Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Biashara unachagua mwenyewe, jiulize biashara gani unaimudu ya hela hio
 
Habari zenu wana JF. Nina sh laki moja na nataka kuingia kwenye biashara. Jen ni biashara gani itafaa nianzishe kwa hicho kiasi cha fedha? Tafadhali naombeni msaada wenu.
Ebana laki moja ni ndogo kidogo, unaweza kufanya biashara ndogo ndogo inategemea uko Katiba mazingira gani na una connection zipi. Unaweza chukua mashirt, T-shirt, boxers, nguo za wadada , Sox za kiume, viatu vya mtumba vya wadada, kadet , skirt nzuri mtumba first clasa, jeans, nguo za office za mtumba, mashuka ya mtumba, pochi za wadada.. nk unachukua bidhaa kko au karume, then unatfuta soko unauza!! Kuna watu wanaishi hivyo miaka yote
 
Kwanza Weka Aibu Pembeni Maana Itakurudisha Nyuma. Angalia kama Upo Jirani na Shule, Vyuo au Njia Ambazo watu huwa wanapita au kukusanyika kwa Wingi. Fanya Mpango uwe Freelancer wa Mitandao yote ya cm, uwe una kazi ya kusajili line, kutengeneza special number, ku renew line, kuuza vocha n.k.

fight upate mwamvuli mf wa voda, chonga meza ya mbao ya kishkaji na kiti cha mbao, au kama vipo home vifanye viwe vya ofisi .

Ongea na Muuza magazeti jirani na wewe, akufanyie mpango nawe uwe wakala, tengeneza stand ya wavu ya chuma ambayo kwa ubavuni na juu kidogo utaweza kutenga eneo la kuweka pipi, biskuits, karanga, hankerchiefs, pen n.k

Tafuta Deli, tengeneza Maji na Juice za kupima, weka na barafu uwe unafaya biashara zako eidha jiran na maeneo ya njia panda, karibu na shule/vyuo, jirani na maeneo ya sokoni au kwenye mikusanyiko ya watu. Pia waweza omba nafasi mbele ya duka mfano la nguo ukaweka biashara yako huku ukawa unamlipa 500-1000 mwenye frem kila siku.

hapo nimekadiria upo home, friji lipo, blender, kiti meza pia unaweza vitoa home. otherwise gharama za mtaji zinaweza fika hata laki 2 au 3.

Mm nimewaza hayo, Mengine utajiongeza mwenyewe depending na mazingira uliopo. Kila la kheri.
 
Kwa mtaji huo tafuta baiskeli ya 50,000 na anza kutembeza maziwa kila siku kuanzia saa 11 asubuhi na kisha rudia kutembeza tena mida kama ya saa 12 jioni.Chakufanya uwe unalangua maziwa kwa wafugaji halafu unaenda kuuza ILA TAFADHALI HAKIKISHA FAIDA UNAYOCHUKUA HAIZIDI SH200 KWA LITA KWANI SIRI YA BIASHARA YA MALIMBICHI NI KUWA UKITAKA FAIDA KUBWA MAUZO HUWA MAGUMU!
 
Habari zenu wana JF. Nina sh laki moja na nataka kuingia kwenye biashara. Jen ni biashara gani itafaa nianzishe kwa hicho kiasi cha fedha? Tafadhali naombeni msaada wenu.
Kama hutajali uwe distributor wa dagaa,ambao hawana nchanga na tayari wamepikwa na spices na chumvi na wamo ndani ya vifungashio.
Shukran
 
Unatafuta distibutors? Ongeza information tuchangamkie fursa!
Kama waweza distribute tufanye biashara.. Ni wale dagaa safi,hawana nchanga,ambao wameshapikwa na viungo na chumvi,waweza kunywea chai,kwenye supermarket wanauza mpaka buku mbili jelo.
huanikwa kwenye vichanja tumewaweka katika vifungashio.
 
Pole mkuu. Have patience, atakuja tu mtu mwenye ideas [emoji362]
 
Unapendelea kufanya biashara, kilimo au ufugaji gani? na upo eneo gani?
 
Uza matunda kwenye vifungashio sambaza maofisini na vinywaji baridi (juice fresh)
 
Back
Top Bottom