joshydama
JF-Expert Member
- May 10, 2016
- 4,623
- 5,039
Pole sana kwa kupigwa Mkuu.Mi nina biashara ya Tigo pesa,nisikufiche laki 5 haitoshi kwa kuanzia hasa kweny upatikanaji wa line.Kwa mfano Tigo line utaipata kwa kwa 250,000,Voda 150,000,Airtel 100,000 hapo bado gharama za frem labda 50,000 kwa mwez miezi 6 ni 300,000 bado hela ya mtaji labda 500,000 iyo ni kwa sehemu ambayo ni ya kawaida ila wastani wa ela ya luz in gush is isipungue 1,000,000.Hapo umejibana sana bado vitu kama meza,simu za kazi,mazingira ya usalama kama vile mlango wa gril n.k.
Maelezo hayo yatawaidia wengi,sio aliyeomba kujulishwa tu.
Laini za Vodacom zinatolewa bure.
Cha msingi uwe na TIN NUMBER & BUSINESS LICENCE.