Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Nashukuru mkuu kwa mawazo yako
 
Nilikosea kuandika bt namaananisha inategemea hyo sehem ipoje maana mjini huwa kuna competitions kubwa tofaut na interior
 
Inatosha kwa duka la vyakula dogo kama unaanza hakikisha mzani unao kisha nunua sukari,unga wa mahindi/ngano,maharage,dagaa kauzu(kigoma),mafuta na mchele afu kiasi kidogo kinachobaki nunua soda kreti,sigara,biskut,juice na nk mkeo utakua umemsaidia hatokuwa anapiga umbea kikubwa ajue bajeti tu mana biashara ya vitu vidogo faida zake ni ndogo kwahiyo ka ni mtumiaji Utakuwa unafanya kazi ya kanisa
 
mkuu usiumize akili kuukuza mtaji kwa haraka kikubwa fikiria changamoto zilizopo hilo eneo lenu KAMA ULIVYOSHAURIWA HAPO JUU weka products zile muhimu na consumable mfano unga mchele kiasi kiujumla nafaka zote kiasi plus mafuta ya kupikia
na usisahau kijigenge kidogo nje viungo vichache yaani mtu akija kwako asikose kitu wali au ugali ushaiva
 
Ni binti mwenye miaka 24 anayeishi kwa shemeji yake pamoja na dada yake. Elimu yake ni form 4 failure. Amedunduliza mpaka amepata hiyo laki moja na nusu. Anahitaji mchanganuo wa biashara ya kuanza nayo ili mtaji wake usimkate. Yupo dar maeneo ya tabata. Sio sister du. Anaweza fanya biashara yoyote. Kwa wale wazoefu tafadhari mchango wenu

=================================



================================

Naomba kujua kwa mtaji wa laki tano unaweza kufanya biashara gani?

 
Mtaji mdogo ndio mzuri tena atakuwa na nidhamu ya kutunz a hela, yeye aanze na vitu vidogo vidogo vile vinavyopendwa na watoto na akina mama,kwa hapo mtaji utapanda haraka sana.(2) Asione aibu ya watu awe kama amejitoa ufahamu,atafika mbali sana.Maana shida ni kupata kazi ila ukishaipata tu kazi hio hio italeta kazi nyingine. Nawasilisha ushauri wangu.
 
kama hujui wapi pa kuwekeza hutokuja kupata biashara ya kukutoa kwa laki tatu.. Alafu kwa mda mfupi.. Aliefanikiwa kufanya hivyo ni bahati na sibu tu... Cha kufanya rudi kwenye kazi au mishe ya kujishikiza ulipoitoa hiyo laki tatu iendelee kukuingizia kipato... Hiyo laki 3 igawe mara tatu, jaribu vitu vitatu tofauti, kitacho tengeneza faida wekeza tena, vingine achana navyo... Au gawanya mara 6 then wekeza vitu 6 tofauti vyovyote uwezavyo kuigawa hiyo hela... Kama ndo hela uliyonayo pekee ya kuwekeza usiiweke sehemu moja tena kwa ushauri utaopewa na mtu mwingine, utawekeza sehemu moja utafeli then utakufa moyo ya kufanya ujasiriamali...
 
Mimi nakushauri kama kweli unataka kufanya biashara kwenye laki tatu elfu 80,000/= nenda kwa fundi chonga kimeza kidogo tuu cha kuuzia urembo, 50,000/= nenda Machinga complex nje/Buguruni/tandika/Mbagala langi tatu stendi,Mwenge na maeneo mengine yenye watu wengi tafuta kigori.
Kisha nenda kariakoo hela iriyo baki unaweza jumua vitu vichache tu vya ulembo kwa kuanzia kutokana na eneo huskika halafu jifunze hapohapo wenzio wanafanyaje kwani wapo wengi na maisha yanasongo tuu hapa mjini
 
hiyo pesa nyingi sana mkuu ukikaza unatoka kabisa baadhi ya wadau wamechangia vizur naunga mkono kama vile genge mtumba ni safi sana pia kwa hapo g/mboto panda gari nenda maeneo ya masaki kule nunua nazi pia inakutoa mkuu
 
Follow african_products01 on instagram ujipatie masai cultural shoes za aina mbalimbali jumla na rejareja kuanzia sh.14000 kwa pair zaidi ya 20
 
Tafta watoto watatu nunua mayai trey Sita chemsa wape watembeze na wewe wa nne


Trey unanunua 6500 na kuuza 12000 faida 5500*2 =11000*4=44000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…