Biashara ya tumbo (chakula) ndio rahisi na inalipa chapchap.......mwisho wa siku jua linapozama unakuwa umejua mzunguko wako. Kwa kuanzia badala ya kuanza ku-invest kwenye capital expenditure, nakushauri tafuta mtu ambaye tayari anafanya biashara then ongea nae kama unaweza kuchangia mtaji halafu faida mgawane pasu kwa kipindi fulani cha mpito. Mfano cheki hawa jamaa wauza mihogo, maji, madafu, samaki, karanga, vitumbua, chapati, miwa, mahindi ya kuchoma nk mtaji wao kwa siku wengi huwa hauziki elfu hamsini. Kuwa mjanja kudadisi wanavyofanya biashara then ingiza wazo la kuongeza mtaji, then atakayekubali hapo utakuwa mwanzo wa kuzungusha hiyo laki kabla hujaimaliza kwa mama ntilie