Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mawazo yangu.. Kwa mtaji kama huo unaweza Fanya biashara ya mashuka ya kuuza nguo za mtumba grade 1
 
Mtoa mada kama unaweza tafuta TILL ya m pesa ama tigo pesa utafute center uweke meza na mwavuli upige kazi kama kuna mzunguko utapata hela! hapo hapo uwe unasajili simcard za mitandao yoye hakika utapata faida sana nimefanya sana hiyo inalipa haina pressure
 
Nikupe deal ya ku sambaza dagaa kwenye ma supermarket ni wale dagaa waliopikwa tayari.
supermarket huuzwa buku mbili jelo
mie nitakuuzia bei ya kutupa
 
Mkuu ngoja nikupe kitu ambacho kipo humu jf, humu siku zote Wana zarau mtaji mdogo tena wengi wao ni wale ambao hawana dira ya nini cha kufanya ila wapo ambao wapo sensitive wapatakupa kile chenye maono. Kitu cha kufanya fanya utafiti kwa sehemu ambazo unatembelea hasa vijijin Kuna fursa nying Sana.... Embu jiulize mhindi na mwarabu ndo huwa na hii tabia ya kukimbilia vijijin Kuna nin kijijin,,,,,,?! Mbona mim na wew tunapakimbia lakin wagen wanapakimbilia..... Laki tano nikubwa Sana huko vijijin nenda kaangalie fursa huko ni kipi kinauhitaji mjini ambacho kipo huko shamba,.... Juzi nilikuwa huko nikakuta Lita ya maziwa n 500 na bado hayapati mteja lkn hayo maziwa mjini kikombe kinaanzia jero to buku,,,,,,, zipo nyingi sema mi c mwandishi mzuri ila kitu muhimu usikubali kukatishwa tamaaa na wachache ambao wanataka kupata buku lakin kashindwa kutumia akili ili apate hamsin na kila siku yeye anasubir kumbe ndo wenzake wanamuacha hivyo yeye kila siku kesho kesho
 
Mtoa mada kama unaweza tafuta TILL ya m pesa ama tigo pesa utafute center uweke meza na mwavuli upige kazi kama kuna mzunguko utapata hela! hapo hapo uwe unasajili simcard za mitandao yoye hakika utapata faida sana nimefanya sana hiyo inalipa haina pressure

Madam Mwajuma, samahan unaweza ukatoa ufafanuz zaid kwenye uendeshaj wa shughul za m pesa na tgo pesa kwa mtaj wa 500,000/=
 
Mi nina biashara ya Tigo pesa,nisikufiche laki 5 haitoshi kwa kuanzia hasa kweny upatikanaji wa line.Kwa mfano Tigo line utaipata kwa kwa 250,000,Voda 150,000,Airtel 100,000 hapo bado gharama za frem labda 50,000 kwa mwez miezi 6 ni 300,000 bado hela ya mtaji labda 500,000 iyo ni kwa sehemu ambayo ni ya kawaida ila wastani wa ela ya luz in gush is isipungue 1,000,000.Hapo umejibana sana bado vitu kama meza,simu za kazi,mazingira ya usalama kama vile mlango wa gril n.k.
Maelezo hayo yatawaidia wengi,sio aliyeomba kujulishwa tu.
 
Kama waweza distribute tufanye biashara.. Ni wale dagaa safi,hawana nchanga,ambao wameshapikwa na viungo na chumvi,waweza kunywea chai,kwenye supermarket wanauza mpaka buku mbili jelo.
huanikwa kwenye vichanja tumewaweka katika vifungashio.
Upo mkoa gani? Naomba masharti ya kuwa distributer wako.
 
Kama una TIN Namba, Leseni ya biashara laini ya Voda(TILI)utapewa bure Mkuu.

Kwa maelezo zaidi nenda vodashop iliyopo karibu na wewe.
 
me ni mwanafunzi na sina hivyo vitu je naweza pata? haraf zinapatikanakwa shiling ngapi?
 
Upo mkoa gani? Naomba masharti ya kuwa distributer wako.
Mjomba mie nipo Dar
Hakuna masharti
Mara zote napatikana katikati ya Jiji..nakuelekeza unakuja kuangalia sample . Tafuta masoko yako ,unanipa changu nakupa mzigo,hata hapohapo mbele yangu ukiuza kwa bei mara mbili haina kwere.
 
Mi nina biashara ya Tigo pesa,nisikufiche laki 5 haitoshi kwa kuanzia hasa kweny upatikanaji wa line.Kwa mfano Tigo line utaipata kwa kwa 250,000,Voda 150,000,Airtel 100,000 hapo bado gharama za frem labda 50,000 kwa mwez miezi 6 ni 300,000 bado hela ya mtaji labda 500,000 iyo ni kwa sehemu ambayo ni ya kawaida ila wastani wa ela ya luz in gush is isipungue 1,000,000.Hapo umejibana sana bado vitu kama meza,simu za kazi,mazingira ya usalama kama vile mlango wa gril n.k.
Maelezo hayo yatawaidia wengi,sio aliyeomba kujulishwa tu.
Acha kumtisha mwenzako lain za uwakala hutolewa buree kama wewe uliombwa hela ujue ulipigwa na wajanja Wa mjini.... Mathalani ili kupata lain ya uwakala yoyote inakubidi uwe na tin number , lesen ya biashara, barua ya utambulisho kutoka serikali za mitaa na kitambulisho chako chochote kile...

Narudia tena lain ya uwakala ni buree cha msingi aende kwenye ofisi za kampuni husika usiende kwa wahuni Wa mitaani.....

NB. Baada ya lain kuwa tayari utaombwa shilingi ambazo si choni ya laki tatu kutegemea na kampuni
. kiasi hicho kitawekwa kama float au mtaji Wa kuanzia kwenye lain yako...
 
Salamu kwenu wana jamii...
Kama heading inavyojieleza...
Ni biashara gani nayoweza kufanya kwa mtaji wa shilingi laki tano za kitanzania..?
Nahitaji mawazo yenu KAKA na DADA zangu wa jamii forums katika jambo hili..!​
Kulingana na hali halisi ya sasa mimi ninakushauri ujiunge na kampuni inayofanya biashara ya kusambaza bidhaa za afya na usafi pia kilimo. Laki 5 zinatosha kuanzisha biashara inayoweza kukupa faida ya laki 3 hivi kwa mwezi. So mimi nakushauri njoo tufanye wote pamoja, ni rahisi kikubwa uwe na dhamira ya kutoka kimaisha na uvumilivu.
Mawasiliano ni 0763797853
 
Back
Top Bottom