenezee kwa bei isiyozidi laki moja na hamsini. kisha tafuta sehemu ya kuweka hilo box. nunua box moja la oil kwa sh 115000 na oil ya dumu kwa ajili ya kupima kwa sh 60000 pamoja na Dumu empty la Lita 30 hili utalitumia kwa kununua petrol.kisha ongea na muokota makopo ya maji awe anakuuzia makopo ya Lita moja na nusu Lita sio mbaya ukiongeza kiasi kidogo kutoka kwa bei anayouzia kwa kilo kwa wafanyabiashara ya kununua makopo. theni Pima oil katika kipimo cha Lita moja na nusu Lita pia petrol katika vipimo hivyo. pesa itakayobakia nunua spare ndogo ndogo kama Bolt nut. bulb za indicator, break pad na stika mbalimbali.

mchanganuo

box=150,000
oil za kopo=115,000
Oil ya kupima= 60,000
petrol Lita 30=66,000
spare ndogo ndogo=109,000

JUMLA=500000

Laki moja hifadhi ili ikusaidie pale majanga yakitokea

Mapato

Oil ya kopo 6,000*24=144,000
oil ya kupim 4,000*20= 80,000
petrol ya kupima 2,500*30= 75,000
spare (109,000)*1.75= 190,750
jumla = 489,750/=

kama kwa mwezi ukauza mizunguko mitatu kwa kila bidhaa

mauzo 489,750*3= 1,469,250
manunuzi 350,000*3=1,050,000
faida kabla ya gharama=419,250/=

gharama

usafiri 20,000*3=60,000/=
Chakula 5000*30=150,000/=
jumla ya gharama= 210,000/=

Faida kuu
419,250-210000= 209,250

Fanya biashara hii huku ukisave 200000 kwa mwezi baada ya miezi kumi tafuta fremu ya jirani na eneo lako fungua duka la virahinishi na spea ndogondogo pia nunua compressor ndogo ya laki mbili tafuta fundi pikipiki mshawishi ahamie mbele ya duka lako na wewe uwe unaziba pancha na kujaza upepo pikipiki na bajaji kama nguvu unayo ya kutosha ziba ata pancha za gari
 
Kama uko kwenye eneo unaloweza kupata hata robo heka ya shamba unaweza ukaanza na kilimo cha kisasa cha beans njegere utatoka mkuuu ndani ndani ya miezi mitatu tu utanipa matokeo ukiwa meno nje

Mkuu Mimi ninaeneo zaidi ya hilo nipe ujuzi huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…