Kwa muda mfupi sana kiongozi wa Tanzania alipata maadui wengi sana

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Kwanza kabisa ni wanachama wenzake ambao walishazoea kupiga madili makubwa. Hawa walishazoea kukwapua mabil ya shilingi na wao huona kama wamekwapua shilingi elfu moja. Hawa walishamchukia sana kwa kuziba mianya yao ya upigaji.

Pili ni wanasiasa wa upinzani ambao baada ya kusambaratisha vyama vyao nao wakawa hoi kisiasa. Na vyama vyao vikwa vimeyumba kisiasa na kiuchumi.

Tatu ni wananchi ambao wengi walimuona kama kiongozi ambae ni dikteta hawa wengi walidai kupoteza jamaa zao au ndugu zao kwa kile kilichodaiwa ni watu wasiojulikana.

Nne ni wafanyabiashara ambao walizoea kuhujumu uchumi kwa kutengeneza bidhaa bandia, kukwepa kodi, wengi walikamatwa na kukwepa kodi na walikuwa magerezani kwa kuhujumu uchumi

Tano ni matapeli na wapigaji hawa walishazoea kulipwa mabilioni ya senti kwa kuwa na kampuni za mfukoni na walikuwa wakilipwa hata kama hawajafanya kazi.

Kwa ujumla kiongozi alikuwa na maadui wengii sana kwa muda mfupi.

Hivi ndivyo Africa ilivyo.
 
Wachina walikwenda hivi kwa miaka isiyopungua 20 na leo tunawaona wako hapa ila sie miaka 5 tu ndg yetu washamuwaisha ahera, haitatokea tukajitegemea watanzania na daima tutaendelea kutawaliwa na kuonewa. Tumechukua upande wa wakataa pema sasa pabaya pametuita rasmi
 
Motion ya huyo hayati wenu haikua na uelekeo wa kutupeleka uchina,ngoma ilikuwa inaelekea ZIMBABWE acheni kufananisha uharo na futari.
NIPO WAZI KABISA SIKUMPENDA JAMAA YENU HAKUWA KIONGOZI RAFIKI WA WATANZANIA.
 
Unasema huvyo kwa sababu hukuwahi kuguswa wakati wa utawala wa yule shetani. Mimi ni mhanga niligombea nafasi Fulani ndani ya chama Fulani tena ni chama cha wafanyakazi tu. Kilichotokea ni maajabu. Kwa kuwa walihisi nipo upande wa pili, nilitekwa nikalazimishwa kujiunga na upande wa kijani. Niliyoyaona huko sithubutu hata kumuomba dua yule kayafa. Mungu amlaze mahali panapostahili.
 
Hawa watakataa unayoyasema.

1. Wale waliopotea na waliopotelewa na ndugu zao katika mazingira tata
2. Wale waliochukuliwa mali zao kidhalimu na ma-task force
3. Wale walipelekwa magerazani kwa miezi na miaka kwa kesi za kubumba
4. Walipoteza maisha katika chaguzi kama Akwilina
5. Waliopoteza biashara kama Kwanza TV na Mbowe
6. Walionyang'anywa passports kama Eyakuze
7. Waliochafuliwa wanafanya biashara za madawa na kipendwa chake bashite
8. Waliopoteza kazi zao kwa mkono na niaovu kama Fatma Karume
9. Wakulima Ambao hawakupewa pesa zao za korosho
10. Waliobomolewa nyumba zao Kimara
 
China na Tanzania kisera ni ardhi na mbingu usifananishe china na vitu vya kijinga kabisa mkuu
 
Unasema huvyo kwa sababu hukuwahi kuguswa wakati wa utawala wa yule shetani. Mimi ni mhanga niligombea nafasi Fulani ndani ya chama Fulani tena ni chama cha wafanyakazi tu. Kilichotokea ni maajabu. Kwa kuwa walihisi nipo upande wa pili, nilitekwa nikalazimishwa kujiunga na upande wa kijani. Niliyoyaona huko sithubutu hata kumuomba dua yule kayafa. Mungu amlaze mahali panapostahili.
Uchaguzi wa chama cha wafanyakazi unahusiana vp na kua chama cha kijani?
 
Motion ya huyo hayati wenu haikua na uelekeo wa kutupeleka uchina,ngoma ilikuwa inaelekea ZIMBABWE acheni kufananisha uharo na futari.
NIPO WAZI KABISA SIKUMPENDA JAMAA YENU HAKUWA KIONGOZI RAFIKI WA WATANZANIA.
sijui una umri gani kiongozi,ila wewe ni kati ya watu wazima wajinga sana.

nyinyi wazembe wachache ndio matokeo ya tz hii ilipo zaidi ya miaka 50 ya uhuru.
 
Hawa watakataa unayoyasema.

1. Wale waliopotea na waliopotelewa na ndugu zao katika mazingira tata
2. Wale waliochukuliwa mali zao kidhalimu na ma-task force
3. Wale walipelekwa magerazani kwa miezi na miaka kwa kesi za kubumba
4. Walipoteza maisha katika chaguzi kama Akwilina
5. Waliopoteza biashara kama Kwanza TV na Mbowe
6. Walionyang'anywa passports kama Eyakuze
7. Waliochafuliwa wanafanya biashara za madawa na kipendwa chake bashite
8. Waliopoteza kazi zao kwa mkono na niaovu kama Fatma Karume
9. Wakulima Ambao hawakupewa pesa zao za korosho
10. Waliobomolewa nyumba zao Kimara
tunawezakuwa tunajadiri na kijana ambaye 2015 kushuka chini alikuwa hajazaliwa au hakuwa na ufahamu wa jambo lolote.

leo hii hayo uliyoorodhesha bado yapo,lakini sababu hutumii akili vizuri pia bado huwezi jua.
 
Wachina walikwenda hivi kwa miaka isiyopungua 20 na leo tunawaona wako hapa ila sie miaka 5 tu ndg yetu washamuwaisha ahera, haitatokea tukajitegemea watanzania na daima tutaendelea kutawaliwa na kuonewa. Tumechukua upande wa wakataa pema sasa pabaya pametuita rasmi
Well said kijana, naionea huruma Tz yangu tulikuwa tumeanza kupaa Sasa tumerudi tena ground
 
Wachina walikwenda hivi kwa miaka isiyopungua 20 na leo tunawaona wako hapa ila sie miaka 5 tu ndg yetu washamuwaisha ahera, haitatokea tukajitegemea watanzania na daima tutaendelea kutawaliwa na kuonewa. Tumechukua upande wa wakataa pema sasa pabaya pametuita rasmi

Mungu ameamua kufanya mabadiliko bila damu kumwagika, baada ya miaka mitano nchi yetu kuwa mikononi mwa shetani. Hakuwa na lolote jipya zaidi ya kiburi cha madaraka fullstop.
 
Propaganda haziwezi kumpaiza mtu yoyote. Subirini wajinga ndio muwalishe hizo propaganda. Yule alikuwa dhalimu sio zaidi ya hapo.
Udhalimu wake ni namna mnavyohisi kuhusika katika tukio la Lissu, Saanane na mnaodai walipotea? Au mnamhusisha na masuala gani ambayo unaweza kuyatolea ushahidi?
 
Back
Top Bottom