eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,214
- 15,853
Kwanza kabisa ni wanachama wenzake ambao walishazoea kupiga madili makubwa. Hawa walishazoea kukwapua mabil ya shilingi na wao huona kama wamekwapua shilingi elfu moja. Hawa walishamchukia sana kwa kuziba mianya yaou ya upigaji.
Pili ni wanasiasa wa upinzani ambao baada ya kusambaratisha vyama vyao nao wakawa hoi kisiasa. Na vyama vyao vikwa vimeyumba kisiasa na kiuchumi.
Tatu ni wananchi ambao wengi walimuona kama kiongozi ambae ni dikteta hawa wengi walidai kupoteza jamaa zao au ndugu zao kwa kile kilichodaiwa ni watu wasiojulikana.
Nne ni wafanyabiashara ambao walizoea kuhujumu uchumi kwa kutengeneza bidhaa bandia, kukwepa kodi, wengi walikamatwa na kukwepa kodi na walikuwa magerezani kwa kuhujumu uchumi
Tano ni matapeli na wapigaji hawa walishazoea kulipwa mabilioni ya senti kwa kuwa na kampuni za mfukoni na walikuwa wakilipwa hata kama hwajafanya kazi.
Kwa ujumla kiongozi alikuwa na maadui wengii sana kwa muda mfupi.
Hivi ndivyo Africa ilivyo.
Umesahau
Wauza madawa ya kulevya.
Majangili wa nyara za serikali, mfano meno ya Tembo.
Mashoga
Waliokuwa wanajiita mamesheni tauni (sijui kama nimepatia jina).
Michepuko ya wanene waliopangishiwa masaki.
Wazee wa bandari