Dah, huwa tunatofautiana sana, huu ujasiri wa kuuliza idea ya biashara baada ya kupata mtaji huwa mnaupata wapi wakuu, wengine plan zipo za miaka 10 mbele na kila hatua na strategies zake kufikia lengo kuu na hakuna pesa itakayoingia ikose pa kwenda au ndio ianze kutafuta pa kwenda.
Idea za bishara za ndoto zangu huwa naandika hatakama sina hata mia na nimeshindia uji ila siachi kuandika idea za biashara.
Mkuu hapa utapata idea nyingi, uza nguo na viatu vya kike, fungua genge la matunda na mbogamboga, tafuta computer used ufungue biashara ya kuweka nyimbo na movie, tafuta eneo zuri choma mishkaki na mengine pia
Tatizo huwa linakuja.
1. Utayari wako (moyo wako utaridhia na hiyo biashara kiasi kwamba hata ukipata hasara hutojilaumu?)
2. Uelewa wa kutosha kuhusu biashara husika (lazima kuna muda wa kutenga kupata dondoo muhimu za biashara husika na hapa usipotilia maanani lazima utakula hasara).
3. Pesa yako kweli ni ya mtaji au umekusanya na ukaamua iwe mtaji kwakuwa unaona inaweza kupotea tu bila kufanyia chochote cha maana? Hiyo pesa unaweza itunza mwezi mzima ukifanya research ya biashara utakayoipenda au ndiyo ile pesa ya matumizi ndani ikiisha huwezi lala njaa huku una laki 7 ndani ?? Ukipata emergency yoyote utakuwa mwepesi kuitoa hiyo pesa ?.
Najaribu tu kuonyesha namna gani ilivyo muhimu kuwa na mpango mzima kabla hata hujapata pesa ya kutekeleza mpango huo ili pesa ikiingia tu basi hushajua wapi inaenda. Pesa haikai mkuu.
Vuta subira ila jitahidi ufanye utafiti wa kutosha kuhusu biashara utakayoamua kuifanya kabla ya kuanza ili ukiingia ukubaliane na matokeo yoyote kiroho safi kabisa.